Nifanye nini niweze kuwa na Upeo wa Akili kama wanasiasa hawa?Nikiwasikiliza najisikia Wivu wa kutaka kuwa kama wao

Kila nikimwona na kumsikia kibajaji anaongea … kwa kweli natamani sana niwe kama yeye… naombea niwe na akili kama zake. Siku nikizipata ntafurah sana maana ntaishi maisha ambayo hayana stress na kiukweli ubongo wangu utapumzika sana. Kwa sasa najiona jinsi ninavyoutesa ,jinsi ninavyousumbua na kuuchosha kwa kuwaza na kuwazua. Kwa mfano kila jambo ninalotaka kulisema public mimi nalifikiria mara mbili mbili lakini kama nikifanikiwa kupata akili kama za kibajaji,elibariki kinge au msukuma wala sihitaji kufikiria mara zote hizo nakuwa huru tu.natiririka tu.

Mwingine ambaye natamani niwe na akili kama zake ni pole pole… aisee.. siku nikiweza kuwa kama yeye ntafurahi sana…. Itanisaidia hata kazini kuishi na maboss vizuri… kwa kweli watanipenda sana maana ntakuwa na akili kama za pole pole ambazo zipo hivyo zilivyo.najua mtanisema mimi mnafiki.lakini nikiwa na akili kama zake wala sitojali. pole pole Anajua to swim with the current…kipindi kile pole pole anapiga piga push ups watu hawakutegemea kuwa zitakuja kumlipa. Jamaa anaona mbali sana. Na kwa kweli nimegundua ana akili za hali ya juu.natamani nikiwa mzee niwe kama yeye… I mean nikiwa mkubwa.

Kwa ujumla tu napenda asilimia kubwa ya akili za wabunge,mawaziri na viongozi wa CCM. Hiki chama ni kizuri ukijiunga nacho unabadilika kabisa… unaanza kupumzisha ubongo.. so hauchoki haraka maana ubongo unatulia kabisa kama maji ya mtungini. Kwa kweli wamebarikiwa. Wasikilize wabunge wa CCM wakiongea.. hadi raha… wanaongea tu maneno yanawatoka hawahitaji kuumiza kichwa kukesha kufikiria kama wengine. Wa CCM wengi wao ni Geniuses wanatiririka tu.. halafu wanapigiana makofi basi nikiwaona nafurahi.. natamani name niwe kama wao… niamke tu kitini nioongeeeeee weee….. wenzangu wagonge meza kwa furaha. Tukitoka hapo tunachukua posho siku inaisha. Aisee… natamani sana.

Hapa nasema siku nikiwa mkubwa nitakuwa rais. Nitakuwa kama rais alivyo… ole wao washakunaku wajifanye kuja kunishauri ujinga…. Nitawatimulia mbali.. maana nitakuwa na akili za kipekee… nitakachosema ndicho kitakuwa. Nikiamka na mabangi yangu hata usiku nafanya ziara ya kushtukiza sehemu ila waandishi wanakuwa wamepewa taarifa so kutegemeana na mabangi ya siku hiyo yamenituma vipi.kwanza ukiwa rais unavuta bangi hata polisi hawakusumbui tena unaweza ukawa unavuta huku na mkuu wao yupo pembeni..au hata unamtuma akuletee ile kali ya Malawi. Hapo sasa nikivuta… wananchi wazembe na wenye kupenda maneno maneno bila kazi watanikoma.

Huwa nawacheck sana wale watu wanaoninyanyasa kwa sasa.. nawatizamana siku yao ipo.. wataimba halleluya..siku nikiwa rais wan chi hii… ntachagua watu ambao nawafaham hawahitaji akili kufiiri… hawa watakuwa wao wanaimba mapambio ya kunisifu na pia nikianzisha wimbo wao wanaimba kibwagizo tu maneno naweka mimi… watacheza na kushangilia. Wenye roho mbaya nitawafutilia mbali.ili nchi ibaki ya watakatifu wenye kunielewa mimi rais. Natamani sana kwa kweli.
Hapo kwenye kuvuta mabangi umenikoshaaaa
 
