Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

Mkuu umenikumbusha mbaaali sana kwene hayo mabasi yenye kichogo chenye curve kule nyuma..dah, damn those good old days..

Public transport sio lazima mabasi tu, kuna tramways, trains, subways, barges/boats,etc..

Hii tuliita KUMBAKISA...ukizubaa tu inakukumba...baaadaye ikaitwa BAYANKATA

kha_ikarus280_yxa01693_20050215_r1.jpg
 
Baiskeli kwa Paris ni sawa kwa kuwa kuna baridi. Dar basikeli huwezi kutembelea, ni joto sana. Pia njia zenyewe za kuendeshea baiskeli ziko wapi>? Tupende tusipende, lazima tufanye OVERHAULD ya city plan kwa ujumla ndipo tuondoe tatizo kubwa la foleni.
Mkuu kama nyumbani au ofisini kuna uhakika wa kuoga, tatizo ni nini? teh teh teh .. tatizo la hili linchi ni kama limelaaniwa au lina gundu...

Matatizo lukuki, watatuaji hakuna..

Nways, cha msingi ni kubuni ufumbuzi based na resources tulizonazo.
 
Sasa kama anahamisha huduma kutoka katikati ya mji kwenda kwa watu, huoni kama CBD itakuwa GHOST CITY? Na kwa maana hiyo haina haja hata ya kujenga barabara/flyovers katikati ya jiji?

Ni options hizo....inasadikika kuwa asilimia kubwa ya wajao mjini hawana shughuli maalum zaidi ya shida zao binafsi na hizo ofisi za umma...mtu anatoka bunju kuja kulipia kodi ya ardhi magogoni...why?
 
flyovers za nini ! hebu fikiria tatizo la foleni bara2 ya Mndela kuanzia TABATA,HAPO NDIPO INAPOONESHA UPEO WETU MDOGO.
HIVI KUNA SABABU gani mtu anayetoka TABATAkwenda kariakoo,posta au muhimbili kupita Buguruni na ilala,BADALA YAKE INGECHONGWA BARA2 KUBWA IANZIE TABATA DAMPO HADI KIGOGO ,IUNGANISHE NA HII YA KIGOGO INAYOINGIA JANGWANI NA ZOTE ZIWE NA NJIA NNE,AFU BARABARA YA KUINGIA TABATA UKITOKA BUGURUNI INGILIE TABATA MATUMBI.
MAGARI YOE YA SEGEREA ,KINYERZI YANAYOTOKEA ILALA YAPITE BUGURUNI KWA MNYAMANI NA HIYO NJIA IPANULIWE IPASAVYO ,HAPAO UTABORESHA MAKZI YA WATU NA KUONDOA FOLENI BARA2 YA MANDELA MAENEO YA TABATA .
KUHUSU UBUNGO ,ILI KUONDOA MSONGAMANO RIVERSIDE ,ICHONGWE BARARA KUANZIA EXTERNAL INAYOKWENDA KIMARA AMBAPO MAGARI YA KIMARA NA MBEZI HAYATAHITAJI KUPITA UBUNGO
 
Spencer imetulia sana hiyo kitu,lakini barabara ya mwenge/bagamoyo nayo inatakiwa itanuliwe kuanzia mwenge hadi bunju,au ikiwezekana old bagamoyo road nayo iboreshwe.

Ujenzi utaanza mapema mwaka ujao. Sasa hivi wako wakandarasi wanahamisha nguzo za umeme, mabomba ya maji na waya za simu.
Barabara zitakuwa nne kuanzia Mwenge hadi Tegeta Kibaoni.
 
