Nielewesheni kuhusu haya madish

zefounda

Member
Nov 26, 2012
97
19
Nilianza kusikia muda mrefu kuhusu kuingia kwenye huu mfumo wa digitally.ninachoomba nieleweshwe ni kwamba,hivi sasa ninatumia dish ambalo linaniwezesha kuona local chanels na baadhi ya chanels za nigeria,swali je siraweza kulitumia tena dish na receiver hii baada ya kugeuka kwa huo mfumo? Lakini pia mbona hii receiver imeandikwa satelite digital receiver?
 
Tangu 16:53 hadi 22:18 kuna 58 vews lakini hakuna jibu, basi wote hatujui! kibaya zaidi hata TCRA katika matangazo yao hili wanalificha kimtindo...
 
Haya madish makubwa yataendelea kutumika coz yanatumia digital. Hivyo they are still useful and they will be used 2. Ndivyo nijuavyo kama nimekosea naomba kurekebishwa
 
Nilianza kusikia muda mrefu kuhusu kuingia kwenye huu mfumo wa digitally.ninachoomba nieleweshwe ni kwamba,hivi sasa ninatumia dish ambalo linaniwezesha kuona local chanels na baadhi ya chanels za nigeria,swali je siraweza kulitumia tena dish na receiver hii baada ya kugeuka kwa huo mfumo? Lakini pia mbona hii receiver imeandikwa satelite digital receiver?

Mkuu kwa knowledge yangu ndogo ya haya mambo ni kwamba all decorders support digital transmission na ni njia pekee inayomuwezesha mtu mwenye TV set isiyo support digital transmission kupata matangazo kwa hiyo yeyote anayetumia decorder (king'amuzi) kiwe ni cha Channels za bure ( free to air, FTA kama cha kwako) au cha kulipia kama DSTV ataendelea kupata matangazo kama kawaida bila kujali aina ya TV set aliyonayo. Kwa kuongeza hata wale wanaopokea signal kwenye TV zao kwa njia ya cable services pia hawataathirika na haya mabadiliko kwa kuwa kabla ya kumfikia mtu wa mwisho matangazo hayo yanakuwa yameshapita kwenye king'amuzi. Tupo pamoja mkuu?
 
Na hivi ni kweli kwamba warushaji ikiwa ni pamoja na Dstv wako obliged kurusha na local channels pia? Hii itatuepusha kulazimika kuwa na decoder zaidi ya moja.
 
Tatizo wanaohamasisha haya mambo ya digital wanaangalia zaidi Dar ambako matumizi ya antenna ni makubwa wakati mikoani pamoja na antena zinashika lakini asilimia kubwa wanapendelea zaidi cable ambapo anapata channel nyingi na zipo clear pia wengine wengi wana-madish hivyo wanapozungumza mambo ya digital wanasahau kwamba kuanzia Manyoni, Igunga, Nzega, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Musoma, Bukoba, Iringa, Njombe, Songea huku wengi wanatumia madish na cable ila kuanzia Dom, Moshi mpaka Dar huko ndio antenna zinatumika kwa wingi hivyo kwa kuwa serikali ipo huko na wahusika wengi wa serikali wanafika maeneo hayo mara kwa mara na kwa kuwa wanatumia hizi antenna kwa wingi wamebaki kuangalia upande huo tu wa antenna wanashindwa kuwaambia wale wa ma-dish wafanyaje. Mbaya zaidi hata wamilki wa tv station zilizopo kwenye dish hawaongei nao wanakomaa na ving'amuzi wakati kiukweli kwa mikoani wao walishajizoelea madish na cable
 
Hilo la DSTV sina uhakika. Ila nilipata kumsikia bwana mmoja kutoka TCRA anaelezea kuhusu obligation ya makampuni yenye kuuza ving'amuzi ( Star times and the like) yanalazimika kuweka national TV channels zote ( hapa nadhani alikusudia local channels zinazorusha thru satellites) kama TBC,STAR TV,CHANNEL TEN, ITV etc. Kwa hiyo yatakuwa yanashindana katika channels za ziada/kulipia. Na hizo national channels zitakuwa zikipatikana hata kama haujalipia king'amuzi husika.
 
Tatizo wanaohamasisha haya mambo ya digital wanaangalia zaidi Dar ambako matumizi ya antenna ni makubwa wakati mikoani pamoja na antena zinashika lakini asilimia kubwa wanapendelea zaidi cable ambapo anapata channel nyingi na zipo clear pia wengine wengi wana-madish hivyo wanapozungumza mambo ya digital wanasahau kwamba kuanzia Manyoni, Igunga, Nzega, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Musoma, Bukoba, Iringa, Njombe, Songea huku wengi wanatumia madish na cable ila kuanzia Dom, Moshi mpaka Dar huko ndio antenna zinatumika kwa wingi hivyo kwa kuwa serikali ipo huko na wahusika wengi wa serikali wanafika maeneo hayo mara kwa mara na kwa kuwa wanatumia hizi antenna kwa wingi wamebaki kuangalia upande huo tu wa antenna wanashindwa kuwaambia wale wa ma-dish wafanyaje. Mbaya zaidi hata wamilki wa tv station zilizopo kwenye dish hawaongei nao wanakomaa na ving'amuzi wakati kiukweli kwa mikoani wao walishajizoelea madish na cable

Ni kweli mkuu,ufafanuzi hautolewi kwa kiasi cha kutosha. Hii inawafanya watu hata wale wa sehemu kama Kigoma ambako wameshazoea FTA channels kupitia dishes and decorders kuanza kuchanganyikiwa kuwa wafanyaje ifikapo 31-12-2012. Wakati haiwahusu!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom