Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2012
Posts
5,352
Reaction score
7,662
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
 
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu...

Hiyo gari ujimilikishi, unapewa, huu ujinga wa kutokujua utaratibu unawapaga hasara sana, wewe haujasajiliwa kufanya hiyo biashara.

Hata kama umeandika IGA jamaa wakorudisha hela hata mwakani gari lao utawapa, labda wawe waungwana.

Dai hela yako kama makubaliano, achana na magari ya watu, hasa wahalifu. Ngoja waje Police ccm wakuambie hiyo gari ilihusika kwenye mauaji ndo utaelewa.
 
Hiyo gari ujimilikishi, unapewa, huu ujinga wa kutokujua utaratibu unawapaga hasara sana, wewe haujasajiliwa kufanya hiyo biashara, hata kama umeandika IGA jamaa wakorudisha hela hata mwakani gari lao utawapa, labda wawe waungwana.

Dai hela yako kama makubaliano, achana nq magari ya watu, hasawahalifu.
Hata mimi sitaki magari ya watu mkuu, vitu vinabeba roho. So siwezi kujua ni kwanini wameniachia hili gari jipya kirahisi namna hii.

Aidha, kuhusu utaratibu wa kujimilikisha hilo gari ni rahisi sana, tena kwa utaratibu halali kabisa wa Kisheria, kuna kitu umechanganya ndio maana umezungumza kuhusu usajili, mimi siko huko mkuu.

Shida yangu kubwa ni hela yangu irudi kwenye biashara zangu.
 
Pesa ndogo iyo kwa Crown. Hao mafia ukiwadhurumu watakutafuta.

Cha kufanya, wakirudi hewani, wakulipe na riba.
Uko sahihi kwa sehemu mkuu. Ni kweli tunapoelekea kuna kutafutana kabisa.

Ila hapo kwenye riba ni labda wakubali kulipa kwa busara tu, kwasababu Kisheria sitoboi kwasababu mimi sio Taasisi ya fedha iliyosajiliwa kwahiyo siwezi kukopesha kwa riba kwani silipi kodi kwa biashara hiyo.
 
Hata mimi sitaki magari ya watu mkuu, vitu vinabeba roho. So siwezi kujua ni kwanini wameniachia hili gari jipya kirahisi namna hii.

Aidha, kuhusu utaratibu wa kujimilikisha hilo gari ni rahisi sana, tena kwa utaratibu halali kabisa wa Kisheria, kuna kitu umechanganya ndio maana umezungumza kuhusu usajili, mimi siko huko mkuu.

Shida yangu kubwa ni hela yangu irudi kwenye biashara zangu.


Okay.
 
Huwezi kujimilikisha gari, kwa sababu kadi haisomi jina lako; tofauti na hapo wanaweza kusema gari imeibiwa na kadi yake, na wewe ukawekwa ndani.

Cha kufanya, watafute wahusika; kama hawapatikani jisalimishe kituo cha polisi utoe taarifa, ili ikiwezekana wakupe nyaraka yoyote ile ya umiliki wa muda ili chochote kitakachokuja kutokea huko mbele uwe na pointi ya kuanzia.​
 
Hapo hujakopesha, bali umetoa msaada. Huna sifa za kukopesha, kwa sababu hujakidhi vigezo vya kuwa mkopeshaji.

Hiyo gari si yako, na wala hakuna mkataba wowote wa mauziano kati yako na jamaa. Wewe ni mtunzaji tu.

Haitoshi, wewe ni sehemu ya wizi. Kukubali kutoa rushwa ya fedha ili kumaliza kesi ya wizi wa gari. Kwenye huo mlolongo upo, na wakianza kutrack msururu wa washiriki, basi nawe huchomoki. Mkiwa pamoja naa hao polisi.

Nini cha kufanya?
.Usilete ujuaji, utajiharibia.
.Wasumbue wahusika wakuletee fedha zako.
.Mdhamini wao muangushie hilo zigo. Akutafutie Million 3 zako.
 
Huwezi kujimilikisha gari, kwa sababu kadi haisomi jina lako; tofauti na hapo wanaweza kusema gari imeibiwa na kadi yake, na wewe ukawekwa ndani...​
Kujimilikisha naweza kwasababu nina makubaliano (mkataba) ambao niliandikishiana nao kwa Wakili. Kitaalamu, kule TRA wakati wa transfer of ownership, badala ya mkataba wa mauziano, unawekwa huu mkataba wangu wa kukopeshana fedha kwa dhamana.

Mimi kukamatwa haiwezekani kwani nina mkataba ambao unaonyesha mmiliki halali ndio amenikabidhi gari lake kama dhamana yeye mwenyewe kwa hiari yake.
 
Rafiki yako alivokataa ulimwona mjinga? Anawajua vzr kuwa sio watu wazuri.

Itunze hio gari, Nina hofu kesi ya uwizi wa gari utasimama nayo
Kesi haiwezi kunipata mkuu. Nina mkataba halali ulioandikwa kwa Wakili ambao mmiliki halali anakiri kunikabidhi gari lake kama dhamana, tena kwa hiari yake yeye mwenyewe.
 
Kuna wakopeshaji wengine, ukiweka kitu bond basi wanakuendea kwa Sangoma.

Ukienda kutafuta hela hupati, mwishowe tarehe zinatimia na hujapata. Anachukua uamuzi wa kujimilikisha kwa bei kitonga.

Ila wanawaoataga wajinga tu.


Mimi sio mkopeshaji mkuu. Nimetoa hii hela kwa heshima ya mshkaji wangu tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom