Nimekupenda bure mdada kawa tabia yako ya ku-question utumiwaji wa hiyo hela. Kwa ulimwengu wa sasa na type ya wanawake tulionao, asilimia kubwa wangechukua tu na kuendelea without questioning anything. Nimependa pia kuwa umemshirikisha mama yako.
Kwa upande wangu, sioni kama kuna tatizo endapo tu jamaa alidhamiria kutoa kama kumbukumbu na uthamini wa upendo wako kwake na pia anaijua hali ya maisha ya kwenu na nadhani hicho ndicho kilichompelekea kukupa hizo fedha akihisi kwamba zitakusaidia in one way or another.
Ili uwe katika safe side, fanya yafuatayo
1: Mtumie msg kumjulisha kuwa umeupata ujumbe wako na unashukuru sana, ile je dhamira iliyokusukuma hasa kunitumia hela ni ipi?
2: Akishakwambia dhamira yake, mueleze kwamba nia yangu mimi ni kukurudishia hizi hela kwa sababu sitapenda kujihusihusisha nawe kwa mawasiliano ya aina yoyote coz wewe ni mume wa mtu kwa sasa na hii hela inaweza kusaidia mengi kwa familia yako. Sikilizia jibu lake
3: Akisisitiza uchukue, mwambie tu if you insist nashukururu ila naomba isiwe sababu ya sisi kurudisha mawasiliano au uhusiano kati yetu. I will keep the money and if that happens, i will give your money back.
Baada ya hapo, tafuta kitu cha kufanya ili kuizungusha hiyo hela izalishe huku ukihakikisha kuwa hiyo 4m inabaki kama capital ili siku akikuzingua unamrudishia mwenyewe.