GreaTtHinkers;
Napenda tujadili suala hili la ujenzi wa Flyovers TAZARA na UBUNGO kama kweli litatua tatizo la fofeni za magari bila kupanua barabara au kuweka zingine mpya.
Kwanza maoni yangu;
Ningeshauri Serikali ione utaratibu wa kutumia Bonde la Msimbazi ambalo linaanzia Salender Bridge,Jangwani,Vingunguti hadi kinyerezi hadi Pugu japo njia NNE KWENDA TOWN/NNE KUTOKA TOWN,
Ningeshauri Serikali ione utaratibu wa kutumia bonde la Mto mzinga/Kizinga kuanzia bandarini,kurasini, mtoni mtongani na kwenda nje ya mji NJIA NNE KWENDA TOWN,NNE KUTOKA TOWN,
Ningeshauri serikali ione utaratibu wa Kuweka barabara NJIA NANE baharini kutokea Salender Bridge, kupitia magogoni posta ya zamani hadi kuunganisha na KILWA ROAD. Hayo majengo yaliyo upande wa baharini yanaweka kiwingu kisicho na maana.
Gharama ya Flyovers ni kubwa sana kwa maoni yangu na ingeza kufanya kazi nzuri zaidi kama watakuwa wako makini katika hili.:target:

Kwanza,Ondoa vipanya vyote na mabasi yabebayo less than 60 passengers.
Jambo ambalo Serikali ya CCM kamwe haiwezi kulifanya.

technologia ya kujenga Barabara za juu kwa juu ni rahisi tu kama tunajenga sisi Watanzania wenyewe, lakini kama tunaleta mgeni atujengee gharama zake ni kiama.
Kujenga madaraja muhimu kwenye vijito vidogo tu taabu kweli,sasa ni vipi tutaweza kujenga madaraja ya kujitakia?? Yaani kujenga daraja pasi na mto??
 
Jiulize kipi kintangulia....Huduma zinawafuata watu au watu wanafuata Huduma?????? Serikali ikipata jibu hili tatizo la foleni kwisha kazi..................
 
Sasa kama anahamisha huduma kutoka katikati ya mji kwenda kwa watu, huoni kama CBD itakuwa GHOST CITY? Na kwa maana hiyo haina haja hata ya kujenga barabara/flyovers katikati ya jiji?

yale maofisi yaliyopo pale samora, wayabadilishe kuwa hoteli, ila bei tofauti
 
GreaTtHinkers;
Napenda tujadili suala hili la ujenzi wa Flyovers TAZARA na UBUNGO kama kweli litatua tatizo la fofeni za magari bila kupanua barabara au kuweka zingine mpya.
Kwanza maoni yangu;
Ningeshauri Serikali ione utaratibu wa kutumia Bonde la Msimbazi ambalo linaanzia Salender Bridge,Jangwani,Vingunguti hadi kinyerezi hadi Pugu japo njia NNE KWENDA TOWN/NNE KUTOKA TOWN,
Ningeshauri Serikali ione utaratibu wa kutumia bonde la Mto mzinga/Kizinga kuanzia bandarini,kurasini, mtoni mtongani na kwenda nje ya mji NJIA NNE KWENDA TOWN,NNE KUTOKA TOWN,
Ningeshauri serikali ione utaratibu wa Kuweka barabara NJIA NANE baharini kutokea Salender Bridge, kupitia magogoni posta ya zamani hadi kuunganisha na KILWA ROAD. Hayo majengo yaliyo upande wa baharini yanaweka kiwingu kisicho na maana.
Gharama ya Flyovers ni kubwa sana kwa maoni yangu na ingeza kufanya kazi nzuri zaidi kama watakuwa wako makini katika hili.:target:

mimi nadha suruhisho ni kupanua huduma. Ukiangalia kwa sasa wakazi wengi wa jiji hukusanyika kwenye hot spot ndogo- yaani shughuli nyingi zinafanyika katika maeneo ya k،koo na kisutu, kitumbini hati kivukoni. Msongamano mkubwa unatokea wakati watu wana strugle kuingia mahali hapa. Kwasasa suluhisho lilenge kuona kuwa huduma muhimu zinapatikana pembeni ya mji kama kigamboni, pugu, kibamba na bunju. Lakini pia ni vizuri dsm ikafuta kabisa baadhi ya huduma na kuzihamishia mkoa wa pwani- mkuranga, kisarawe na b،moyo,mf: bidha kama mitumba ya aina zote ikihamishiwa huko itapunguza watu wanaohitaji kuingia city centre kwa huduma hizo.
 
