Nijuavyo! Kuna kesi mbili za wanachi wakiishitaki serikali! Moja tu inasikika, ile ya mkulima na kina makamba imeishia wapi?

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,122
Wakati mawakili wa serikali wakiendelea kunyeshewa mvua ya mawe mahakani kwa mkataba tata wa bandari zetu, shauku yetu kama watanzania na wafia nchi, ningependa kusikia hili la ufujaji wa mapesa yetu walipa kodi

Huyu mkulima aliyetangaza kuwafikisha mahakamani mawaziri kadhaa wa serikali kwa ubadhirifu wa matrilion ya kodi za watanzania iliishia wapi?


Alibinywa pumba ama imekuwaje? Alihongwa ili aondoe jalada la kesi hiyo mahamani?

Kwa sasa ingekuwa huku kuna DPWORD iliyoletwa kimagumashi na wananchi, na huku ni mkulima na kina Nchema na wenzake

Mnaofahamu hii kesi ya mkulima na mawaziri mtusaidie kujua imefikia wapi
 
Back
Top Bottom