Nakukunda
JF-Expert Member
- Jul 10, 2017
- 877
- 1,635
Wapendwa,
Naomba mnisaidie mbinu ya kumfanya mtoto wa miaka nane kuacha kukojoa na kunyonya kidole
Nimeshaomba na kufunga na bado namwamini Mungu atamfungua
Japo naamini mpo ambao watoto wenu wamepona na kuacha hizo tabia, naomba mnielekeze nimsaidie binti yangu.
Unaweza hata kumuamsha mara mbili na bado atakojoa, tunamzuia kunywa vitu vya maji maji kuanzia saa moja jioni ikiwa ni pamoja na kumsimamia akojoe kabla ya kulala na bado atakojoa.
Na kinachonishangaza anakuwa kama anatafuna na kujikaza misuli wakati wa kukojoa. Na anaweza lala hata ndani ya nusu saa na akakojoa.
Ameanza hii tabia akiwa na miaka mitatu chini ya hapo alikuwa hanyonyi kidole wala kukojoa Kuna nyumba niliwahi kupangisha miaka hiyo nahisi haikuwa nzuri sababu licha ya kuanza kukojoa mtoto alikuwa anaumwa kifua mno.
Nimeamua kujikita katika kumwombea japo ningeomba mnipe mbinu za malezi mlizowahi kutumia kusaidia watoto wenu waliopitia changamoto kama hii maana naona inamnyima mtoto wangu confidence maana hata yeye hapendi na namwona kabisa anaumia.
Naombeni mnipe mbinu ya malezi kwani ana wadogo wake wawili hawajikojolei hata wanywe maji vipi ila dada yao ndo ananipa wakati mgumu kwa kweli.
Ahsanteni