Nifanyaje ili niache kupanga? Kipato 400,000 kwa mwezi

Niliishi na wategemezi 5, bajeti ilikuwa 10,000 kwa siku ukitoa gas, umeme.
Hiyo ni chakula tu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Aiseee kweli hela haitoshi mboga ni dagaa, maharage, kabichi nyama ni siku za kuhesabu kuku ndo kabisaaaa, matunda mpaka itokee tu bahati njiani unanunua kipande cha 200.
Sasa hivi tupo watatu elfu kumi inatosha na change inabaki ni mwendo wa samaki, fresh juice, mboga za majani, uji wa lishe, maziwa asubuhi.
Life kidogo tu naenjoy.
Back to mleta mada kuwa na kabiashara kadogo usitegemee mshahara.
Buni biashara aiseee.
Kama una wategemezi, tufanye unaishi nao nyumbani.
Piga budget ya elfu 5 kwa siku. Wapike chakula nyumbani.
Kwa mwezi ni laki na nusu.

Wewe chai utakunywa nyumbani na dinner, lunch utakula kazini isizidi 2000 kwa siku. Kwa mwezi 50000.

Jumla 200k. Baki 200k.

Sasa hapa inabidi usave 100k kwa ajili ya ujenzi na 100k kwa ajili ya dharura kila mwezi.

Hapa utaweza kujenga kama una kiwanja tayari na utaanza kidogo kidogo.

Pia tafuta kazi za ziada za ku raise kipato chako. Kama umeoa na mke ajishughulishe ili aweze kukusaidia majukumu ya nyumbani mfano chakula nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo unatakiwa uache starehe za kukaa bar,kama unataka kuoa oa mke ambae ataendana na kipato chako,
 
Kimsingi hiyo ni pesa kubwa sana kama yuko kijijini au kwenye miji midogo lakini kama yuko miji mikubwa hapo ni mtihani
Ushauri ni kwamba ajitahidi kulima ili apunguze gharama za chakula na kupata kipato cha ziada..Kama uko mjini ukijitahidi ku sevu ni laki kwa mwezi ambapo itakuchukua miaka si chini ya 7 kuweza kujenga nyumba na kuhamia
 
swali gumu sana kichaa pekee yake anaweza kulijibu kwa mtu mwenye akili timamu hawezi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
piga chakula tu, nauli ya mwezi , umeme au mafuta ya taa, mkaa , hapo una ndugu yoyot, wala mtoto na mke au watoto, 400,000/ sio pesa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
aisee, nashukuru sana, naahidi kujenga kwa mawazo yenu haya ya kufanikiwa, nitaleta mrejesho hapa miaka kadhaa ijayo, barikiwa sana!!!
 
Mkuu mi nakupinga vibaya mno kutaka kujenga. Mi nakushauri umiza akili ni namna gani uatongeza kipato maradufu. Badala ya kujiuliza vipi uongeze kipato wewe umewahisha kujiuliza kivipi ujenge. Nakuhakikishia utatumia nguvu nyingi vibaya mno na utaishi kama shetani. Kama una familia utaitesa mno. Sasa ufanye nini?
Piga hesabu yako nzuri kabisa ya kujibana. Lets say utatumia 250,000 kwa mwezi (uhalisia wa kutumia laki mbili kamili siuoni). Hiyo 150,000 unayobaki nayo idundulize kwa miezi mitatu utakuwa na 450,000 kisha ifanya mtaji.

Hapa ndo akili ifanye kazi nzito, buni biashara au njia yoyote ya kukupatia wastani usio chini ya 8,000 kwa siku. Hii hela ukianza kuipata usiifanye iwe ya matumizi yako ya kila siku maana kumbuka ukila faida yote biashara haikui au itakufa kabisa. Sasa unajua nini, hiyo elfu nane usiyoigusa fanya kuizidisha kwa mwezi:
8,000×30= 240,000. Tusijipendelee hivo, fanya tutapata 200,000 tu.

