Nikaushe au niendelee kujipa moyo?

Quan Lup

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
640
751
Wakuu nina rafikia wa kike aliposting picha ya rafiki yake status whatsapp nikampenda nikamuomba namba akanipa.

Nikamtafuta nikamuambia fulani kanipa namba yako akasema poa, nikaa kama week nikamuomba tuonane akakubali tukaonana, tukafahamiana nikamueleza ya moyoni akaniambia nimekusikia nikamuambia sawa.

Tukaendelea kuchati vizuri saana as friend huku nikisubir majibu tukachati nikamuomba appointment akakubali , sikutokea, nikamuomba radhi akakubali nikamuomba tena nyingine akakubali bahati mbaya sana nikabanwa na majukumu sikutokea nikamuomba radhi akasema hakuna shida.

Baada ya muda akaanza kubadilika nikawa nikimtext hajibu au anajibu kwa kuchelewa, simu ndio kabisa hapokei. Nikaendelea kukomaa nikamuomba appointment akawa anagoma anasema yuko busy.

Siku ya siku akakubali nikaenda daah akaniambia, wewe unanijua mimi? Nikamuambia kiasi chake.
Akaniambia yeye ana mtu hawezi date na mimi, nikamuambia poa naheshimu maamuzi yako akasema poa. Nikasepa zangu.

Tokea hiyo siku sikuwahi mtafuta wala yeye hakuwahi nitafuta, ila cha ajabu ni kwamba kila nikipost status anakuwa ni wa kwanza ku view, yaani ni just now na ni zaidi ya miezi bado yeye anakuwa ni wa kwanza kuview status zangu, sijui anawezaje ni mara chache sana anakua sio wa kwanza.

Sasa hapa najiuliza ni kwanini sijui, ndio ame ni pin au, sielewi!
 
Kwahiyo hapo unaona anakukubali sana sababu ya kuwa wa kwanza kuview status zako? nakushauri achana na mambo ya status usipoweza punguza
Flz__TPXEBQ0QHo.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom