Niite jina lolote ila ndivyo nilivyo

Niite jina lolote ila ndivyo nilivyo

3. Mimi sio mzalendo.
Kuwa mzalendo maana yake ni kua uwaheshimu viongozi walioko madarakani(profesa shivji).

mkuu Shivji ni kiongozi wa wapi? Au ametumika hapo

Mbona kama hyo ya 5 itakinzana na mada
 
Hakika unaipenda nchi yako, wewe ndiye mzalendo hasa kwa kukataa kuburuzwa na mafisadi!
 
Jina lako ni nanihii ngoja niende uwani nakuja ila nakuunga mkono

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Acha kujidanganya wewe kenge maji. Kw kifupi kodi unalipa kila siku. Mf mahitaji yako ya kila siku yote unalipa kodi nukta.

Mkuu usikurupuke, soma vizuri uelewe kisha ndio umshambulie huyu MKWEPAKODI
 
samahani mkuu The Unknown naomba unieleweshe kuhusu hiyo direct tax na indirect tax....na mbinu za kukwepa kodi....
 
Last edited by a moderator:
Niite msaliti,mwizi,sio mzalendo au vyovyote ila haya yafuatayo siyafanyi.

1. Silipi kodi.
Sitalipa na huwa silipi kodi ya moja kwa moja au wanaita direct tax. Huo ni utaratibu wangu,silipi na huwa nafanya kadri niwezavyo kuikwepa,nikiuza au kununua sidai lisit,hata nikibanwa sana bora nikubaliane na afsa kodi tuigawane ila isiende serikalini.

2. Siwataji na sitawataja wala rushwa na wakwepa kodi
Hata kama ntamjua mtu anaehujumu uchumi sitamtaja kwa wahusika na wala sina mpango huo isipokua tu waovu kama majambazi.

3. Mimi sio mzalendo.
Kuwa mzalendo maana yake ni kua uwaheshimu viongozi walioko madarakani(profesa shivji). Hivyo basi mimi sio mzalendo na wala sina huo mpango.

4. Sipigi kura na wala sina huo mpango.
Sina mpango wa kuja kupiga kura nchi hii hadi pale ntakapokua nimejiridhisha mwenyewe.

5. Kuwasaidia watu wanaotaka kukwepa kulipa kodi.
Kwa kua nimefanya kazi na watu wa mapato kwa muda,ukijumlisha na kua mimi ni mtu wa mahesabu najua wapi kuna udhaifu wa kukusaidia kutolipa au kukwepa kodi,ntamsaidia watu kadri niwezavyo wakwepe kulipa kodi.

Hayo matano tu. Unaweza kuniitaje?au unaweza kusema nikoje?

Duuh! kweli umeichoka gvt.
 
hiyo maana aliitoa shvji. Namba 5 inakinzana kivipi?
Juu ulisema
"ILA HAYA SIYAFANYI"

halafu

5.Kuwasaidia watu wanaotaka kulipa kodi

Sasa soma hilo na usome hiyo 1, 2, 3 na 4 kama maudhui ya mada yatakuwa sawa
 
Juu ulisema
"ILA HAYA SIYAFANYI"

halafu

5.Kuwasaidia watu wanaotaka kulipa kodi

Sasa soma hilo na usome hiyo 1, 2, 3 na 4 kama maudhui ya mada yatakuwa sawa

Soma mada vizuri,sio wanaotaka kulipa,ni wanaotaka kukwepa kulipa kodi. Soma tena kisha urudi mkuu.
 
Pm maujanja! nimechoka kudhulumiwa,change nataka nile na wanangu tu!
 
Back
Top Bottom