Greg50
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 1,953
- 2,431
Habari wakuu,
Hawa Nida nadhani kazi waliyopewa ya kuwapa wananchi vitambulisho hawaiwezi. Sasa hivi kila huduma serikalini wanadai uwe na kitambulisho cha Taifa, kuanzia uhamiaji, TRA mpaka TCRA.
Lakini tatizo linakuja kukipata hiko kitambulisho Nida utazungushwa bila mafanikio na huku mambo yako yakichelewa. Kwanza namba zao walizoweka mitandaoni kila muda zinatumika au hazipatikani, ile huduma yao ya *152*00# inakula tuu pesa yako majibu hupati, ukienda ofisini kwao utakutana na foleni kubwa utakaa, utafika pale mbele kwa mhudumu anakwambia wewe chako bado wanakiprocess huko kibaha, rudi wiki ijayo wiki ijayo, ukienda hiyo wiki ijayo ni kalenda tena, unachoma nauli mpaka unachoka.
Tatizo hili naamini si la kwangu peke yangu bali ni watu wengi, Niwaombe serikali wampatie investor yeyote yule tenda ya kutengeneza vitambulisho, hawa Nida wabaki kukusanya documents na taarifa za wananchi tuu ila vitambulisho wasitengeneze wao.