Imekuwa ni adha na tabu ya kila siku kwa wakazi wa dar kutumia masaa mawili na zaidi kwenye misururu ya magari ambayo inachosha na kuharibu mipango mingi ya maendeleo,mimi nauliza hali hii mwisho wake lini au wanajamii hatuoni kero hii?
 
Tunasubiri pesa za 'wadhungu'! Budget yetu ni ya kula tu. Foleni zitaendelea to the next unforeseeable future!
 
Kwanini wananchi wenyewe tusichukue hatua? Serikali imekuwa inajivutavuta kwa muda mrefu sasa kiasi cha kwamba nia yao ya kukabiliana na tatizo hili inatia shaka. Pili halmashauri husika zimekuwa zinafumbia macho vitu vidogo vidogo kama vile matengenezo ya barabara hizi chache zilizopo hali ambayo imechangia kuongeza kero hizi. Halmashauri hizi pia zimebariki uchimbwaji wa mashimo/mahandaki eti ya kupitishia mikonga ya mawasiliano ya data kwenye barabara nyingi tu za jiji hili ambayo mpaka leo hii bado hayajafukiwa na hakuna dalili za kufanya hivyo. Na kabla haujakaa sawa kuna kodi ya amana za kudumu (property taxes) ambazo wakazi wa jiji mtakuja kutwangwa nazo muda si mrefu.

Njia pekee ni sisi wananchi pekee kuchukua hatua. Tuhame Dar es Salaam, tujijengee miji yetu mipya sisi wenyewe. Ila kwa hili serikali inabidi pia itusaidie mambo ya ardhi na upimaji wake. Haingii akilini kuona bei ya ardhi iko juu hata kwenye mapori kisa eti hayo ni mashamba ya watu. Kama mtu hauwezi kuendeleza shamba lako basi kuwa tayari kuliachia kwa manufaa ya umma.
Si lazima watu wote tuishi Dar es Salaam, hivi tukihama tutakosa nini?
 
Nadhan kuna umuhimu wa kuunda agency kwa ajili ya kuratibu mambo ya usafiri kwa jiji la dar es salaam!! Kwa kweli ilivyo sasa ni karaha tupu!! Tutalalamika hadi Tuone cha mtemakuni!! Kweli hali inatisha!! Ila ni muhimu sasa kwa taasisi zinazohusika ziweze kufanya Tathimini juu ya perfomance ya barabara hizi Chache tulizonazo, Kwa jitihada za Haraka ambazo nimezifanya binafsi, ila sina wa kuweza kumwakilishia kutokana na kutokuwa na chombo kimoja cha kushughulikia hayo matatizo, inaonekana barabara zote za Dar Zipo underperfomance,
Hii Imechangiwa na Yafuatayo
1. Uwepo wa shughuli Nyingi za kibinadamu Katikati ya barabara (Uuzaji wa icecreams na Wamachinga)
2.Kutokuwepo mipangiliao maalumu kwenye intersections, (Multiple U turns at Junctions - Ubungo junction)
3.Kutokuwepo vituo vya kusimama mabasi, Kulingana na idadi ya mabasi yanayotakiwa kuwepo hapo kituoni (Stand ya Mabasi ya Msasani na posta eneo la stand ya Mikoani)
4. Uwepo wa madereva wasiokuwa na haraka barabarani, ie. kuzingatia alama na sheria zilizopo!! (Hawa ni wengi na siku zinavyoendelea wanaongezeka)
5.Polisi wanaokuwepo kwenye junctions wapewe Stop watch ili waweze kufanya zoezi hilo kwa umakini na waache kufanya kwa Hisia zao Binafsi, Kwa mawazo yangu Hawa ni kero zaidi kuliko Manufaa!! Ningependelea Kama taa za kuongoza magari zinafanya kazi wao wangesimamia pendekezo numba 4. nakuacha taa zifanye kazi kwani ni more effective na fair.
Ya kwangu ni Hayo mwingine anaweza kuongezea

6.
7.
 
