Nidhamu na motisha katika kufikia malengo (discipline and motivation in achieving goals)

Powell Gonzalez

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
622
1,276
Kabla sijazungumzia kuhusu nidhamu na motisha ( discipline and motivation) Nianze Kwa kutoa mfano, Hapo zamani kidogo nilipokuwa nasoma sekondari nilikuwa napenda Sana kuangalia filamu za akina Vin Diesel, Dwyn Johnson na akina Jason Statham nilipokuwa olikizo.

Basi siku Moja nikawa naangalia filamu Moja ya Jason Statham inaitwa Mechanics, wakati naangalia Ile filamu nilikuwa naangalia na msichana mmoja ambae alikuwa ni ni mrembo, au niseme nilikuwa pengine navutiwa nae kuliko wasichana wote Kwa kipindi hicho, lakini sikuwa nimewahi kufungua kinywa kumwambia kuwa nampenda pengine ni utoto.

Basi wakati filamu inaendelea ikafika mahali ambapo Muhusika mkuu,yaani Jason Statham alikuwa kavua Shati, yupo kifua wazi, Kwa wanaomfahamu Statham, Alikuwa na mwili uliokatika kimazoezi, kifua kipana tumbo lenye bustani Sita (six park) na vitu kama hivyo. Basi Yule binti pembeni ambae naweza kusema Kwa lugha nyepesi She Was my crush akawa amesema " Huo ndio mwili wa Mwanaume ninaemuhitaji " Ile kauli ikawa imenipa majibu kuwa kumbe crush anahitaji mwanaume wa Namna hii? Nikaona Sina jinsi zaidi ya kuwa vile anavyotaka ili nimvutie pengine. Basi kutoka hapo nikaanza kutafuta sehem ya kufanya mazoezi ili niwe na ule mwili wa Jason Statham nimpagawishe mchumba!

Kwa kuwa sikuwa na pesa nyingi ya kulipia basi nilipata sehem Moja ya mazoezi ( Gym) ambapo kuliwa na gharama nafuu, ilikuwa elfu Kumi Tu Kwa mwezi, nikalipia kisha nikatoa maelezo Kwa Yule ambae ndio angekuwa Trainer wangu nakumbuka swali langu kumuuliza ilikuwa ni itachukua mda gani kuwa na " chest" pamoja na " six park" jamaa akaniambia ukiwa na Nidhamu basi baada ya wiki tatu utaanza kuona matokeo.
Sikuelewa alichomaanisha kusema "nidhamu" Ila I didn't care all I needed was a sex body ili nimvutie binti wa watu! Basi nikaanza mazoezi kesho yake Tu tena Kwa motisha Sana, haikuwa rahisi lakini nilifanya kila nilichoelekezwa kwa siku mbili za Mwanzo, nilienda mara mbili kama nilivyoambiwa, lakini baada ya siku nne Tu sikuwa na motisha tena ya kwenda gym, nilishasahau kama hata nimelipia pesa, sikuwaza hata kwamba nilikuwa nahitaji mwili sexy Kwa ajili ya kumvutia crush, motisha wote ulikuwa umekwisha na sikuwahi kurudi tena gym!

Sikuwahi kupata majibu kwanini niliacha kwenda Gym wakati nilianza Kwa morale ya kufa mtu!
Lakini hapa ninapoandika basi Nina majibu, na ndio maana nikaandika! Keep reading!

Kiufupi ni Kwamba unapokuwa Una lengo la kufanya kitu fulani, iwe katika Masomo, biashara, mazoezi, au chochote kile basi mwili huwa na tabia ya kutengeneza kitu kinaitwa " Motisha" ( Kwa lugha ya Kule mbali wanaita Motivation) Motisha huwa ni matokeo ya mwili kutoa homoni ambayo wanabiolojia wanaita Dopamine, basi homoni hii huwa inakazi ya kukupa motisha Wa Kuanza kufanya jambo fulani Kwa kuwa unaamini ni zuri na litakusaidia kufanya kitu fulani.

