Nihurumieni mwenzenu nakufa

Pesa zinawekwa kimakosa kwenye akaunti yako halafu unazitumia?. Wewe ni mtu wa ajabu sana. Kwa nini hukuuliza kule zilikotoka?.
 
Imani imekuwa ndogo sana miaka hii uenda ikawa kweli lakini je ni nani atasimama nawewe kwenye ilo tatizo lako
 
Mhhh. Hii story imefanywa iwe ni Kweli au imefanywa iwe ni Fix????!!!
Hivi eti, wamekuingizia kimakosa m25 ktk A/C yako na ww ukazilabua kimakosa m25 zote hata usinunue kakuku kamoja hadi senti ya mwisho? mhh! Kama umeshindwa kutumia Fursa ya m25 ulizopata kimakosa utawezaje kutumia m25 utakazopata kihalali?
 
Mkuu, mleta mada, Embu weka namba yako hapa tuanze kukusukumia michango yetu.
Kwa pamoja lazima hilo deni tulifyekelee mbali.
 
Mm aniwekee hapa benki statement inayoonesha aliingiziwa M25,na ioneshe alitoa yote,baada ya kuona aje PM achukue M kadhaa zimsaidie.
 
mtu wa kutapeliwa biashara ya 25 million anafaa kusaidiaa kweli kwa huu uzembe!!!

Pole lakini
 
Vyuma vya Baba J, buma ka Jei Kei
Huna kukaba bei, vuma la cheichei
Danga la Darislamu
Janga kabla salamu
Mpela mpela, shuta karamu, nanga haramu
Mnyonge Hanga, zubaa bila shufaa kaa sanamu
Moto boiling point ka Jehanamu, sina hamu
Kufa hatufi, maisha zigo la chuki
Mizinga na mikuki, kama nyuki
Kaiba haiba, swahiba kaimba
Faida sikawaida,kawinda kwa inda
Vumbua mavumba, zaa toa ugumba,
Uza nyumba weka heshima bar Zanzibar kindumba
Deni unalifuga, halifungi,halimbungi
Tamthiliya kubwa, "Weep Not, Child" wa Thiong'o Ngugi
 
Pole mkuu ila pesa iliingia kimakosa na wewe umeitumia kimakosa hapo ngoma droo
 
Mkuu katumikie tu mvua 10, tamaa ni hasara.
Kwa ufupi tamaa imekuponza, na jaji/hakimu atakuhukumu ili liwe fundisho kwa watu wengine.
 
Ushauri mzuri sana.
Mnamo mwaka 2001,nilikutana na binti mmoja aliyekuwa na shida ya kwenda India kufanyiwa upasuaji,alikuwa na tatizo la moyo. Alikuwa anatafuta 14 milioni na tayari alishapata documents zote toka sehemu husika (MNH,Wizara ya Afya,Mambo ya Nnje).
Alinionyesha docs nami nikajiridhisha kuwa ni halisi. Nikamsaidia milioni kadhaa. Baada ya miezi saba,nikaja kukutana naye Dodoma Hotel,pool side akiogelea. Nilimsogelea na kumkagua kama ana kovu lolote la kupasuliwa (alikuwa amevaa panty & bra tuu,so sehemu kubwa ya tumbo na kifua ilikuwa wazi),sikuona dalili hata ya mchubuko.
Nikamuuliza vipi kuhusu upasuaji wake,kilichotokea ni kuniambia anakuja nimsubirie atanipa story,lakini nikamsubiria mpaka giza,hakurudi na sijawahi onana naye tena,japo nasikia ndio kawaida yake kutapeli hivyo.
Mm aniwekee hapa benki statement inayoonesha aliingiziwa M25,na ioneshe alitoa yote,baada ya kuona aje PM achukue M kadhaa zimsaidie.
 
Anatuzingua tu huyu mkuu mill 25 yote adhulumiwe kiboya boya alafu atuletee shida zake humu
Inawezekana mkuu, kuna mzee alistaafu vijana wakamlainisha kuwa kuna biashara nzuri ya faida, akawapa milioni hamsini yaliojiri ni siri yake.
 
Mzee uko vizuri nilikuwa najaribu kuchana kupitia hizi bars zako daah fresh sana
big up Mkuu Kiranga
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…