Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,555
Nianze kwa kusema hivi; mwaka 2018 nilikuwa mkoani Tabora nikifanya kazi kwenye kampuni moja na ndiko nilikojiandikisha kupata NIDA. Baada ya mwaka mmoja nikarejea Dar pasipo kupata Kadi yangu, nikawa mjini kwa mda wote huo hadi 2023 niliporudi Tabora kwa masuala yangu na mara hii nilibahatika kwenda hadi ofisi ya kata ambako niliambiwa vitambulisho havijatumwa katani badala yake niende wilayani. Kufika wilayani nikaambiwa nenda mkoani, kufika huko nikaambiwa tena vitambulisho havijatoka bado.
Niliendelea kuuona huu mchakato ni usumbufu na nikaamua kuondoka tena na kurejea Dar.
Ukiachilia usumbufu nilioupata mie kuna kubwa la watanzania masikini ambao walidai kusumbuliwa vivyo hivyo kama mie na hata wengine kutakiwa kuhonga vitu mbalimbali ili kupata vitambulisho vyao.
Juzi mh. Waziri aliamua kuingilia Kati na sisi wengine tukaona walau sasa tutapata haki yetu hii japo imecheleweshwa sana, jamaa wa NIDA nao wakajifanya kucheza na akili za raia kama kawa. Kwamba sasa watu waende katani na baada ya mwezi mmoja zoezi litasitishwa,. Hapa unajiuliza, ni kwanini hadi waziri kuingilia ndo wananchi kuambiwa waende katani?
Haya, watu tukaenda katani vitambulisho vyetu kule hamna. Mie nikajaribu kumtafuta mawasiliano na katani kila namba niliyopewa siyo sahihi, mda wa mwezi umeisha mara sasa vimerudi tena wilayani. Yaani mlolongo wa NIDA ni kama unatafuta kuingia mbinguni. Mimi ni raia wa nchi hii, nimefata taratibu zote na kupoteza sana mda wangu tokea kupanga foleni hadi mizunguko kwenye maofisi yao lakini wapi.
Leo hii tunaambiwa mwezi ujao ndo mwisho wa kutumia namba na asiye na Kadi basi atajua mwenyewe na hapa ndo pana maswali lukuki. Kwanini Kadi zimekuwa zinapiga chenga kiasi hiki, ni kwanini tusiamini ni kweli kuna mazingira ya rushwa? Pili, wengine tulishabadili hadi namba za simu lakini wakasema ohoo eti wametafuta namba zetu za sasa na wametutumia sms huko, binafsi sijawahi kuiona hiyo sms yao wakinitumia wakati sms za kutoka Polis, bank, mitandao n.k zinatumwa kila siku kwangu na nazipokea ..sasa sijuhi ya kutoka NIDA inaiogopa simu yangu ama pana nini? Na je, hiyo kesho mkifunga matumizi ya namba mnataka raia badala yake wafanyaje ama ndo kwa vile nyie mna Kadi zenu na mlizipata ndani ya dakika sasa mnaona hawa masikini si lolote si chochote? Ama ni kwa vile nyie mmeshika mpini na wao wameshika kwenye makali?
Mwisho niseme, hamkuwa na sababu ya kumzuga waziri, waziri alifanya kuwasaidia wanyonge lakini kwa vile mmekuwa wanufaika wa mambo haya mkaona mumpige chenga kwa zengwe la hivi. Mnawaumiza sana raia masikini wa nchi hii na hii yote ni uzembe tu wenu maana iweje toka kuandikishwa mtu akae miaka 2 na kuendelea haujapata Kadi alafu ukianza kufatilia ndo mizunguko kibao, hapa mnakuwa mnataka nini eti? Na kama ni kwamba basi vinauzwa basi tangazeni tu wananchi tujue hata kama ni kwa laki mbili ama milioni ili tujue tunaipataje kuliko haya maigizo mnayoyafanya kwa maana nyingine mmefeli katika karne hii ya sayansi na teknolojia kujua ni kwa namna gani mnaweza kuhakikisha kila raia anapata ID yake pale alipo haijalishi kahama mkoa ama yuko mkoa uleule, uwezo wenu wa kutafakari pengine ndo hapo ulipokomea na sasa mkaanza kuwaza pesa. Kwani hapa mie napoishi leo hakuna mamlaka za serikali? Kwanini msinitake nijisajiri taarifa zije huko ili mjue niko wapi ndo mnitumie ama hili nalo mpaka mpewe seminar?