Nifanyaje kumzuia mtoto anayenyonya kidole?

Steph JK

Senior Member
Joined
Sep 14, 2018
Posts
104
Reaction score
110
Habari wadau,

Mwanangu mwenye miaka minne ana tabia ya kunyonya kidole, nimejaribu kumweka pilipili na baadae kumfunga bandage lakini hajaacha kutumia.

Niliwahi sikia madhara ya kunyonya kidole ni pamoja na meno kutoka nje.

Naomba kwa anayejua jinsi ya kumzuia anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
subiri akiwa amelala mpake...pili pili ila inatakiwa uwe na ujasiri sana...na hakikisha pili pili inakuwa kari zaidi
 
Binti yangu tulimfanyia hivi ila hakuacha, akaja kuacha tu automatic akiwa kidato cha kwanza. Kila mbinu iligonga mwamba.
 
Ukianza naye akiwa bado mchanga ni rahisi, akiweka mdomoni mnamtoa.

Ila akishafikisha miaka minne ni ngumu sana kuacha, labda mpaka wenzake waanze kuwa wanamcheka shuleni ndo anaweza kuacha.
 
Wangu tulimzembea nadhani, shule ya msingi kachekwa weee na wenzie ila hakuacha. Kaja kuacha sekondari.
 
Inatokea, mara nyingi ni kumuwahi akiwa bado mchanga, asiruhusiwe kuweka kidole mdomoni kabisa.
 
Back
Top Bottom