Nifanyeje nipate haki yangu

Nifanyeje nipate haki yangu

Wakuu samahani am just very new here sasa naomba msaada nimechelewa kumuomba ruhusa ya maternity leave muajiri yani ile miez mitatu kabla imepita nimeapologize na kuomba afikirie kunipa hizo siku zote anataka kunipa just 6 weeks naomba msaada kisheria nifanye nini nipate siku zangu zote. Asante
Cc Invisible
Tafadhali hamishia huu uzi panapo husika
 
Likizo ya uzazi inaelezewa chini ya Sehemu ndogo D ya Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004. Mfanyakazi atastahili likizo ya uzazi/ulezi baada ya kumaliza miezi sita (6) kazini toka siku mkataba wa kazi ulipoanza. Kigezo kingine cha mfanyakazi kustahili likizo ya uzazi/ulezi ni masharti ya sheria yanayomuhitaji mfanyakazi kutoa taarifa ya maandishi kwa mwajiri juu ya dhamira yake ya kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu (3) kabla ya siku anayotarajia kujifungua. Taarifa hiyo ni lazima iambatane na cheti cha madaktari.
Mfanyakazi atastahili likizo ya uzazi/ulezi baada ya kumaliza miezi sita (6) kazini toka siku mkataba wa kazi ulipoanza.

Inapo tokea muajiri kuninyima likizo ya uzazi /ulezi kwa kushindwa kutoa taarifa kama inavyotakikana....
Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 imeweka kigezo hiki kwa mfanyakazi kuweza kupata likizo ya uzazi/ulezi. Sheria iko kimya juu ya kitakachotokea kama utashindwa kutoa taarifa kama inavyotakikana. Kwa hivyo inashauriwa kwa mfanyakazi kutoa taarifa ya miezi mitatu kwasababu mwajiri anaweza kukataa kutoa likizo ya uzazi/ulezi yenye malipo kwasababu ya kushindwa kufata taratibu zilizowekwa na sheria.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, wewe ndie mwenye makosa na hakuna haki yenye utaipata kwasababu tayari kimesha fanyika kile ambacho ulipaswa upate ruhusa ili ukakifanye. Nakushauri tu uendelee na kazi na kuwa mpole kwasababu hata hizo wiki 6 ulizo pewa ni bahati yako ama muajiri ameonyesha uungwana
 
Back
Top Bottom