NIDA hawakujiongeza

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,604
Ilitakiwa ukikitazama kitambulishe cha taifa namba ya kitambulisho peke yake tu bila kutumia kifaa chochote ikuambie kuwa kitambulisho hiki ni cha mkazi wa Mkoa fulani, Wilaya fulani, Kata fulani na kijiji fulani. Kila Mkoa ungepewa code number yake ya kuonyesha Mkoa na wilaya zake, tarafa, kata na vijiji vyake, Hivyo namba ya kimbulisho ingeweza kusababisha kitambulisho kilichookotwa Dodoma kiweze kurudishwa Mtwara, na kikifika mtwara kipelekwe Wilaya husika hadi kijiji.

Katika usajili huu kila mkoa ungepaswa kuhangaika na wlaya zake, na kila wilaya ingehaika na tarafa zake na kila tafara ingehangaika na Kata zake na kila kata ingehangaikia vijiji vyake kikamilifu.

Namna ilivyofanyika watu wote walirundikana sehemu moja kwenye mkoa kujiandikisha na kusababisha yafuatayo:

1. watu waliokosa nauli walishindwa kusafiri kwenda kujiandikisha

2. watu wenye kazi nyingi kama watumishi, wakulima, wafugaji na wafanya biashara walishindwa kuacha kazi zao na kwenda kujisajili

3. Wale waliofanikiwa kujisajili mapema waliwasajilia ndugu na jamaa zao line zao wasioweza kwenda kule usajili unakopatikana. Hivyo, Asilimia kubwa wa wanavijiji walisajiliana line zao ili kuzinusuru zisifungiwe. Utakuta mwenye simu ni mwanaume lakini line ina jina la kike na kupoteza maana ya kitambulisho cha taifa.

Jamani wenzetu mliopewa madaraka mbalimbali msaidieni Rais kuwahudumia wananchi kikamilifu kwa njia ambazo zitawaondolea usumbufu.
 
Back
Top Bottom