Hiyo 200,000 ya faida ya biashara kila mwezi ijumlishe na ile savings ya kila mwezi ya mshahara: 200,000+150,000=350,000.
Kumbe utatumia miezi 3 kudunduliza mshahara 450,000. Mwingine mmoja kuifanya biashara, unaofuata tena ukijumlisha savings na faida ndo unakuwa na hiyo 350K. Jumla miezi mitano.

Chukua 350,000 kila mwezi uirudishe kwenye mishe hiyohiyo uzungushe (kumbuka ulichagua biashara unayoiamini na unayoimudu). Unafanya hivi kwakuwa umeajiriwa hivo huna nafasi ya kufanya mishe nyingi, wewe hadi muda huu bado ni mfanyakazi sio mjasiriamali.

Mwezi wa sita ukiwekeza hiyo 350K maana yake unaikuza, na unaendeleza wala sio kuanza. Ile 450K uloanza nayo + 350K = 800,000.
Badala ya kupata 8,000 faida kwa siku utapata wastani wa 15,000 faida.
NB: Hizi gharama za uendeshaji utajua ukouko chamsingi faida ndo naisemea.

Mwezi wa saba unauanza ukiwa na 150,000 salary + (15,000×30) faida ya mwezi ulopita thats 450,000= 600,000.
800,000 iliyokuwepo kwenye mzunguko plus 600,000 faida ya mwezi huu jumla 1,400,000. Sasa wewe nani ufanye kazi kwa kujinyima miezi nane yote, ukute utaumwa, utapata tatizo fulani au labda utakwama kuna mzigo umeagiza kiasi fulani hakijafika. Mkusanyiko wa shida zote hizi tuusawazishe kwa kusema ndani ya miezi 11 yote, miezi nane ndo ilikuwa ya neema.

2021 utauanza ukiwa na hakika ya 1.4M kwa mwezi kwenye biashara hivo ndo nafasi ya kuamua kuacha kazi au kuendelea nayo. Hiyo biashara assume imefikia ukomo wa kuendelezwa hivo inabidi utafute nyingine. Sasa utatulizana utafute kiwanja na uanze ujenzi.

Mwenzako mwenye salary ya laki nne kama wewe akidunduliza ili ajenge, mpaka anamaliza atakuta una nyumba, gari, madogo wako shule nzuri, wale tegemezi washaongezeka, na neema juu ya neema.
NB: Ukinielewa 65% tu utafanikiwa. Hebu mimi nikafue nguo zangu then niende home wanipe hela ya kutumia maana nina shilingi mia sita tu hapa.
 
Mkuu mi nakupinga vibaya mno kutaka kujenga. Mi nakushauri umiza akili ni namna gani uatongeza kipato maradufu. Badala ya kujiuliza vipi uongeze kipato wewe umewahisha kujiuliza kivipi ujenge. Nakuhakikishia utatumia nguvu nyingi vibaya mno na utaishi kama shetani. Kama una familia utaitesa mno. Sasa ufanye nini?
Piga hesabu yako nzuri kabisa ya kujibana. Lets say utatumia 250,000 kwa mwezi (uhalisia wa kutumia laki mbili kamili siuoni). Hiyo 150,000 unayobaki nayo idundulize kwa miezi mitatu utakuwa na 450,000 kisha ifanya mtaji.

Hapa ndo akili ifanye kazi nzito, buni biashara au njia yoyote ya kukupatia wastani usio chini ya 8,000 kwa siku. Hii hela ukianza kuipata ifanye iwe ya matumizi yako ya kila siku lakini kumbuka ukila faida yote biashara haikui au itakufa kabisa. Sasa unajua nini, hiyo elfu nane usiguse fanya kuizidisha kwa mwezi:
8,000×30= 240,000. Tusijipendelee hivo, fanya tutapata 200,000 tu.

Hiyo 200,000 ya faida ya biashara kila mwezi ijumlishe na ile savings ya kila mwezi ya mshahara: 200,000+150,000=350,000.
Kumbe utatumia miezi 3 kudunduliza mshahara 450,000. Mwingine mmoja kuifanya biashara, unaofuata tena ukijumlisha savings na faida ndo unakuwa na hiyo 350K. Jumla miezi mitano.

Chukua 350,000 kila mwezi uirudishe kwenye mishe hiyohiyo uzungushe (kumbuka ulichagua biashara unayoiamini na unayoimudu). Unafanya hivi kwakuwa umeajiriwa hivo huna nafasi ya kufanya mishe nyingi, wewe hadi muda huu bado ni mfanyakazi sio mjasiriamali.

Mwezi wa sita ukiwekeza hiyo 350K maana yake unaikuza, na unaendeleza wala sio kuanza. Ile 450K uloanza nayo + 350K = 800,000.
Badala ya kupata 8,000 faida kwa siku utapata wastani wa 15,000 faida.
NB: Hizi gharama za uendeshaji utajua ukouko chamsingi faida ndo naisemea.

Mwezi wa saba unauanza ukiwa na 150,000 salary + (15,000×30) faida ya mwezi ulopita thats 450,000= 600,000.
800,000 iliyokuwepo kwenye mzunguko plus 600,000 faida ya mwezi huu jumla 1,400,000. Sasa wewe nani ufanye kazi kwa kujinyima miezi nane yote, ukute utaumwa, utapata tatizo fulani au labda utakwama kuna mzigo umeagiza kiasi fulani hakijafika. Mkusanyiko wa shida zote hizi tuusawazishe kwa kusema ndani ya miezi 11 yote, miezi nane ndo ilikuwa ya neema.

2021 utauanza ukiwa na hakika ya 1.4M kwa mwezi kwenye biashara hivo ndo nafasi ya kuamua kuacha kazi au kuendelea nayo. Hiyo biashara assume imefikia ukomo wa kuendelezwa hivo inabidi utafute nyingine. Sasa utatulizana utafute kiwanja na uanze ujenzi.

Mwenzako mwenye salary ya laki nne kama wewe akidunduliza ili ajenge, mpaka anamaliza atakuta una nyumba, gari, madogo wako shule nzuri, wale tegemezi washaongezeka, na neema juu ya neema.
NB: Ukinielewa 65% tu utafanikiwa. Hebu mimi nikafue nguo zangu then niende home wanipe hela ya kutumia maana nina shilingi mia sita tu hapa.
BARIKIWA MNO!!!
 
Habari wakuu?

Kwa kipato cha 400,000 kwa mwezi nibajeti vipi mambo yangu mpaka nifanikiwe kujenga? Sina wategemezi wengi, hawafiki watano kwa jumla yao. Kipato hicho hakibadiliki sana kwa kila mwezi, niambie ni mbinu gani ulitumia kufanikiwa kujenga kwa kipato kama hicho au unaweza kufanyaje kwa kipato hicho ukajenga?

Maoni yako yanaweza kumsaidia na mwingine mwenye shida kama yangu.

Tafuta namna ya kujiongezea kipato. Kwa uhalisia kipato chako ni kidogo, hapo utaishia kula tu na kamwe hakitakuwezesha kujenga!
 
Habari wakuu?

Kwa kipato cha 400,000 kwa mwezi nibajeti vipi mambo yangu mpaka nifanikiwe kujenga? Sina wategemezi wengi, hawafiki watano kwa jumla yao. Kipato hicho hakibadiliki sana kwa kila mwezi, niambie ni mbinu gani ulitumia kufanikiwa kujenga kwa kipato kama hicho au unaweza kufanyaje kwa kipato hicho ukajenga?

Maoni yako yanaweza kumsaidia na mwingine mwenye shida kama yangu.
ACHAKAZIII
SOLN
UTAJENGA
 
Back
Top Bottom