Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 532
- 1,036
Wasalam mabibi na mababu..
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, Nimekuwa nikiteseka sana kwa kukosa usingizi usiku na ata mchana kwa muda kama mwezi naa,,, kichwa changu kimekuwa kikiandamwa na mawazo sana ya kiuchumi michongo haipo tena wala fursa yani nachezea bakora za mtaa haswa, lakini mawazo mengine yananijia japokuwa sio sana ni ya kumpoteza Baba angu mzazi mwaka huu mwezi wa tatu ukizingatia mimi ndio nilomuuguza mpaka akanifia mikononi mwangu.
Yani inafikia hatua mpaka naona hii mishipa ya fahamu huku nyuma ya kichwani ad shingon inauma sana, yani cpati usingizi ata lepe ata nikijilazimisha vipi, ata nikijilazmisha nisahau mawazo yangu lakini wapi.
Nimekuwa nikijitahidi sana aidha niangalie ata movie, najipeleka hadi kwenye mabanda ya mipira, nakaaga maskani na watu tofautitofauti lakini wapi. Najiona kama sina bahati na haya maisha, kila kukicha naona heri ya jana.
Asilimia kubwa ya mawazo ninayowaza ni namna gani nitajinasua kiuchumi nami nitusue walau nipate stara ya maisha, haya maisha yana ramani ila alomchorea masikini peni ilimgomea Njiani.
Kwa namna ya maisha nayopitia saivi nyimbo zangu kubwa ni tatu tu kwenye Playlist yangu ni kabwela ya stamina, matatizo ya harmonize pamoja na Usilie ya Christian bella.
Kuna mtu kanishauri ninunue dawa za usingizi lakini naona kama sio vizur mana nkizizoea mazima uenda zikanipa tabu baadae.
Je nifanyeje ili niweze kupata usingizi na mimi usiku??? Nimechoka kuwa team Popo.