Na hii Motisha huja pale unapokuwa unatamani kuwa na kitu au kufikia malengo fulani. Kwa mfano unahitaji kuwa na biashara, ukapata wazo kuwa biashara nzuri ni kuanza Kuuza nguo kwa kuwa ulimuona Mtu anabiashara hiyo na amefanikiwa au, umeona hii ni fursa nzuri basi unakuwa motivated Kuanza kuifanya, kuwa motivated inamaanisha kwamba ubongo umetoa homoni ya dopamine ambayo inakupa nguvu na ujasiri wa kutosha Kuanza kufanya hicho unachataka kukifanya.

Kitu cha ajabu ni kwamba Kwa kuwa hii Motisha ni matokeo ya homoni basi huwa haidumu huwa ni ya muda mfupi tu, huwa ina kazi ya kukufanya uanze, Ila baada ya Mda huwa Inakata. Hii ndio sababu huwa unaanza kufanya kitu Kwa motisha lakini baada ya muda unakuwa hujisikii tena kukifanya hicho kitu. Kumbuka kwenye hadithi yangu Huko juu, basi pale Mimi nilipata motisha lakini baada ya siku nne Motisha ilikata, Ndio maana Trainer alisema nikiwa na "nidhamu" basi nitafanikiwa.

Kwa hiyo Nidhamu huwa inachukua nafasi baada ya Motisha kukata. Nidhamu inamaanisha kufanya kile ulichokianzisha mpaka ukimalize, iwe unataka au hautaki. Nidhamu (self discipline) inamaanisha kuwa unaheshimu mipango yako vilivyo, yaani kama ratiba yako ni kuamka Saa 11 kila siku na kufanya Kazi Hadi Saa 9 basi , lazima ufanye hivyo kila siku Uwe unataka au hutaki. Kama ulianzisha biashara na inakutaka Uwe unaifanya kila siku mpaka Saa Sita usiku, basi ukiweka nidhamu inamaanisha utakuwa unafanya hivyo kila siku.

Kwa hiyo kila Mtu huwa anakuwa na motisha lakini sio kila huwa anakuwa nidhamu, Kwa sababu Mtu akiwa na motisha basi atafanya kitu huku akiwa anakipenda, lakini discipline means you have to it whether you want or don't.

Sio rahisi kuwa na nidhamu hata kidogo, ndio maana wengi huanzisha vitu alafu wanaishia njiani. Sio rahisi kuwa na nidhamu ndio maana hata mwanafunzi huwa analazimishwa kuwa na nidhamu, yaani afike shuleni Kwa Muda na akae Hadi atakaporuhusiwa, akienda kinyume anapewa adhabu lakini bado ni wanafunzi wachache Tu ndio huwa wanakuwa na nidhamu. Sasa Kama mwanafunzi ambae anasimamiwa tena Kwa adhabu anashindwa kuwa nayo , vipi wewe ambae husimamiwi na hupewi adhabu?

Ni hii self discipline ndio itakufanya Jambo lako mpaka litimie, ni hii nidhamu ndio itakufanya usikate Tamaa, ni nidhamu ndio itakufanya ilupambane na changamoto ilimradi Jambo lako litimie. Ni vizuri kujua kuwa wakati unaanza kufanya jambo basi hiyo ni motisha inakuongoza kufanya, na ujue kuwa kuna siku hiyo motisha haitakuwepo hivyo itabidi uendelee kufanya Tu Kwa nidhamu hata kama hujisikii kuendelea tena.

Huwezi kuwa na motisha siku zote hata Uwe unahitaji kiasi gani kufanikiwa au kupata kitu.
Kwenye Ile hadithi yangu, Kama ningekuwa na nidhamu basi ningejilazimisha kwenda Gym hata kama nilikuwa sitaki mpaka nitimize Lengo langu!

Mara kadhaa nimewahi kuwaona wanafunzi wakianza likizo Kwa kwenda shule kila siku na kusoma Kwa bidii wakiwa na lengo la kufaulu lakini baada ya Mda wanaacha, discipline!

Sasa nianze kuzungumzia jinsi ya kujenga self discipline!

Ila ngoja kwanza nione mmeipokeaje mada, nikiona mmeipokea vizuri basi nitarudi kuzungumza kuhusu jinsi ya kujenga self discipline.
RAPHAEL KALOLO.
mail: raphaelmathewkalolo@gmail.com


364d94b37e6ebb381523a8d82b40dce1.jpg
 
Back
Top Bottom