Ukiwa na mtu wa kufikiri kwa niaba yako ni raha hadi kufa.Tafsiri ya upumbavu inasema hivi,Ni ile hali ya kuujuwa ukweli,kuuona ukweli,lakini unaendelea kuamini katika uongo.
 
nashindwa.... najitahidi sana..nashindwa.
GuDume jana niliisoma post yako lakini kila nivyokua naisoma nikajikuta nacheka lakini hii ya leo nayo dah. haya bwana nimekusoma. ila si akili za wabunge tu hata akili za police na postmortum ya mauji ya watu mbalimbali yani hawaumizi kichwa wanakuwa na majibu tayari kama motokeo ya upelelezi wa akwilina
 
Kila nikimwona na kumsikia kibajaji anaongea … kwa kweli natamani sana niwe kama yeye… naombea niwe na akili kama zake. Siku nikizipata ntafurah sana maana ntaishi maisha ambayo hayana stress na kiukweli ubongo wangu utapumzika sana. Kwa sasa najiona jinsi ninavyoutesa ,jinsi ninavyousumbua na kuuchosha kwa kuwaza na kuwazua. Kwa mfano kila jambo ninalotaka kulisema public mimi nalifikiria mara mbili mbili lakini kama nikifanikiwa kupata akili kama za kibajaji,elibariki kinge au msukuma wala sihitaji kufikiria mara zote hizo nakuwa huru tu.natiririka tu.

Mwingine ambaye natamani niwe na akili kama zake ni pole pole… aisee.. siku nikiweza kuwa kama yeye ntafurahi sana…. Itanisaidia hata kazini kuishi na maboss vizuri… kwa kweli watanipenda sana maana ntakuwa na akili kama za pole pole ambazo zipo hivyo zilivyo.najua mtanisema mimi mnafiki.lakini nikiwa na akili kama zake wala sitojali. pole pole Anajua to swim with the current…kipindi kile pole pole anapiga piga push ups watu hawakutegemea kuwa zitakuja kumlipa. Jamaa anaona mbali sana. Na kwa kweli nimegundua ana akili za hali ya juu.natamani nikiwa mzee niwe kama yeye… I mean nikiwa mkubwa.

Kwa ujumla tu napenda asilimia kubwa ya akili za wabunge,mawaziri na viongozi wa CCM. Hiki chama ni kizuri ukijiunga nacho unabadilika kabisa… unaanza kupumzisha ubongo.. so hauchoki haraka maana ubongo unatulia kabisa kama maji ya mtungini. Kwa kweli wamebarikiwa. Wasikilize wabunge wa CCM wakiongea.. hadi raha… wanaongea tu maneno yanawatoka hawahitaji kuumiza kichwa kukesha kufikiria kama wengine. Wa CCM wengi wao ni Geniuses wanatiririka tu.. halafu wanapigiana makofi basi nikiwaona nafurahi.. natamani name niwe kama wao… niamke tu kitini nioongeeeeee weee….. wenzangu wagonge meza kwa furaha. Tukitoka hapo tunachukua posho siku inaisha. Aisee… natamani sana.

Hapa nasema siku nikiwa mkubwa nitakuwa rais. Nitakuwa kama rais alivyo… ole wao washakunaku wajifanye kuja kunishauri ujinga…. Nitawatimulia mbali.. maana nitakuwa na akili za kipekee… nitakachosema ndicho kitakuwa. Nikiamka na mabangi yangu hata usiku nafanya ziara ya kushtukiza sehemu ila waandishi wanakuwa wamepewa taarifa so kutegemeana na mabangi ya siku hiyo yamenituma vipi.kwanza ukiwa rais unavuta bangi hata polisi hawakusumbui tena unaweza ukawa unavuta huku na mkuu wao yupo pembeni..au hata unamtuma akuletee ile kali ya Malawi. Hapo sasa nikivuta… wananchi wazembe na wenye kupenda maneno maneno bila kazi watanikoma.

Huwa nawacheck sana wale watu wanaoninyanyasa kwa sasa.. nawatizamana siku yao ipo.. wataimba halleluya..siku nikiwa rais wan chi hii… ntachagua watu ambao nawafaham hawahitaji akili kufiiri… hawa watakuwa wao wanaimba mapambio ya kunisifu na pia nikianzisha wimbo wao wanaimba kibwagizo tu maneno naweka mimi… watacheza na kushangilia. Wenye roho mbaya nitawafutilia mbali.ili nchi ibaki ya watakatifu wenye kunielewa mimi rais. Natamani sana kwa kweli.
Natamani sana kuwa kama Wasira au mwigulu,wasira alisinzia bungeni kisha gazeti la mwananchi likamweka hewani,wasira akaja juu na kudai hilo gazeti linataka kuleta machafuko nchini,kuwa ccm ni raha sana.
mwigulu alimwita binadamu aliyeumbwa na Mungu kuwa ni kinyago,wakati huo huo anajiita mcha Mungu,hakyanani kuwa ccm ni full burudani.
 
Hii Kali kumtuma mkuu akuletee cha Malawi
Umegundua kitu nini maaana wangu hawabanduki katk ziara zake anaeshika mmoja wa dozi nini
 
Hapo kabla nilijua jf membaz ni great thinkers kumbe kuna vilaza level ya milembe! Hivi kweli watu hawajamwelewa mleta mada na ametumia kiswahili? Hivi zikiwa mada heavy kweli watu wataona chochote? Ndo maana ukianza ongea economic diplomacy au international ishuz watu wanachangia shudu leo nimepata majibu! Nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kumiliki digrii moja, naamini ambao hawajaelewa uzi mwepesi kama huu maana nawaona wanaruka na kukanyagana ninawasi wasi kama la saba wamefika. Nawaomba moderators waanze kukagua vyeti humu ndani angalau milembe members mkae pembeni.
 
naona GuDume umeamua kuwaponda ccm jinsi walivyo vilaza, wako shallow kiakili na hawana muda wa kuwazia mambo mema nchi hii wao kwao bora posho na Raisi ndiyo kama hivyo alivyo bhana naye ni mule mule sema nin tuna Raisi mchapa kazi sana aiseee( kusifia muhimu si unajua ile sheria ya kutaka member watambulike majina yao halisi inakuja very soon najiandaa kisaikolojia)

Ila safi bandiko lako linahitaji akili kuelewa ujumbe wako mzuri
 
Kwa ujumla tu napenda asilimia kubwa ya akili za wabunge,mawaziri na viongozi wa CCM. Hiki chama ni kizuri ukijiunga nacho unabadilika kabisa… unaanza kupumzisha ubongo.. so hauchoki haraka maana ubongo unatulia kabisa kama maji ya mtungini. Kwa kweli wamebarikiwa. Wasikilize wabunge wa CCM wakiongea.. hadi raha… wanaongea tu maneno yanawatoka hawahitaji kuumiza kichwa kukesha kufikiria kama wengine. Wa CCM wengi wao ni Geniuses wanatiririka tu.. halafu wanapigiana makofi basi nikiwaona nafurahi.. natamani name niwe kama wao… niamke tu kitini nioongeeeeee weee….. wenzangu wagonge meza kwa furaha. Tukitoka hapo tunachukua posho siku inaisha. Aisee… natamani sana.
Hapa nimekuelewa vyema.
 
Da! Hapo kwenye bangi tena kitu cha Malawi umezifanya mbavu zangu zinyooke.

Teh teh teh teheeeeeeeeeeee!!!!!!!
Daaah. Umenikumbusha Mbali
tapatalk_1509547631140.jpeg
 
naona GuDume umeamua kuwaponda ccm jinsi walivyo vilaza, wako shallow kiakili na hawana muda wa kuwazia mambo mema nchi hii wao kwao bora posho na Raisi ndiyo kama hivyo alivyo bhana naye ni mule mule sema nin tuna Raisi mchapa kazi sana aiseee( kusifia muhimu si unajua ile sheria ya kutaka member watambulike majina yao halisi inakuja very soon najiandaa kisaikolojia)

Ila safi bandiko lako linahitaji akili kuelewa ujumbe wako mzuri

mkuu watajuaje kama hili ni jina langu halali na si feki au watataka tusajili na vitambulisho vyetu? magufuli ni kichaa kamili,mwisho wa siku atakuja kusema wasio ccm siyo raia wa Tanzania kwa hiyo waondoke Tanzania.
 
Back
Top Bottom