Amekuwa blocked kwenye simu zake zote baada ya kuachana hali ya kuwa wana mtoto

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,118
Nanukuu;

"Nimedumu na huyu mwanamke kwa muda wa miaka 3 na tumefanikiwa kupata mtoto 1, kutokana na tabia zake mbaya za muda mrefu nilivunga kutopeleka mahari kwao licha ya kuwa walishanipangia na hatua zote za mwanzo nilifanya.

"Ni mwanamke mkorofi sana, nimejaribu kila njia kumuweka sawa lakini wapi? Ndugu, jamaa, wachungaji tumewapotezea muda wao hadi najuta kwa nini nisingemuacha mapema sana.

"Sikuwahi kumpiga wala kumtukana matusi mabaya kwa kuwa nilimpenda sana ila sikupenda tabia zake. Kilichotokea hadi kuachana nilimpiga hadi akazimia baada ya kunifanyia jambo la ajabu sana.

"Kesi ilifika maeneo husika wafanya maamuzi wakafanya ila akadai anafuta kesi ila tuachane na mimi nikalipokea kwa mikono miwili swala la kuachana kila mtu aishi maisha yake, maana ningeuwa sijui ingekuwaje na huwa sina mtindo huo wa kupiga na hata siku hiyo sijui ilikuwaje hadi leo najiuliza sina jibu. Mbaya zaidi nilimpiga kipigo kimoja tu sikuongezea hata kumgusa na kidole na akatupa macho juu mara tatu, nilijua nimeuwa.

"Anyway, kufupisha nimeamua kumwachia kila kitu ndani ya chumba tulichopanga na nimeenda kuishi sehemu nyingine nianze upya kujipanga mambo ya ndani, lakini cha ajabu kablock simu zote za kwangu nikitaka kuwasiliana na mtoto.

"Maana mtoto anaongea, anasema niwe naazima simu kwa watu na kuhusu matumizi au kumuona mtoto niwe naenda alipo kwenye biashara yake au kwake na mimi sitaki tena kumsogelea kabisa.

"Tukiachana na kipigo, kesi na yote yaliyotokea naomba kuuliza, ni sahihi yeye kuniblock wakati tuna mtoto na je mimi niridhike nisimtafute au niendelee kutumia njia ya kuomba simu ambapo nikipiga anapokea na anampa mtoto tunaongea?

"Mazingira nilipopata hifadhi wakati najipanga nipate kwangu anapajua, sasa amekuwa akija nyumba hiyo na kuita dada mmoja mpangaji pale pale na wanaongea kilugha chao hata sijui huwa wanaongea nini!

"Akikutana na washikaji zangu anawauliza kama nipo bado mjini au nimeondoka home kwetu, kwa sababu kabla ya ugomvi anajuaa nilikuwa na safari ya kwenda home mkoani.

"Kiufupi anafatilia kila hatua yangu ya maisha kwa sasa. NIMEFIKIRI SANA KUWA BADO ANANIPENDA NA ANATAMBUA ALIKUWA NA KOSA NDIYO MAANA NILIMPIGA. Kinacho msumbua ni shinikizo la ndugu na jamaa pengine na marafiki japo sina uhakika. Narudia tena, simpendi hata kimaisha kanirudisha sana nyuma.

"Sitaki tena kuwa mdhaifu kwake japo inaniuma kuishi bila mwanangu.

"Naomba ushauri nifanyeje?"

Mwisho wa kunukuu.
 
Kiufupi anafatilia kila hatua yangu ya maisha kwa sasa. NIMEFIKIRI SANA KUWA BADO ANANIPENDA NA ANATAMBUA ALIKUWA NA KOSA NDIYO MAANA NILIMPIGA kinacho msumbuwa ni shinikizo la ndugu na jamaa pengine na marafiki japo sina uhakika. Narudia tena simpendi hata kimaisha kanirudisha sana nyuma. Sh....t!
Huyu hashauriki.
Kauli hizo hapo juu ni za kijana ambae bado hajajua kama anampenda huyo mkorofi wake ama la.
Angekua amechochora asingekua anafuatilia haya yote bali angejikita kwenye kutafta njia mbadala ya kudeal na mwanae kiutu uzima zaidi kama vile kwenda huko kwa hao wanaowasuluhisha wapange utaratibu n.k.
 
Huyu hashauriki.
Kauli hizo hapo juu ni za kijana ambae bado hajajua kama anampenda huyo mkorofi wake ama la.
Angekua amechochora asingekua anafuatilia haya yote bali angejikita kwenye kutafta njia mbadala ya kudeal na mwanae kiutu uzima zaidi kama vile kwenda huko kwa hao wanaowasuluhisha wapange utaratibu n.k.
Sijakuelewa mkuu.hashauriki kivipi?

Ufafanuzi plz!
 
Amekwambia uende kwake, mtego huo, kuna styles mpya zimetoka, "maridhiano ya bandari" na nyingine "ujenzi wa bandari ya Bagamoyo" hiyo ya pili ni kiboko lazima usalimu amri na urudishe majeshi upyaaaa.
Akienda nyumbani si atarudi kulekule kama.anavyolalama keshapoteza hadi vitu vya msingi sababu ya manyanyaso ya huyo duu!
 
Back
Top Bottom