Tunaomjua Mwamba wa Lusaka (Chama) na makubwa aliyoyafanya katika ligi hii lazima tutafakari tuhuma alizopewa kuwa ni mtovu wa nidhamu

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,295
12,790
Timu za kariakoo (Simba sc na Yanga Sc) Hawa mapacha huwa wanakasumba sana haswa Hawa viongozi wanapoulizwa kuhusu suala la masilahi.

Nimemshuhudia Chama (kipenzi Cha mashabiki) akicheza mpira katika ligi yetu hii kwa nidhamu kubwa kwa misimu kadhaa bila kusikia kakwaruzana na mchezaji mwenzie au kiongozi mwenzake je leo hii Kuna Nini kwa Chama?

Tulizoea kusikia Mkude kafanya hivi au Benard Morson kafanya kile hapo nzungumzia wakiwa Simba sc acha Yanga Sc kwa Bernard morsoni watu Kama Hawa mwisho wa siku mashabiki tulizoea kutokana na utundu wao.

Aliachwa Saidoo ntibazonkiza pale Yanga Sc juu juu tu hakuna sababu ya maana iliyoelezwa, hii ni kasumba kwa timu yetu/timu zetu za Kariakoo na hii hutokana na viongozi kutoa ahadi zisizo na vitendo na wachezaji wakihoji wanaonekana ni watovu wa Nidhamu.

Maoni Yangu: ifike hatua timu za kariakoo ziache janja janja haswa kwenye masilahi/posho za wachezaji.

Hakuna shabiki wa Simba sc na Yanga Sc asiyejua kuwa Chama kwenye Suala la nidhamu yupo vizuri Ila janja janja za viongozi wa kariakoo huwa zinatengeneza hadithi za kumtoa mtu kwenye Reli.

Nawasilisha hoja.
 
Utovu wa nidhamu ni nini?

Lazima ujue kwanza maneno hayo yanamaana pana sana. So usikimbilie ku judge.

Cha msingi ni hao wanaosema kuwa ana utovu wa nidhamu wabainishe ni kipi alichofanya kila mtu afahamu.

Simba ni taasisi, kwanini wanaficha taarifa muhimu? Kulikuwa na haja gani yakurelease hiyo statement kisha kuficha huo utovu wenyewe?
 
Hoja yako umeielezea upande mmoja tu wa Chama.

Chama kila kipindi cha usajili huwa anakuja na drama zake.

Nitajie mwaka gani ambao msimu wa usajili umefika hujasikia longolongo za Chama

Akifakisha achukuliwe hatua na hiyo ndio inapaswa kuwa nidhamu endelevu, wachezaji wajue kuheshimu mamlaka.

Sisi mashabiki na sisi tutambue kuwa wachezaji wetu tunaowapenda tuna fursa ya muda mdogo sana ya kumuona mchezaji.

Katika huo muda ni awapo kiwanjani tu, na akiwa hapo hutamuona akiongea.

Maana yake kuna mengi yanayofanyika akiwa eneo ambalo sisi mashabiki hatupo.

Eneo hilo ndio sehemu anayopata fursa ya kuongea na kufanya mambo mengi ambayo mengine pengine hata sisi mashabiki tungepata fursa ya kuyaona kama si kupunguza mahaba yetu basi tungeweza kumchukia mazima.

Sasa kama huko ndio anafanya mambo yanayokiuka sheria, sisi mashabiki hatuwezi kuwa na guts za kuwalaumu viongozi kwa adhabu watayotoa kisa tu ni mchezaji kipenzi.
 
Simba ni kubwa kuliko mwajiriwa yoyote! Makubwa aliyoyafanya yasimfanye aone ndo kila kitu, kama kakosea ni lazima aadhibiwe. Hakuna sheria inayomuexclude mchezaji kisa mchango wake ktk klabu.
Unajua kafanya nini kwanini tusielezwe alichofanya tukipime
 
Unajua kafanya nini kwanini tusielezwe alichofanya tukipime
Ukikipima baadae utamuondolea adhabu iliyotolewa? Au unahisi club inaonea wachezaji? Suala limepelekwa kamati ya nidhamu likajadiliwe, we ni nani haswaa na why midomo kwa chama mbona hamuongelei Kapama? Mapenzi yenu kwa mchezaji isiwe kigezo cha kuona fulani kaonewa, acha kamati husika ilitazame.
 
Simba ni kubwa kuliko mwajiriwa yoyote! Makubwa aliyoyafanya yasimfanye aone ndo kila kitu, kama kakosea ni lazima aadhibiwe. Hakuna sheria inayomuexclude mchezaji kisa mchango wake ktk klabu.
Except BOKO maana jua limeshakua la saa 12, lakini tukikumbuka mchango wake kwa klabu, watuwezi kumpa thenk yuu.
 
Simba ni kubwa kuliko mwajiriwa yoyote! Makubwa aliyoyafanya yasimfanye aone ndo kila kitu, kama kakosea ni lazima aadhibiwe. Hakuna sheria inayomuexclude mchezaji kisa mchango wake ktk klabu.
KAKOSEA NINI HUYO CHAMA?
LAITI KAMA WACHEZAJI WANGEKUA WANAJIELEZA/ELEZA MBELE YA CAMERA WALAHI TUNGEKIMBIA.
 
Kama amezingua acha apate mfungo,hatuwez kuabudu mchezaji kana kwamba yey ndo kaibeba club toka 1936!ila tu pasiwepo uonevu kama amezingua acha aonje mfungo
 
Hoja yako umeielezea upande mmoja tu wa Chama.

Chama kila kipindi cha usajili huwa anakuja na drama zake...
Unaweza kusema chama kasimamishwa kwa sababu gani?

Kuhusu suala la chama kwenye usajili kuleta drama hiyo ni awaida kaja kutafuta pesa hapa lazima atingishe walau hata mkataba usome achukue kibunda.

Hakuja kuimbwa bila masilahi siyo klabu ya baba ake hii.
 
Back
Top Bottom