Rais wa Nigeria afuta safari za Viongozi za nje ya nchi kwa miezi 3 ili kubana matumizi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1711023386643.png
NIGERIA: Rais Bola Tinibu amepiga marufuku safari zote za Nje za Viongozi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Aprili 1, 2024, lengo likitajwa kuwa ni mpango wa kubana na kupunguza Matumizi ya Serikali yasiyo na ulazima

Hatua ya Rais inafuatia uwepo wa malalamiko ya Wananchi wanaodai Serikali imekuwa na matumizi makubwa ya Fedha za Walipa Kodi yasiyo na tija zikiwemo Safari za Mfululizo za Viongozi akiwemo Rais aliyefanya safari 15 kwenda nje ya nchi tangu alipoapishwa

Hii ni mara ya pili kwa Rais Tinubu kuchukua maamuzi ya kudhibiti matumizi ya Serikali ambapo Januari 2024 alitangaza kupunguza kwa 60% idadi ya Watu wanaokuwa kwenye Misafara ya Viongozi akiwemo yeye mwenyewe. Hata hivyo Tinubu hajaweka wazi kama safari zake pia zitasitishwa.

==============

Nigeria's President Bola Tinubu will introduce a three-month ban on ministers and other government officials from going on publicly funded foreign trips.

Mr Tinubu's chief of staff said the move was prompted by the president's "concerns about the rising cost of travel expenses" by public officials.

The ban will take effect on 1 April.

President Tinubu and his administration have been criticised by some for their frequent visits abroad.

Since his inauguration in May, Mr Tinubu has made more than 15 foreign trips.

The Nigerian president is said to have spent at least 3.4bn naira ($2.2m; £1.8m) on domestic and foreign travel in the first six months of his presidency - 36% more than the budgeted amount for 2023, the Nigerian newspaper Punch reported in January, citing GovSpend, a civic tech platform that tracks government spending.

Mr Tinubu's chief of staff Femi Gbajabiamila said the travel ban will cut costs amid Nigeria's "current economic challenges and the need for responsible fiscal management".

The West African country is grappling with one of its worst cost-of-living crises in decades, a situation that has led to widespread hardship and anger.

The three-month block on official travel by government officials is Mr Tinubu's latest attempt at countering the public backlash.

In January, the Nigerian president announced a reduction in the size of the official travel delegation by about 60% , including cuts to his own travel entourage.

When the ban takes effect in April, government officials will only go on foreign trips "deemed absolutely necessary". They will also require President Tinubu's approval at least two weeks before they travel.

Mr Gbajabiamila added that the halt on travel will ensure that government officials "focus on their respective mandates for effective service delivery".

Despite clamping down on travel by government officials, Mr Tinubu has not said whether he will reduce his own trips.

The president and his representatives have in the past defended his trips as being vital in addressing the economic problems he is accused of ignoring.

BBC
 
Rais wa Nigeria Bola Tinubu atangaza marufuku ya miezi mitatu kwa mawaziri na maafisa wengine wa serikali kwenda safari za nje zinazofadhiliwa na umma kuanzia Aprili mosi.

Rais Tinubu, katika barua yake aliyoiandika, aliagiza kuzuiliwa kwa safari zote za nje, lakini akasema kwamba ruhusa inaweza kutolewa kwa safari zinazoonekana kuwa muhimu sana.

Barua hiyo iliongeza kuwa Tinubu alisema ruhusa hiyo itahitaji idhini ya rais ambayo lazima itafutwe wiki mbili kabla ya safari iliyopangwa.

Kulingana na barua hiyo, marufuku hiyo itadumu kwa siku 90 kwa mara ya kwanza na itaanza kutumika Aprili 1, 2024.

Mkuu wa wafanyikazi wa Bw Tinubu alisema hatua hiyo ilichochewa na "wasiwasi wa rais kuhusu kupanda kwa gharama za usafiri".Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Aprili.

Rais Tinubu na utawala wake wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya watu kwa ziara zao za mara kwa mara nje ya nch
 
Shida hela za kigeni kuna upungufu mkubwa wa pesa za kigeni hasa doka Nigeria

Hata Tanzania pesa za kigeni dola zimeadimika sana shida kupata
 
Rais wa Nigeria Bola Tinubu atangaza marufuku ya miezi mitatu kwa mawaziri na maafisa wengine wa serikali kwenda safari za nje zinazofadhiliwa na umma kuanzia Aprili mosi.

Rais Tinubu, katika barua yake aliyoiandika, aliagiza kuzuiliwa kwa safari zote za nje, lakini akasema kwamba ruhusa inaweza kutolewa kwa safari zinazoonekana kuwa muhimu sana.

Barua hiyo iliongeza kuwa Tinubu alisema ruhusa hiyo itahitaji idhini ya rais ambayo lazima itafutwe wiki mbili kabla ya safari iliyopangwa.

Kulingana na barua hiyo, marufuku hiyo itadumu kwa siku 90 kwa mara ya kwanza na itaanza kutumika Aprili 1, 2024.

Mkuu wa wafanyikazi wa Bw Tinubu alisema hatua hiyo ilichochewa na "wasiwasi wa rais kuhusu kupanda kwa gharama za usafiri".Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Aprili.

Rais Tinubu na utawala wake wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya watu kwa ziara zao za mara kwa mara nje ya nch
Uchumi wao utakuwa mdogo kuliko wa Bongo , hivyo hatuwezi kufuata uamuzi wao.
 
Back
Top Bottom