NIDA Ukonga ni jipu sugu!

Yudatade Edesi Shayo

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
2,903
4,306
Hivi ni kwamba waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi kubwa kama nida wameishiwa maarifa kabisa? Ukifika NIDA Ukonga pale hutoamini kama hizi ni zama za sayansi na tekinolojia.

Foleni ni ndefu na watendaji ni wachache mtu unapoteza siku nzima na huduma hupati.

La kushangaza hakuna hatua zinazochukuliwa wakati watu wanaumia.

Labda Rais Magufuli ukifanya ziara pale Ukonga Gerezani upite na NIDA Ukonga pale labda ukitoa maagizo wewe mambo yatabadilika sababu hali siyo nzuri kwa kweli na muda unakwenda!!
 
Zoezi la vitambulisho vya taifa halijawahi kuwa serious japo lipo na linafanyika.
Upo sahihi mkuu limekuwa na malalamiko kibao ila hakuna hatua zozote zinachukuliwa na kusaidia raia kupata huduma stahiki.
 
Zoezi la vitambulisho vya taifa halijawahi kuwa serious japo lipo na linafanyika.
Kabisa kabisa mkuu,maana ni zoezi sensitive sana ila malalamiko ni mengi ,hakuna hatua sijui wanafanya makusudi ile waendele kupata allowance hata baada ya muda kuisha..waongezewe muda
 
Yani nikipita pale na gari naona foleni ndefu ile mbaya lakini cha ajabu ukirudi tena unakuta watu wale wale tu.inamaana hata foleni yenyewe uwa haisogei kabisa

Nasikia ukienda na kiapo cha mwanasheria kutoka sehemu nyingine unaletewa mizengwe kuwa mwanasheria uyo sio wa NIDA kwa iyo toa elfu 14 upate kiapo kwa mwanasheria wa NIDA.yani hii nchi sijui rushwa itaisha lini
 
Kabisa mkuu wana mbinu nyingi sana za kukufanya utoe rushwa unaweza enda na barua ya serekali ya mtaa wak ukaambiwa mbona muhuri umepauka sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom