Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

kitunda kuna foleni ya hovyo sana kutokea airport pale njia mbili zina-converge mpaka banana. unaweza kutumia dakika 10 kutoka tazara ukishavuka taa mpaka kufika hiyo sehemu...umbali wa kama km 5 au 6 hivi na pale penye kama km1 au 1.5 ukatumia dakika 30...

na hizi facilities ni pamoja na kuomba ofisi nilikoajiriwa ihamie home au??????

yap!!! pamoja na huduma za afya benki, elimu na kadhalika!!!
unawatumia kazi zao kwa email tu (sasa kama kazi yako inauhitaji uwepo wako mie simo)
 
Njoo uishi k/koo ndo suruhisho la foleni. Maana kila kitu utakipata huwezi kumbana na foleni. Ukitaka chumba nione.
 
Nje ya dar patakufaa..Say Dodoma, hamna foleni kama za dar..Maisha siyo ghali ukilinganisha na dar! Labda vumbi na upepo mkali vikuchanganye..
Kama unataka dar hamna jinsi foleni huiepuki..Dar bila foleni haiwezekani!..
 
wakataka na kauili iwafae maishani

akatamka mgonjwa ninumwa kweli kweli
................(kumbukumbu yangu ndo mbofu kabisa bora yako shostito)
hata kama nikichanjwa haitoki homa kali;
roho naona yachinjwa kifo kinanikabili;
semeni niseme nini.........................
 
Nenda kokote mbali ila usiugue wala kuwa na shida mjini, unalo!
 
yap!!! pamoja na huduma za afya benki, elimu na kadhalika!!!
unawatumia kazi zao kwa email tu (sasa kama kazi yako inauhitaji uwepo wako mie simo)

...we bht wacha maskhara....tanzania hii au nyingine...
 
Nje ya dar patakufaa..Say Dodoma, hamna foleni kama za dar..Maisha siyo ghali ukilinganisha na dar! Labda vumbi na upepo mkali vikuchanganye..
Kama unataka dar hamna jinsi foleni huiepuki..Dar bila foleni haiwezekani!..

....aah Belinda kweli....ikiwa Tanzania na joto hili bila malaria inawezekana courtesy mkuu wa inji hii....itakuwa foleni jamani....
 
Nenda Kaishi Kigamboni, foleni utakayokutana nayo ni ya kusubiri panton tu hakuna foleni nyingine
 
Dar es salaam ,Dar es salaam,Dar es salaam!!!!!
Lini utakapokuwa ni mahali patulivu kimbilio la watu lenye kuleta faraja?
Foleni wewe!
Uchafu wewe!
Joto wewe!
maisha magumu wewe!
jamni Dar es Salaam! Nakumbuka miaka hiyo ya Tisini ulikuwa binti Mrembo sana mwenye kutamanika na kila mtu.Ona sasa umepoteza urembo wako woooote.Masikini Dar,Mafataki wamekuharibu uzuri wako wote.Hutamaniki tena wala hupendezi.
 
Usiende kabisa hizo sehemu zenye foleni piga simu uletewe- door to door service!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hizi ndio gharama za kuwapa watu wasio na akili wawe viongozi wetu. Tumeikubali system yetu mbovu ya utawala na sasa tunakula matunda yake. Kama tungekuwa tunao mfumo wa kuongozwa na wataalamu badala ya wanasiasa (ambao kimsingi hawana technical abilities za kutatua matatizo ) tungekuwa at least a middle class society with promising future.

As I see it now, makazi holela yanaongezeka, miundombinu hakuna, hii ni ground for further creation of slums. Inashangaza nchi yenye ardhi kubwa kaa Tz inakuwa na slums kana kwamba tu Rwanda ua Urundi with land shortages and highest population densities. THIS IS CRAZY and shows our STUPIDITY.

Nway, inasikitisha kuwapo ktk dying nation like TZ. 100% hopeless.

Bid up! What you are saying is true!
 
karibu kigamboni...foleni ni wakati wa kuvuka tu....anyway..daraja litajengwa November 2010,inshallah
 
Swali lijamvini
Mawazo nisaidieni
Nimezidiwa wajameni
Hili jambo laniudhi

Hili nalo laniudhi
Lawahusu walanchi
wapitapo wao kwetu maudhi
Nasema kweli si ajizi

Tazama wapitapo
Vimulimuli mbele yao
Vingine nyuma yao
Wao foleni si tatizo

Shida ni kwamba
wapitapo kwetu karaha
foleni kuzizidisha
kututesa kama manamba

Kuna ndugu amesema
Hapo juu akichangia
Pengine nitumie chopa
foleni kuiepuka

Hakika ushauri kuntu
Nami nimeuhusudu
lakini sina thubutu
kwani uchumi ni butu

Asante kwa ushauri
wa kuishi kwa raisi
lakini raisi si mshikaji
si kila mtu amjali

labda nami nishauri
hasa kwa mkuu wa nchi
ikiwa atatumia chopa
foleni atatupunguzia
 
Jamani tutafakari juu ya hizi foleni za asubuhi,mchana,jioni!
Tunashukuru kwakuchaguliwa Mh, John Pombe Magufuli,na zaidi Wizara imepunguziwa mjukumu ili iwezekufikia malengo yake swali je Waziri mwenye dhamana ataleta ufanisi??
 
Back
Top Bottom