Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,763
kiukweli miaka 7 iliyopita nilikuwa na uhusiano na mke (bibi) wa mtu ambao hawajafunga ndoa hadi leo. kipindi hicho damu inachemka kwa sana. akashika mimba na wala hakuniambia mimba ni yangu. baada ya kujifungua ndipo akaniambia kuwa mtoto ni wangu. sikutaka kukubali na akawa ananilazimisha na kutishia kunisusia mtoto. kila aliyemwona alisema mtoto ni wa kwangu. uhusiano na huyo bwana wake nao ukawa na migogoro kipindi hicho. ikafika wakati nikaanza mchakato wa kumkubalia alichosema. ndipo siku tukakutana akaniambia kuwa yule mtoto si wangu na alikuwa anataka kunibambikizia tu. akasema kuwa ndugu wa bwana wake walikuja kumwona mtoto na wakaridhika kuwa ni damu yao. nikakubali shingo upande. huwa nakutana na rafiki yake wa karibu na huwa namuuliza kuhusu huyo mtoto nae anasema kuwa ni wangu, na kwamba wanawake wana siri sana. huwa nakutana na huyo mke wa mtu kwa nadra (si kufanya mapenzi) na nikimuuliza anakataa kabisa na kunipotezea. siku zinavyoenda nazidi kuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli na ikibidi kuthibitishiwa ukweli. cha ajabu hadi leo hawajaongeza mtoto mwingine wakati huyo ana miaka 7 sasa. kuna uwezekano wa kumpata huyo mtoto au ndio basi?