Nifanyeje wadau? Nisaidie

Nifanyeje wadau? Nisaidie

rupande

Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
47
Reaction score
5
nimepapa schoraship kwenda kusoma UK ya nchi miezi 5, lakini nimechumbiwa na mpango wa ndoa umeshaanza. mwanaume amenikataza nisiondoke. lakini harusi siandai mimi ni wazazi na mda wa harusi nitakuwa nimesharudi tanzania.
huyu mwanaume amesema nikiondoka ataniacha. lakini masomo haya nikiyapata yatatunufaisha sisi sote. tena ni nafasi pekee yaani golden chance, haijirudii tena nikiikosa. hebu nisaidie mawazo wanajukwaa.
 
Elimu ndo ndoa pekee inayodumu
Swala hapo jiongeze tuu ukasome chapchap saana bila kumfklia huyo
 
^^
Chukua kalamu na karatasi,uandike faida na hasara ya masomo na zile za ndoa.
Mwisho chukua uamuzi utakaokupa faida kubwa kwa gharama kubwa.
Pole kwa wakati mgumu ulionao,Mungu akuangazie njia sahihi.
^^
 
'you can force a dunkey to a river but you cant force her to drink...............kama unaskilizia mtarimbo wee endelea kuskilizia huo mtarimbo kwani mtarimbo upo mmoja?,akikuacha na akuache hujui kuwa mlango mmoja ukifungwa kuna mingine itakuwa imefunguliwa tena hukohuko utakapoenda kusoma kama akikuacha utapata mwingine mama nenda kajisomee mwaya,umeshakaa nae mda gani mpaka ashindwe hiyo miezi sita...'
 
nimepapa schoraship kwenda kusoma UK ya nchi miezi 5, lakini nimechumbiwa na mpango wa ndoa umeshaanza. mwanaume amenikataza nisiondoke. lakini harusi siandai mimi ni wazazi na mda wa harusi nitakuwa nimesharudi tanzania.
huyu mwanaume amesema nikiondoka ataniacha. lakini masomo haya nikiyapata yatatunufaisha sisi sote. tena ni nafasi pekee yaani golden chance, haijirudii tena nikiikosa. hebu nisaidie mawazo wanajukwaa.

Nadhani mwanaume amekua moga kidogo kutokana na tabia ya wa dada wengi wakishasafiri hubadilika na mara nyengine hukutana na wanaume huko2 nje na kuwadanganya kwamba watawatafua visa na nini na mambo kibao na kuwaacha wapenzi wao wa zamani.. Hiyo issue inabidi muiongelee kifamilia na umuhakikishie mchumba wako kwamba hauta msaliti wala haudanganyikkki. Bilashaka atakuelewa! shule ni muhimu na ndoa ni muhimu pia. Pole kwa changamoto...
 
Hii habari haileweki "uk ya nchi" ndo nini then hiyo ni scholarship au short kozi.umechakachua jipange urudi tena,ndo maana jamaa haimuingii akilini.
 
Muambie asipokuruhusu uende na wewe utamuacha!
Na ujijue hapo ndo shule na mikazi ya maana bye bye. He is a control freak. Kwani hukuwa umemuambia kakukuta na bwana mwingine anaitwa career na yeye ndo small hausi? Kiranga njoo utoe ushauri huku
 
Last edited by a moderator:
Hahaha kuna wanaume wengine ni wajinga kuliko ujinga wenyewe...
We bidada nenda zako kafanye hiyo workshop/training or short course...
Kama kweli ana mpango wa kukuacha sasa kisa elimu, basi mpango kama huo unaweza kuibuka hata ndoani kwa sababu nyingine tu...
 
Dah!Kweli wengi mtamshauri huyo dada akasome nje lakini kwa ka-experience kangu kadogo kwakweli nimewashuhudia wanawake matendo yao wanayoyafanya, mbaya zaidi wake za watu wanaokwenda nje kusoma wanagegedwa sana tena kupita hata wanawake ambao bado wapo wapo (Japokuwa si wote lakini naweza sema kwa kule niliposomea ni karibia 80%, tena wanakuwa maharage ya mbea sana kwa watu wa mataifa mengine hasa waafrika magharibi).Na nimekuwa najiuliza hili linatokana na nini lakini sipati jibu sahihi. Kuanzia hapo nikala kiapo kuwa sitakuja kumruhusu mke wangu kamwe akasome nje tena hasa kwa kipindi kirefu ndiyo hatari zaidi. Naongea haya kwa ushahidi wa kuushuhudia mwenyewe.

Kwangu mimi hapo nakosa cha kushauri, sijui mwanaume huyo anamakosa au ana mawazo kama yangu kwakweli sijui.
 
nimepapa schoraship kwenda kusoma UK ya nchi miezi 5, lakini nimechumbiwa na mpango wa ndoa umeshaanza. mwanaume amenikataza nisiondoke. lakini harusi siandai mimi ni wazazi na mda wa harusi nitakuwa nimesharudi tanzania.
huyu mwanaume amesema nikiondoka ataniacha. lakini masomo haya nikiyapata yatatunufaisha sisi sote. tena ni nafasi pekee yaani golden chance, haijirudii tena nikiikosa. hebu nisaidie mawazo wanajukwaa.

