SolarPower
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 223
- 27
any way ni mawazo nayo
tusiogope mabadiliko kwa faida ya wengi na taifa kwa ujumla.
any way ni mawazo nayo
natumia mobile, mlioko kwenye pc naombeni mnihakikishie kuwa hii thread ipo kwenye jukwaa la jokes.....
ni muhimu ukaniomba radhi kwa kauli yako hii.
Unless uwe unatania au unataka kuongeza posts tu,hili wazo lako SolarPower ni la kichekechea zaidi. Inajulikana wazi kabisa kuwa tatizo la foleni Tz ni barabara zake kuwa ndogo au finyu,kiwango/ubora duni, chache na sababu nyingine kibao. Barabara ziboreshwe na zipitike kwa urahisi,channels ziongezwe na wadau wali-suggest uwepo wa flyovers inapobidi. Nway kwa vile umetoa wazo,basi ngoja tulichukulie kama wazo tu!!
Sitanii bali namaanisha hicho nilichokiandika. Ni muhimu sana kuongeza bei ya mafuta kwa gari ambazo si za abiria na mizigo. Hayo uliyoyasema yatafuata baadaye kwani utekelezaji wake si wa leo au kesho. Pia si lazima tuanze na bei hiyo niliyopendekeza. Hata kiwango cha shilingi 5,000/= kwa LITA MOJA ya mafuta kwa gari zisizo za abiria au mizigo kinaweza kuwa kizuri kuanza nacho na kupima matokeo yake ndani ya miezi sita.
Kati ya mawazo negative... Hili linaweza likaongoza!
Fikiria vizuri ndugu yangu kabla ya kupost topic,wewe mwenyewe unajua kuwa mafuta yakipanda kufikia hiyo bei uliyoitaja vitu vyote hapa nchini vitapanda kuliko maelezo.
tusio na magari binafsi wakati mwingine tuna hasira!!!!Sitanii bali namaanisha hicho nilichokiandika. Ni muhimu sana kuongeza bei ya mafuta kwa gari ambazo si za abiria na mizigo. Hayo uliyoyasema yatafuata baadaye kwani utekelezaji wake si wa leo au kesho. Pia si lazima tuanze na bei hiyo niliyopendekeza. Hata kiwango cha shilingi 5,000/= kwa LITA MOJA ya mafuta kwa gari zisizo za abiria au mizigo kinaweza kuwa kizuri kuanza nacho na kupima matokeo yake ndani ya miezi sita.
Wala si wazo HASI bali ni wazo zuri katika kutusaidia wote. Naona wengi mnaogopa kutumia usafiri wa umma. Hatuna njia lazima tufikie huko.
tusio na magari binafsi wakati mwingine tuna hasira!!!!
hahahaaaaaaaaa nadhani wenye magari madogo wote watabadilisha usajili wa magar yao from binafsi mpaka taxi ili walipe bei ndogo kwa mafuta.
Mheshimiwa Solar Power Je, huo usafiri wa umma uko wapi? Ni huu wa watu kusubiri saa kadhaa vituoni bila kujua watafika lini kazini au kurudi makwao saa ngapi? Je, ni huu usafiri ambao watu hupitia madirishani badala ya milangoni ili kuwahi siti? Kama ni huu basi wazo lako haliwezi kutekelezeka asilani.
Bei ya Lita Moja ya Diezel na Petrol kwa Gari ambazo si za ABIRIA IWE SHILINGI 12,000 KUANZIA TAREHE 01 JUNI 2011.
Nadhani kuna watu huwa wanaamka na ndoto..na kukurupuka..Anyway, hii inaitwa changamsha baraza kwa wale waliokata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha kama sisi watanzania..Unashindwa kufikiri utakula nini kesho kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha ikiwapo bei ya mafuta..unawaza kupunguza foleni..Kwa nini tusifunze toka kwa wenzetu ambao wana Public Transport nzuri ukaona jinsi zinavyotatua tatizo la foleni kwani haina haja ya kung'a ng'ania magari mabovu na mitumba ya "kafa ulaya"..eti bei ya mafuta ikiongezwa watu watakuwa forced kwenda na daladala.. Hizo public Transport ziko.wapi?.au tunaongelea hayo magari mabovu ambayo yanaruhusiwa kutembea kutokana na njaa ya wale wenye mamlaka wanaopokea rushwa daima.. Kalagabaho!