Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

duh huyu kanikumbusha mashiri enzi zile primary...

karudi baba mmoja
toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja
na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja ili kumtaka hali
.

nimesha sahau maneno!
 
duh huyu kanikumbusha mashiri enzi zile primary...

karudi baba mmoja
toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja
na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja ili kumtaka hali
.

nimesha sahau maneno!

wakataka na kauili iwafae maishani

akatamka mgonjwa ninumwa kweli kweli
................(kumbukumbu yangu ndo mbofu kabisa bora yako shostito)
 
ARE YOU SERIOUS......??? KITUNDA.....!!!!!!!!! Hakiyanani tena waleee jamaa wata-WIPE familia yako............. YAANI WEWE UNA FACILITIES ZOTE HALAFU YEYE AHANGAIKE NA MAYAI..............
am serious in the sense that hakuna sehemu dar utaishi uepuke foleni
foleniz are there to stay.......mpaka flyover za President zikamilike (lini vile??)
 
Anayefanya mambo mjini hapa yawe magumu anaitwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam. Nimezurura duniani sijapata kuona halmashauri ina roho mbaya kama halmashauri ya Dar es Salaam. Ni shetani kwelikweli, hatutakii mema hatutakii amani hatutakii pepo.
Hii foleni ipo kwa sababu :
-hakuna public transport ya kuaminika ambayo itafanya wanaotaka kuwahi maeneo yao wafanikiwe. matokeo yake kila mtu anataka kagari kake ka kumuwahisha.
-hawatengenezi barabara mpaka Ikulu iwatukane.
- mainjinia wake ni kama wale wa wakati wa Mwalimu Nyerere waliokataa kutengenezwa kwa kinu cha kufua umeme stigler eti kwa sababu wakati huo hawakuwa wanahitaji umeme, majitu malofa hayakufikiria karne ya 20 wala 21. Hawa walikuwa malofa wa akili na hawakuangalia mbeleni kuna nini.
-Wanawapa shida trafiki kwani kazi yao si kusimamia magari na kuyaamrisha kwenda kaskazini, kusini, mashariki na Magharibi.
-Maeneo ambayo yalistahili kujengwa madaraja ya juu kuondoa ghasia za msongamano wao ndio kwanza wanayashiti wanakumbuka kuuza maeneo ya wazi ,ili watunishe fedha zao kwa dai la kutafuta usasa.
-Wanatudanganya na mabasi yaendayo kasi wakati hata dalili hakuna .
-Wanatudanganya kutupatia usafiri wa treni posta mpaka tegeta kupitia ubungo kumbe wanatuzuga tu halafu kazi yao kukimbizana na wamachinga wanaleta majambazi na vibaka wengi mjini
-Foleni unaweza kuipunguza kwa akili ,lakini kwa kuitegemea polisi trafiki ni wazimu matokeo yake kuanzia Bendera tatu hadi mjini ni saa nzima wakati kutoka Mbagala mpaka Bendera tatu ni dakika 15.Serikali kuu imejenga eneo lake posheni iliyobaki ni ya halmashauri kufikiria namna ya kupunguza msongamano wanaiomba polisi idizani njia mbili penye njia moja huku ndio kwenda kibongo bongo,badala ya kufikiria kuwavusha watu bandarini ili waendao posta wakanyage na waenda Kariakoo wavuke kijireli chao. pale relini pamechoka hata kupakarabati ili magari yaende kasi hawaoni lakini kwa kuisaka kodi hawajambo.
sijui niendelee kuelezea tatizo la foleni nikiendelea utadata wacha nieachie hapa
 
kuna mipango miji wa kila wilaya, tangu uhuru, hakuna vision ktk kazi zetu, kama mipangowangetimiza wajibu wao tangu baada ya UHURU bila shaka, leo watu wakipawa wasingekua kwenye udhalili wa kiwango kile, watu wakigamboni wasingefikia hapo walipofikishwa leo.
nakubaliana nawe kuwa kuna mengine ni ya kitaalamu, tatizo yanaamuliwa kisiasa zaidi.
hatuna sera ya pamoja ya taifa katika kutimiza wajibu wetu, kila mtawala anakukuja na porojo zake.

Trust me, hao mipango miji sijui wapanga transport system., they are simply annoying pieces of losers wanaosubiria kubusu makalio ya wanasiasa ili next time wapate safari wale per diem na n.k. Tatizo kubwa la Tz ni MFUMO WA UTAWALA MUFLIS.

