nifanye nini nimpate mwanangu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nifanye nini nimpate mwanangu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, Jan 30, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kiukweli miaka 7 iliyopita nilikuwa na uhusiano na mke (bibi) wa mtu ambao hawajafunga ndoa hadi leo. kipindi hicho damu inachemka kwa sana. akashika mimba na wala hakuniambia mimba ni yangu. baada ya kujifungua ndipo akaniambia kuwa mtoto ni wangu. sikutaka kukubali na akawa ananilazimisha na kutishia kunisusia mtoto. kila aliyemwona alisema mtoto ni wa kwangu. uhusiano na huyo bwana wake nao ukawa na migogoro kipindi hicho. ikafika wakati nikaanza mchakato wa kumkubalia alichosema. ndipo siku tukakutana akaniambia kuwa yule mtoto si wangu na alikuwa anataka kunibambikizia tu. akasema kuwa ndugu wa bwana wake walikuja kumwona mtoto na wakaridhika kuwa ni damu yao. nikakubali shingo upande. huwa nakutana na rafiki yake wa karibu na huwa namuuliza kuhusu huyo mtoto nae anasema kuwa ni wangu, na kwamba wanawake wana siri sana. huwa nakutana na huyo mke wa mtu kwa nadra (si kufanya mapenzi) na nikimuuliza anakataa kabisa na kunipotezea. siku zinavyoenda nazidi kuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli na ikibidi kuthibitishiwa ukweli. cha ajabu hadi leo hawajaongeza mtoto mwingine wakati huyo ana miaka 7 sasa. kuna uwezekano wa kumpata huyo mtoto au ndio basi?
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mithali 1 : 7 'kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa' hebu mrejee Mungu ukitubu dhambi ya kuiba mke wa mtu huku ukijua fika kuwa ni makosa, na Mungu atakupa maarifa, hata hivyo usirudie tabia hiyo mbaya
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  nimekupata
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,634
  Likes Received: 9,129
  Trophy Points: 280
  Three letters, DNA.

  Na hiyo ni kwa consent ya huyo mama, kama anataka wote mjue ukweli.

  Ama sivyo kubali tu, ulikuwa unafanya mambo kwa ashki tu na hukupanga kupata mtoto, na mtoto kuna chance kubwa si wako, kwa hiyo sahau tu.
   
 5. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani uendelee na maisha yako tu maana kitanda hakizai haramu.


  Annina
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  sina uhakika kama unayaelewa uliyoyasema au umeysema tu kwa vile yapo mdomoni
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  inawezekana ikawa kweli. Si watoto wote ni wa ndoani
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Hadithi kama za SHY hizi!
   
 9. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,393
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mambo hayo sio unatuletea hapa, peleka tamwa huko ukadadadike na wenzako.....fankuro!!
   
 10. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Story yako haina flow ya kueleweka. Umetunga au umemodify situation. Kama ni kupotezea watu muda, wamekushtukia.
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hujaombwa kuchangia. Its optional
   
 12. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,625
  Likes Received: 8,004
  Trophy Points: 280
  Kingi,

  Kama yule mama uliyezaa nae anaishi na yule bwana, na wewe, suddenly, from nowhere, uibuke sasa hivi (after 7 years) useme ati yule ni mwanao, utaonekana kama umedata flani hivi. Kwanza utaanzaje?

  Imekula kwako hiyo mjomba, anza mbele na maisha yako.

  BTW, wewe huna mtoto/watoto wako?? kama unao, wapende hao kwanza na anza kuwajengea msingi bora wa maisha yao ya baadae (shule etc)
   
 13. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ona mkorogo huo...... ulikuwaje na mke wa mtu ambaye hawafunga ndoa hadi leo? hukutembea na mke wa mtu.
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sure inabidi kukubali tu, labda itokee sintofaham na yeye (mwanamke) mwenyewe anieleze tena ukweli
   
 15. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Kiranga umeongea kweli kuhusu issue ya DNA lkn gharama zake zikoje kwa hapo TZ maana nilisikia ni gharama kubwa kweli.

  Hiyo issue ya jamaa inafanana na moja nimeiona kwenye program moja hivi channel 4 na DNA test ikaweka mambo hadharani.. Naona wazungu wanaenda kwenye program kama hizi ili kukwepa gharama maana inakuwa bure wakienda kwenye program kama hizi. Ebu kama unajua price ya kufanya DNA test bongo tufahamishane in future inaweza kuwa na umuhimu.
   
 16. M

  M-Joka JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 13, 2007
  Messages: 308
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  1. Mtoto wakati wote ni halali iliyo wazi kwa mama(mwanamke). Kinachofanya uhalali kwa mwanamme (baba) ni NDOA tu, peke yake. Hapana ndoa hakuna mtoto kwa mwanamme kwa maana ni zinaa imepita na ni mtoto wa upande mmoja. Kisharia hatia ya makosa ya zinaa kwa mwanamke ukiondosha ushahidi redhanded ni kule kwa yeye kushika uja uzito pasipo na ndoa. kama ukijitokeza basi ulitakiwa na wewe uadhibiwe kwa uzinifu kama huyo mwanamke.

  2. Ukisikia neno linaloitwa "mtoto wa haramu" maana yake ni kwamba siyo mtoto wa haramu kwa mama yake, la hasha, bali ni mtoto wa haramu kwa yule mwanamme aliyebandikizwa kuwa baba yake na ilihali ya kuwa ndoa haikuwepo. Hivyo ni haramu yake.

  3. Tafadhali usimfanywe abandikwe jina baya la "mtoto wa haramu" huyo mtoto kwa utamanifu na enjoyment yako ya kuitwa baba, hana kosa kustahili hivyo, na makosa mnayo nyinyi mliofanya zinaa. Shika njia yako utubie na huyo mama ashike njia yake na mwanawe atubie, kama nyote ni watu wa ku-reflect na kutubia. Dhambi unayoihadithia katika kadamnasi ni vigumu kufutika.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  very interesting. wewe ni mchungaji, au shehe? una mafundisho mazuri, na yaelekea huna hatia weye
   
 18. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,397
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kama stori hiyo ni ya kweli..basi bwana huyo ni **** ila mbaya!!! kwanza ni mzinzi na mwizi wa mke watu halafu anapata nguvu gani za kudai hivyo..si anajitafutia balaa
   
 19. y

  yegomwamba Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mithali 1 : 7 'kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa' hebu mrejee Mungu ukitubu dhambi ya kuiba mke wa mtu huku ukijua fika kuwa ni makosa, na Mungu atakupa maarifa, hata hivyo usirudie tabia hiyo mbaya __________________

  Tena tamaa yako itakupeleka motoni acha kabisa,mrudie Muumba wako.Hivi Kingi mbona unataka kuchefua wana jfhivo?
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  huwa inatokea, mkuu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...