Ndugu yngu kasome..Ndoa ipo tu labda wew mwenyew usijielewe ukafanya mambo ya ajabu..Ukisharudi na kupata mafanikio ndo atatambua kuwa ulikuwa na nia nzur na hiyo ni kwa faida ya familia yenu mtakayoianzisha..
 
yani akuache kwa jambo la msingi kama hilo?
nenda kasome mwaya..hana sababu ya maana ya kukuacha
 
Huyo mchumba wako hapendi uende nadhani kwa sababu zake za msingi, na ni kipimo cha kuangalia unampenda kiasi cha kusacrificre nn kwa ajili yake.
Wengi watakushauri elimu ni bora kuliko ndoa, lkn elimu haitunzi mume na elimu inapatikana muda wowote, tofauti na mume kama huyo kaka uliyempenda sasa na ukakubali akuoe.
Ipi "golden chance" kati ya kuolewa na mtu ambaye hujaona mfano wake na kwenda nje?
Nje unaweza enda muda wowote, scholarship zipo kila leo.
Fikiri na kuomba sana kabla hujaamua.
 
Kasome wewe acha ujinga! Miez 5 c mingi ka anakupenda! Afu nahsi utakuwa umemzidi kama c elimu bas financialy that y anahofu!
 
Hahaha kuna wanaume wengine ni wajinga kuliko ujinga wenyewe...
We bidada nenda zako kafanye hiyo workshop/training or short course...
Kama kweli ana mpango wa kukuacha sasa kisa elimu, basi mpango kama huo unaweza kuibuka hata ndoani kwa sababu nyingine tu...
wanaume wa hivyo tunayaita madume ya mbwa!aisee mimi ningekuja mwonyesha visa siku yakuondoka tu akitaka aniache akitaka anisubiri umenikuta na elimu nasoma sasa wewe unipangie nini? hebu nenda huko lol jinga kabisa hilo
 
nimepapa schoraship kwenda kusoma UK ya nchi miezi 5, lakini nimechumbiwa na mpango wa ndoa umeshaanza. mwanaume amenikataza nisiondoke. lakini harusi siandai mimi ni wazazi na mda wa harusi nitakuwa nimesharudi tanzania.
huyu mwanaume amesema nikiondoka ataniacha. lakini masomo haya nikiyapata yatatunufaisha sisi sote. tena ni nafasi pekee yaani golden chance, haijirudii tena nikiikosa. hebu nisaidie mawazo wanajukwaa.

Angalia future yako ww....wanaume wapo tu...hawaish...nenda kasome!!!!!!
 
Mwambie akufundishe yeye hiyo course ili usiende ULAYA ................!:love:
 
kama inawezekana fungeni ndoa bila sherehe,makanisa yote yanaweza fanya hilo.then wewe nenda kasome.Mchumba wako ana hofu tu kuwa utaweza kumkimbia na yeye ndo keshaoza kwako kwa malove love.kaa nae mueleweshane kwani mwisho wa siku ni nyinyi tu wawili ndo wahusika wakuu wa penzi lenu,some times haya yanatokeaga ila mkikaa ukamwuliza hofu yake ataweza funguka na mkaenda sawa goodluck
 
shauri lako ukimkacha huyo jamaa ujue keshakuacha hvyo..

olewa mwaya..wanaume wenyewe hawa wamepinda
utakuwa kama makinda!
mazima.
 
Mi naona tungeijadili hiyo elimu na point alizotumia mchumbako kuikataa (Tena ya bure wakati its sooo expensive kusoma cku izi!!!!)
Iseme tu tuijadili maana ndo point muhimu!
Anaenda kuwa mmeo for life, kichwa cha nyumba na mapema hii keshaanza ku exercise uwezo wake wa kuchambua mambo kwa kuangalia faida na hasara.
Kaa nae chini mwaya, kama kweli unamrusha roho mpaka kaamua kukuoa show him why u r his choice...mfunulie vizuri sababu za wewe kwenda kusoma na faida yake kwenu. Trust me ukishow your convincing power kila kitu kitaenda sawa. Mambo mengine wala huhitaji bunduki!
 
Ndugu hiyo ni chance ya pekee sana wala usithubutu kuiacha eti kisa NDOA kwani hutaipata tena na wala haitatokea tena huyo mchumba wako ana wivu hataki wewe uendelee kimasomo hataki maendeleo ya wanawake huyo anataka kukatisha nuru iliyoingia kwako, cha kufanya wewe ongea na watu wazima wamshauri ili mpange tarehe ya harusi mbele pindi ukitoka kwenye hayo masomo
nimepapa schoraship kwenda kusoma UK ya nchi miezi 5, lakini nimechumbiwa na mpango wa ndoa umeshaanza. mwanaume amenikataza nisiondoke. lakini harusi siandai mimi ni wazazi na mda wa harusi nitakuwa nimesharudi tanzania.
huyu mwanaume amesema nikiondoka ataniacha. lakini masomo haya nikiyapata yatatunufaisha sisi sote. tena ni nafasi pekee yaani golden chance, haijirudii tena nikiikosa. hebu nisaidie mawazo wanajukwaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom