Tatizo wanaohamasisha haya mambo ya digital wanaangalia zaidi Dar ambako matumizi ya antenna ni makubwa wakati mikoani pamoja na antena zinashika lakini asilimia kubwa wanapendelea zaidi cable ambapo anapata channel nyingi na zipo clear pia wengine wengi wana-madish hivyo wanapozungumza mambo ya digital wanasahau kwamba kuanzia Manyoni, Igunga, Nzega, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Musoma, Bukoba, Iringa, Njombe, Songea huku wengi wanatumia madish na cable ila kuanzia Dom, Moshi mpaka Dar huko ndio antenna zinatumika kwa wingi hivyo kwa kuwa serikali ipo huko na wahusika wengi wa serikali wanafika maeneo hayo mara kwa mara na kwa kuwa wanatumia hizi antenna kwa wingi wamebaki kuangalia upande huo tu wa antenna wanashindwa kuwaambia wale wa ma-dish wafanyaje. Mbaya zaidi hata wamilki wa tv station zilizopo kwenye dish hawaongei nao wanakomaa na ving'amuzi wakati kiukweli kwa mikoani wao walishajizoelea madish na cable