Kama kungekuwa na system nzuri nakuhakikishia mambo yangesoea kuanzia juu mpaka chini. Usitegemee watu mipango miji wapange miji wakti hakuna mipango ya kueleweka kuanzia juu. Kumbuka wao sio independent, wanawategemea watu wengine ktk kujiendesha. Usitegemee transport system zitakuwa in place wakati kuna utawala wa kisiasa usiojali techinicalities za ishu zenyewe. Trust me usione nchi nyingine watu wanaendelea ukadhania walianza with EXCESS never.


Walikaa chini wakapanga mikakati kidogo kidogo na wakaifuatilia up to the bottom. Wahenga walisema usione vyaelea. ..Sisi na watawala wetu mediocre, mipango mediocre we are doomed to die poor mpaka mwisho wa dahari, iwapo hatutabadilisha mfumo wa kujitawala.
 
ishi upanga.
hospitali aga khan
sokoni kisutu..
ofisi sokoine.
mazoezi gymkhana
starehe movenpik
shule watoto aga khan mzizima.
 
njoo uishi kijijini kwetu ,maisha tunategemea zaidi kilimo pesa zako huna haja ya kuweka benki utazichimbia chini na balance utaweka chini ya mto kwa kununulia mihogo,karanga ,maharage,maboga,usafiri tunatumia baiskeli zaidi ,hospital zipo za kata lakini hakuna vitanda feel free kujiunga na maisha yetu ya uswazi,
 
njoo uishi kijijini kwetu ,maisha tunategemea zaidi kilimo pesa zako huna haja ya kuweka benki utazichimbia chini na balance utaweka chini ya mto kwa kununulia mihogo,karanga ,maharage,mmabogakisa

kijijini kwenu wapi?
hulali wewe?
 
ishi upanga.
hospitali aga khan
sokoni kisutu..
ofisi sokoine.
mazoezi gymkhana
starehe movenpik
shule watoto aga khan mzizima.
inapendeza, lakini ni maisha ya kufikirika tu hayo.
 
Swali lijamvini
Mawazo nisaidieni
Nimezidiwa wajameni
Hili jambo laniudhi

Kila upitapo watu kibao
Kila uendako watu kibao
Hakukosea aliyeimba hivyo
Mchizi Mox heshima kwako

Hospitalini foleni
Sokoni foleni
Barabarani foleni
Nitajie pasipo foleni

Pesa zangu zibenki
Nikizitaka kwa foleni
Nakaishi wapi Dar hii
Nikimbie hizi foleni

Foleni zanikuta
Kwa kuwa nashi Dar
Hapa foleni imezaliwa
Mikoani imezikwa

Najua foleni ni sawa
Uungwana kwa waloendedelea
Kwani watu si wanyama
Foleni huleta usawa

Lakini foleni ikizidi
Uvumilivu huwa majaribuni
Na hatari iliyopo
Ni watu kuwa kama Popo

Naomba niishie hapa
Muda wangu umeisha
Niendako ni mbali
Wacha niwahi foleni

hujasema uwezo wako kifedha....unaweza kuishi popote na ukaepuka hizo foleni
just get urself a CHOPPER(u can get one for around £100,000 cheaper than PORSCHE 911 GT)
 
hujasema uwezo wako kifedha....unaweza kuishi popote na ukaepuka hizo foleni
just get urself a CHOPPER(u can get one for around £100,000 cheaper than PORSCHE 911 GT)

Hiyo Chopper itatua wapi?
 
Bunju na kazi yako iwe ni kulima matikiti maji na sisi wakulima tuwe tunakuja kununua huko shambani kwako!

hii inaweza kunisaidia, ngoja nijifunze ujasiriamali...maana kwa sasa i still work for money....
 
au kitunda kabisa ajiwekee na facilities zote nyumbani kwake

kitunda kuna foleni ya hovyo sana kutokea airport pale njia mbili zina-converge mpaka banana. unaweza kutumia dakika 10 kutoka tazara ukishavuka taa mpaka kufika hiyo sehemu...umbali wa kama km 5 au 6 hivi na pale penye kama km1 au 1.5 ukatumia dakika 30...

na hizi facilities ni pamoja na kuomba ofisi nilikoajiriwa ihamie home au??????
 
njoo uishi kijijini kwetu ,maisha tunategemea zaidi kilimo pesa zako huna haja ya kuweka benki utazichimbia chini na balance utaweka chini ya mto kwa kununulia mihogo,karanga ,maharage,maboga,usafiri tunatumia baiskeli zaidi ,hospital zipo za kata lakini hakuna vitanda feel free kujiunga na maisha yetu ya uswazi,

asante first lady....

Kwanini naishi Dar
Mimi ni mwajiriwa
Newe wajua nje ya Dar
Ajira ni haba
 
Back
Top Bottom