Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,827
- 3,569
Wanapaita hospitali ya rufaa lakini vifo nje nje! Ukifika pale kwanza kasheshe ni jinsi ya kuingia ndani, mizinguo inaanza getini. Ukipenya geti ukafika ndani unakutana na foleni ya balaa, foleni kila mahali na haitembei! Na kila hatua kuna wanafunzi lukuki, ukidhani sasa ndio unatibiwa unakuta ni mwanafunzi anakupotezea muda weeeee halafu anakupasia kwa mwanafunzi mwingine unapapaswa unachokonolewa weeeee halafu unafaulishwa kwa mwanafunzi mwingine hivyohivyo hadi watosheke, hawajali maumivu yako. Wagonjwa wengi sana wamefia mikononi mwa wanafunzi.
Ukitoboa hapo kwa wanafunzi (hapo utakuwa umeshasota foleni masaa!) kama ni wa kulazwa ni kilio upyaaaa! Tatizo linaanzia kwenye ile machela ya kukupeleka wodini, utaisubiri masaa! Ikipatikana anatafutwa wa kukupeleka, masaa!
Akipatikana anakukokota kama mzigo hadi wodini, hapo utawekwa kwenye korido masaa! Kisha wanaingia kundi lingine la wanafunzi wanakuanza upyaaaa! Usife kwanini?
Watu wakachunguze ile hospitali ni balaa! Mtu anaweza kulazwa asubuhi akaanza kutibiwa usiku au hata kesho yake! Kama mtu umekodi gari ikuwahishe hospitali ya rufaa unajiuliza mara mbili ulikuwa unaharakisha nini? Hii ni jipu kabisa inatakiwa itumbuliwe harakaaaa!