NIDA, mbona wageni wana vitambulisho na sio namba?

NIDA, mbona wageni wana vitambulisho na sio namba?

Kwa anayefaham anijuze.

Hiv kufanya ASSUANCE kwenye taarifa za NIDA inachukua muda gani?

Nahangaika na Kurekebisha majina mawili yaliyokosewa Herufi.

Mwezi wa 3 huu sijafanikisha naambiwa. ASSUANCE bado
 
Mi mwanangu alihangaika kupata kitambulisho cha NIDA karibu miezi miwili, kuna siku alipoenda ofisi za wilaya aliambiwa hasa fomu zako hazionekani....aliponiambia nikamwambia niachie kazi mimi... siku tatu tu kapata namba ya NIDA. Jamaa alienisaidia ananiambia ukitoa 20K tu unapata kadi yako kesho, ukitoa 5K utapata kile cha copy. Sitoi hata sumni, sijatulia tu lkn siku nikiwaamulia kadi ya NIDA mwanangu ataipata. Tunatakiwa kujiamini kwenye kudai haki zetu, tatizo watu wanaongea chinichini tu inawezekana habari haziwfiki wakubwa wanaohusika
 
Kwa anayefaham anijuze.

Hiv kufanya ASSUANCE kwenye taarifa za NIDA inachukua muda gani?

Nahangaika na Kurekebisha majina mawili yaliyokosewa Herufi.

Mwezi wa 3 huu sijafanikisha naambiwa. ASSUANCE bado
mmmhhh, hio ndio imetoka ikirudi pancha. Hayo majina yalokosewa ndio yashakuganda hayo. huna hata connection mkuu ukasaidiwa?
 
Mi mwanangu alihangaika kupata kitambulisho cha NIDA karibu miezi miwili, kuna siku alipoenda ofisi za wilaya aliambiwa hasa fomu zako hazionekani....aliponiambia nikamwambia niachie kazi mimi... siku tatu tu kapata namba ya NIDA. Jamaa alienisaidia ananiambia ukitoa 20K tu unapata kadi yako kesho, ukitoa 5K utapata kile cha copy. Sitoi hata sumni, sijatulia tu lkn siku nikiwaamulia kadi ya NIDA mwanangu ataipata. Tunatakiwa kujiamini kwenye kudai haki zetu, tatizo watu wanaongea chinichini tu inawezekana habari haziwfiki wakubwa wanaohusika
Punguzeni siasa kwenye mambo ya ukweli,NIDA ni tatizo,mbona vitambulisho vya kupigia kura hutoka papo kwa papo?
 
Haya mambo yana uhusiano mkubwa na umasikini wa jamii na taifa kwa ujumla.
Yanaweza kuondoka kwa;

1 Wananchi na watumishi wa serikali waeleweshwe na wajielewe waache tabia za kitumwa za kujitoa (submissive na kupendelea wageni.

2. Raia wa kuzaliwa wajue kuwa waungane kudhibiti nchi yao wakijua kuwa wao ndiyo first class.

3. Kuwadhibiti wageni wanajipenyeza serikalini na kwenye taasisi za uma.

4. Kudhibiti rushwa kwa kuwadhibiti wapokeaji na watoaji kwa kuweka hadharani (kutajwa, ushahidi hata wa kimazingira, picha, documents , transactions, accounts ...)
Hasa pale haki za raia kwa ujumla zinapopindishwa.
 
NIDA imejaaa uhuni mwingi sana, Ulaghai na ujanja ujanja na kwa sasa wamewekeza sana kwenye Media. Diily wako kwenye media kuelezea mafanikio yao ambayo kiuhalisia hayapo zaidi ya Hadaaa tupu.

Raia wazawa waliojiandilisha 2018 wana namba pekee hadi sasa na kadi wanapigwa danadana hazija printiwa.

Cha kushangaza wageni wote wawe wanapewa vitambulisho vya ukaazi au vya uraia vya magumashi au vya halali ila wote wana vitambulisho na sio number.

Wahindi wote wana vitambulisho na sio number, wahamiaji haramu wana vitambulisho vya uraia na sio number.

Kuna raia mmoja ni Mkenya sijui alifanya fanya vipi akajiandilisha NIDA wanajua utaratibu wao wanao tumia kuwapa watu wasio raia Vitambulisho vya Uraia,Sasa huyo Raia amejiandikisha mwezi wa 6 mwaka huu,na tiyali ana kadi ya kitambulisho.ELewa kwamba kajiandikisha mwaka huu mwezi wa 6 ila NIDA wameisha mpatia kitambulisho.

Raia wanasafa tangia mwaka 2018 kadi zao hazijawahi printiwa.ila kuna watu wao wanakuja nyuma tena kagumashi na wanapewa kadi.

Sasa je raia wote na wao wanyoeshe mkono kwa stafu wa NIDA ili wapate kadi?

Taasisi imejaaa hadaaa sana ila cha ajabu inasifiwa na watawala nashindwa kukua wanasifiwa kwa lipi hasa.
Corrupted system. Rushwa kila kona.
 
Kila nikifikiria raia walikuwa wanaamka saa9 ucku kwenda kupanga mstari ili kuwai namba alafu Mtu anatoka kenya leo leo ndani ya wiki 1 anapata kitambulisho cha NIDA wakati yule mzaliwa ata namba kupata nayo ni shida..
 
Naona jazba imetawala kweli Vitambulisho vinachelewa lakini hao NIDA wanatoa Id's si kwa raia tu, kuna wageni, wakimbizi na walowezi. Usishangae kuona mhindi, mchina anacho.
Lakini kuna watu wa asili mbalimbali ambao sana uraia wa kuandikisha nao wanapata cha raia.
 
Kila nikifikiria raia walikuwa wanaamka saa9 ucku kwenda kupanga mstari ili kuwai namba alafu Mtu anatoka kenya leo leo ndani ya wiki 1 anapata kitambulisho cha NIDA wakati yule mzaliwa ata namba kupata nayo ni shida..
Mbona wanatangaza kuwa vipo kwenye Serikali za Mitaa na ofisi za NIDA?
 
Basi sekta ya Uchawa ndio ipewe NIDA ili ukimsifia Maza tu unapewa fasta.
Ukikutana na Baba levo lazima akuulize majina ya watoto wa Diamond Platnumz ukishindwa unakuwa sio mtanzania, hupewi hata namba ya NIDA😆
 
Back
Top Bottom