Nikajifanya kumchanganya, akalikoroga zaidi…..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikajifanya kumchanganya, akalikoroga zaidi…..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 2, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nimetoka shule ya sekondari ya Pugu, ambako nilienda kumwona ndugu yangu anayesoma pale. Nakumbuka ilikuwa ni Jumapili mwaka 1999. Nilipanda basi kurudi mjini baada ya mazungumzo na huyo ndugu yangu. Wakati nikiwa kwenye basi, alipanda abiria mmoja ambaye alionekana kuutwika mtindi. Kwa Jumapili jioni, huwezi kushangaa kukuta mtu kautwika mtungi saa 11 jioni. Yule bwana kwa bahati mbaya akaja kukaa kwenye kiti nilichokuwa nimekaa.

  Alipokaa hakunisalimia, bali alinitazama sana, yaani kwa muda mrefu hadi nikakereka. Halafu alisema, ‘usinitishe bwana, kwani nimefanya nini. Kama mambo yalishaisha sasa kwani ni lazima uyaendeleze.' Nilishangaa, kwa sababu nilikuwa simfahamu na sikuwa naelewa anachosema. Aliendelea, ‘sikiliza afande, najua leo umenishika, lakini mambo si yalishaisha, hela zake nilimrudishia, basi kama unaona kunikamata ndio utafaidi, sawa nikamate niko tayari.' Sikumwelewa, lakini nilihisi kwamba ananichanganya na polisi fulani.

  Niliona nimchanganye tu na yeye. ‘Kwa nini ulizichukuwa hela zile?' Nilimuuliza. ‘Wewe mwenyewe unajua usawa wa nyumbani, ungekuwa hutujui sawa. Wewe mwenyewe unamchukua mamangu mdogo anakupa stori za homu, sasa unauliza kwa nini nilizichukuwa, si shida.' Niliona naanza kuadhirika kwa sababu abiria wengi waligeuka kumtazama huyo afande anayemchukuwa mama mdogo wa yule mlevi ambaye pia alishajitangazia kuwa ni kibaka. ‘Sawa, nimeelewa, yameisha, sina haja ya kukukamata.' Nilisema nikijua yameisha, kumbe yalikuwa ndiyo yanaanza.

  Aliniambia, ‘lakini afande wewe siyo mchezo. Mama yangu unamchukuwa, sista umebamba, haikutosha, mama Mona naye hukuachia, halafu yule demu mwenye grosari karibu na mtendeni shop ukabeba. Haki ya Mungu afande unaniacha hoi, unafagia...! lakini angalia ukimwi, angalia afande....!'
  ‘Kama usiponyamaza nitakukamata nikurundike ndani,' nilisema nikiwa nimekereka. Niligundua kwamba, mtu anaweza kufanya jambo kimzaha, likageuka hadi mwenyewe akalihisi kama ni kweli. Nilijuta kumjibu kwa kujifanya mimi ni huyo afande kweli.
  ‘Hapo sasa ndiyo sikuelewi. Wewe siri zako zikianikwa unatishia kuniaresti. Mimi nimesema ukweli tu, lakini unakuwa mkali, wala sijakosea wala nini, na wala sitamtonya mama mdogo kwamba wewe ni kifyagio. Kwanza nilipie nauli.' Alisema.

  Nilitoa nauli haraka na kumlipia. ‘hapo sasa sawa. Simwambii mama mdogo wala sista, wewe swaga tu, wanawake wa mjini nao wanapenda mkwanja sana...' Alisema na kusimama. Alikuwa amefika. Alishuka huku akisema, ‘lakini afande angalia, ngoma, kilo mbili hatari...' Abiria wote sasa macho yalikuwa kwangu. ‘Uzuri wa ulevi ndio huo,.. unampa mtu ukweli wake bila kujali,'abiria mmoja alisema. Sikutaka kujibu, sikutaka yawe makubwa zaidi.


  Hii kusema cha ukweli inanihusu mimi mwenyewe na wala sio rafiki yangu…………..LOL
   
 2. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,
  Pole na mwaswaibu hayo,
  Bora ungempotezea tu kuliko ulivyomjibu lol!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Shkamoo baba. Impersonation ni mbaya sana, mie mtu akinifananisha tu naruka kimanga futi 100.
  Sasa baba, zile nguo za mwaka mpya si unaleta leo maduka yameshaanza kufunguliwa?
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  pole Anko, umenichekesha leo..
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Yale maneno ya changu wa Kinondoni niloweka humu last week umemwambia mama yako, imekuwa taabu hapa nyumbani! hivi unatarajia kweli nikununulie nguo za za thikukuu
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hapi nyu iya ankoli mtambuzi..
   
 7. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  The the the the teh
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,122
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi heri ya mwaka mpya,
  pole pia na masahibu ya mvua,
  pole sana na hayo ya kibaka,

  Na mimi dada yako mkubwa uliniahidi kuwa mwaka huu
  utaninunulia shamba kule Bagamoyo,
  je ahadi yako unaikumbuka?
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siku zote ukiona mlevi jaribu kukae naye distance y ambali sana, mana hana akili, mwenye akili hawezi kwenda kununua ujinga.

  Ukikaa naye inabidi na wewe ukbali kuitwa mjinga.
   
 10. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  heri ya mwaka mpya ,... nafurahi mwaka umeanza na naamini utakuwa mzuri kwako na kusahau machungu ya 2011
   
 11. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hahaha mtambuzi leo inakuhusu ww nimekukubali.
  pole kwa maswahibu hayo mkuu.
  ila unajua kupanga maneno jaman , yan unaadithia had balaa loh.
  jiunge 2 na shigongo jaman.
  hapy new year mkuu.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hahahahahahaha pole, sipati picha ulivyojawa fadhaa siku hiyo,
  inawezekana alikuwa kweli amelewa au hakuwa na nauli akatumia njia hiyo
  mjini shule...
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nawasalimu tu, mtambuzi proposal yangu bado iko ON.
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu naomba unitumie makabrasha ya mswada wako niufanyie kazi
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kweli mjini shule..................
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Tangu tukio hili linipate, ujinga umenitoka..................... Na nimepunguza kihehere
   
 17. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Sasa kila mtu ana cheo chake wenye kuita Babu, Mjomba, haya nami naita Babu sasa tuone nani zaidi, baada ya hayo Pole sana Babu yangu.
   
 18. dazipozi

  dazipozi JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 1,143
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuma salamu kwa wa2 watatu
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,122
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  naomba niwe mmoja wa tatumiwa salamu,
   
 20. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,635
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  heri ya mwaka mpya mtambuzi...umenifanya nijisikie vizuri....kuna uzi mmoja kule kwenye Siasa wa akina ENL, RA,JKM umenitoa kwenye 'mudi' tangu jana. Asante mkuu!
   
Loading...