Ni maneno mazito sana kumtamkia mtu hata kama amekukera kiasi gani, huna miadi na Mungu kwamba utatangulia wewe kufaulu na kama utakufa hicho kifo cha kuzikwa,
Wengi walifia majini wengine kwenye moto na wengine hawakuonekana kabisa, Kwahiyo ni maneno ambayo hayana msingi sana japo huelezea hisia za kweli za mtu kutokana na kukerwa kulikopitiliza
Wengi walishatamka maneno kama hayo na yakafanya kazi na kuleta madhara makubwa
Tujipe kuwa na subra na hekima neno ni kama risasi inapotoka imetoka hairudi, tuchague maneno ya kusema tunapoudhiwa na kuguswa hisia zetu za ndani
Kumbuka hekima ya mtu huonekana Wakati wa, kughadhibika na si Wakati wa amani au furaha
Tuna jukwaa zuri mno la cc tumo members wa kila aina mwenye maono na mitazamo tofauti , tujifunze kukubali mitazamo yetu kwa utofauti wale hata kama mingine inakera na kukarahisha
Na hii isiwe Hapa cc tu hata kwenye maisha yetu ya kawaida huko uraiani na kwenye mishemishe zetu
Niwatakie wikiendi njema afya na furaha tele wenu
Mshana Jr a.k.a baba Angel Ny..!
Stay bleesed