NIDA, mbona wageni wana vitambulisho na sio namba?

NIDA, mbona wageni wana vitambulisho na sio namba?

NIDA nina namba toka 2019..nilienda mwaka 2021 nikaambiwa badoo kitambulisho
 
😂😂 kwanini Mkuu?
Sasa mkuu tatizo ni wahindi na wasomali na wa kuja au tatizo ni tamaa za wafanyakazi wasiokuwa na maadili na tamaa zao?
Nacheka kwa sababu naona lawama kwa wageni wakati hawajaiba bali wakiomba wanapewa fasta

Nchi masikini ndio ziko hivyo siwalaumu mkuu
 
Sasa mkuu tatizo ni wahindi na wasomali na wa kuja au tatizo ni tamaa za wafanyakazi wasiokuwa na maadili na tamaa zao?
Nacheka kwa sababu naona lawama kwa wageni wakati hawajaiba bali wakiomba wanapewa fasta

Nchi masikini ndio ziko hivyo siwalaumu mkuu
Mkuu njaa husababisha Roho mbaya.
 
Mkuu njaa husababisha Roho mbaya.
Halafu wanalalamika ooh nchi iko hatarini kwa usalama
Ila sio njaa mkuu ni hulka ya watu kuwa na tamaa yaani hawa wanaweza kukupa hata bunduki aliyopewa kazini
Sio kuwa hawana maisha la utakuta mpaka wakubwa wenye mshahara mnono anakuomba kilo ya nyama

Huwa siwaelewi kabisa
Na wanakuwa wabaya zaidi kila siku
 
NIDA imejaaa uhuni mwingi sana, Ulaghai na ujanja ujanja na kwa sasa wamewekeza sana kwenye Media. Diily wako kwenye media kuelezea mafanikio yao ambayo kiuhalisia hayapo zaidi ya Hadaaa tupu.

Raia wazawa waliojiandilisha 2018 wana namba pekee hadi sasa na kadi wanapigwa danadana hazija printiwa.

Cha kushangaza wageni wote wawe wanapewa vitambulisho vya ukaazi au vya uraia vya magumashi au vya halali ila wote wana vitambulisho na sio number.

Wahindi wote wana vitambulisho na sio number, wahamiaji haramu wana vitambulisho vya uraia na sio number.

Kuna raia mmoja ni Mkenya sijui alifanya fanya vipi akajiandilisha NIDA wanajua utaratibu wao wanao tumia kuwapa watu wasio raia Vitambulisho vya Uraia,Sasa huyo Raia amejiandikisha mwezi wa 6 mwaka huu,na tiyali ana kadi ya kitambulisho.ELewa kwamba kajiandikisha mwaka huu mwezi wa 6 ila NIDA wameisha mpatia kitambulisho.

Raia wanasafa tangia mwaka 2018 kadi zao hazijawahi printiwa.ila kuna watu wao wanakuja nyuma tena kagumashi na wanapewa kadi.

Sasa je raia wote na wao wanyoeshe mkono kwa stafu wa NIDA ili wapate kadi?

Taasisi imejaaa hadaaa sana ila cha ajabu inasifiwa na watawala nashindwa kukua wanasifiwa kwa lipi hasa.
Ubabaishaji ni mwingi sana
 
Back
Top Bottom