Hamna mpango wowte zaidi ya bodaboda kushika hatamu. Hata bajaji zitashindwa kuingia jijini. Hamna mpango!:A S cry:
 
Imekuwa ni adha na tabu ya kila siku kwa wakazi wa dar kutumia masaa mawili na zaidi kwenye misururu ya magari ambayo inachosha na kuharibu mipango mingi ya maendeleo,mimi nauliza hali hii mwisho wake lini au wanajamii hatuoni kero hii?

Yakika hali ya maisha ya wakazi wa Dar inakua mbaya kila kuchwao. Mambo ya kutoka nyumbani usiku na kurudi usiku yaanaiathiri si afya ya akili tu Bali hata afya ya uzazi. Tuko hatarini.
 
Bila kupanua barabara zilizopo na kuhakikisha ya kuwa barabara zote ambazo si rasmi zinapitaka muda wote swala la foleni Dar halitaweza kutatuliwa kwa muda mrefu ujao
Nadhan kuna umuhimu wa kuunda agency kwa ajili ya kuratibu mambo ya usafiri kwa jiji la dar es salaam!! Kwa kweli ilivyo sasa ni karaha tupu!! Tutalalamika hadi Tuone cha mtemakuni!! Kweli hali inatisha!! Ila ni muhimu sasa kwa taasisi zinazohusika ziweze kufanya Tathimini juu ya perfomance ya barabara hizi Chache tulizonazo, Kwa jitihada za Haraka ambazo nimezifanya binafsi, ila sina wa kuweza kumwakilishia kutokana na kutokuwa na chombo kimoja cha kushughulikia hayo matatizo, inaonekana barabara zote za Dar Zipo underperfomance,
Hii Imechangiwa na Yafuatayo
1. Uwepo wa shughuli Nyingi za kibinadamu Katikati ya barabara (Uuzaji wa icecreams na Wamachinga)
2.Kutokuwepo mipangiliao maalumu kwenye intersections, (Multiple U turns at Junctions - Ubungo junction)
3.Kutokuwepo vituo vya kusimama mabasi, Kulingana na idadi ya mabasi yanayotakiwa kuwepo hapo kituoni (Stand ya Mabasi ya Msasani na posta eneo la stand ya Mikoani)
4. Uwepo wa madereva wasiokuwa na haraka barabarani, ie. kuzingatia alama na sheria zilizopo!! (Hawa ni wengi na siku zinavyoendelea wanaongezeka)
5.Polisi wanaokuwepo kwenye junctions wapewe Stop watch ili waweze kufanya zoezi hilo kwa umakini na waache kufanya kwa Hisia zao Binafsi, Kwa mawazo yangu Hawa ni kero zaidi kuliko Manufaa!! Ningependelea Kama taa za kuongoza magari zinafanya kazi wao wangesimamia pendekezo numba 4. nakuacha taa zifanye kazi kwani ni more effective na fair.
Ya kwangu ni Hayo mwingine anaweza kuongezea

6.
7.
 
Hawana mpango wowote zaidi ya kupanga fedha za chai kenye bajeti za manisipaa na jiji,hivi Masaburi anaweza akatoka kifua mbele kama Meya wa jiji ambaye amshindwa kuongoza jiji kwa nyanja mbalimbali likiwamo la kupunguza makali ya foleni sasa hivi foleni ya Dar es Salaam ni all weather,yaani kutoka subuhi mpaka saa tano usiki,miji mingine foleni ni pick hours asubuhi,lunch time na jioni lakini sio Dar es Salaam,Mainjinia wa Manisipaa za Dar es Salaam,Mameya,wakurugenzi,mkuu wa mkoa wote wamekaa mata.......ko mbwata hakuna wanachowaaza zaidi ya kuchota pesa na kunnemesha matumbo yao,AIIIIIIIIIIIIIIIIIIBU kubwa kwa jiji la Dar es Salaam kila wakati tunaonekana hatuna heshima,hatujali muda kwenye kazi tunaitwa watanzania ni Lazy affair,mama mmoja aliniambia is not an offense but Tanzanians they have to check themselves on what is their priority becouse they seem not knowing what they want ,Halmashauri za jiji zinatakiwa zivunjwa kabisa hazitusaiidiii kitu
 
Back
Top Bottom