Kwenye mapenzi jitahidi uwe mvumilivu na mwelewa, usikurupuke soma kisa changu

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Kwema wana Jf

Mwaka huu january nilipataga demu mmoja hivi pisi kali sana wa Arusha nikamuomba namba akanipa .

Hapa nilikua sijawahi kuiona kabisa sura yake ila ni picha tuu na story tukawa tunapiga sana story nikamuelewesha akakubali tukawa wapenzi rasmi mahaba kama yote na video call.

Mwezi wa 3 nikamuambia nakuja arusha kwa ajili yako akaniambia karibu sana mimi nipo. Nikafunga safari za dar mpka Arusha kuonana na pisi nilkwa njiani tulichati fresh saana. Mpaka nafika Arusha tukawa tunachati nilifika alhamisi akaniambia tutaonana jumamosi kesho naenda kusuka nikamuambia poa.

Nikaa mpaka jumamosi maana pisi ilisema itakuja saa 8 mchana nikapiga simu hakupokea badae akanipigia nikamuambia mimi kesho napaswa kurudi dar maana j3 kazini akasema atakuja jioni nikasema poa.

Imefika saa 12 napiga simu haipatakani daah nikachoka nikamtumia message nikamuambia asante kukupenda imekua mateso kwangu kesho yake asubuhi nikapanda Tilisho nikarudi Dar.

Kwenye mida ya saa 8 mchana akanipigia simu uko wapi nikamuambia nakaribia dar akasema ni uwongo nikamuambia piga video call kweli akapiga akaamini akaanza kuomba msamaha na kulia nikamuambia mimi sina shida nimekusamehe akaniambia atakuja yeye mweyewe na atakuja kuniambia tatizo nikamuabia poa nikakata simu.

Yeye ndo akawa anapiga simu tuu na kutuma message terehe 20 mwezi wa 4 akaniambia anakuja dar kwangu na ataka siku 6 nikamjibu poa kweli bana tarehe 22 iddy akanitumia picha yupo kwenye basi anakuja aisee mood ikabadilika nikawa furaha sana.

Ilipofika saa 11 jioni mtoto nikampokea tabata segerea weeee ni hatari nikamkaribisha pale.

Baadaye alikuja kuniambia alipata tumbo la hedhi gafla na akaona hata akiniambia sitamuelewa basi yakaisha alikaa kwangu mpaka juzi jumapili ndo aliondoka.

Alikuja kwa nauli yake na kurudi kwa nauli yake mimi nilimpa elfu 40,000/tena kwa kumlazimisha alikua hataki now moyo wangu umemsamehe tunapendana tena.
 
Back
Top Bottom