Nichukue PCM au PCB, naomba ushauri wako

Are you good in Mathematics or Biology ?

Jibu lipo hapo hayo mengine ni ya ziada
 
Unataka kuajiriwa wapi? Pcm/pcb hazitoi ajira. Hizo ni njia 2. Hata ukisoma pcmb ukipata 0 haina maana. Muhimu kwa sasa ni kufaulu mtihani wako wa mwisho 2. How? Kwa kuchagua combination ambayo unaweza kuimudu ili mwisho ufaulu vizuri. Baada ya kufaulu sasa ndo uje JF kuomba advice ukasomee fani ipi ambayo itakuwa marketable kwa kipindi hicho.
Maoni yangu:
Pcm/pcb zote nzuri. Faida ya pcm ni
- ina wigo mpana wa fani kuliko pcb.
- Msuli wake unatembea.
Kwa pcb;
- Kama lengo lako ni kusoma medicine ukikosa 1 na 2 nzuri sahau udaktari.
- Msuli ni heavy weight kimtindo (msuli tembo matokeo sisimizi)
CONCLUSION:
Zote ni rahisi kama utakuwa comitted. Soma unayoweza kumudu.

ahsante..!
 
I'm good in both subject Biology and Maths.

Kama kweli zote zinapanda basi nakushauri ukachukue PCB kwani udaktari kwako itakuwa rahisi na pia serikali itakulipia ada tofauti na wale wa Engineering,

Kama unapenda sana kazi za kuajiriwa na kupata kipato kizuri bila jasho basi tafuta chuo ukasomee Ubunge
 
nadhan hapo umekosea!!!!! mbona watu wengi tu wapo engineering na wanapata 100% nikimaanisha wanalipiwa kila kitu na serikali??? au wewe unasemea engineering ipi,political engineering au?????
 
FUTA ILO WAZO LA KUAJIRIWA KWANZA!!!
Kuhusu ukasome nin angalia kitu unachokipenda na Malengo nacho!
PCM or PCB zote ziko pwoa!
 
we soma yeyote tuu maana bado ni ngazi ya chini saana katika elimu, kama unataka kusoma msc sawa ndo uombe ushauri we ni kama mtoto anayetaka kutembea hawezi uliza atembeeje ila akishajua kutembea anaweza kuuliza aende wapi, we bado saaaaaana kijana soma tuu yeyote afu huu ujinga wa kuuliza ajiri bado hata form ya shule hujapa unatoa wapi huu ujasiri
 
Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....
:rockon:
 
Listen to your heart and go for it!! Mimi nimesoma PCB na sasa ni daktari ila siku katazi kuja huku wala kwenda kule!! Just do what u think you want to do and give it your BEST mengine yatafuta!!
 
Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....

Zote nzuri ila PCB ni the best kwani inakupelekea kuchukua kozi za afya ambazo zinalipa sana, kuna upungufu mkubwa sana wa wataalam wa Afya nchini, kwa mfano wilaya nyingi sana hazina Madaktari (MD) ambao ni Graduates zinaendeshwa na Assistant Medical Officers(AMOs).

Ajira za upande wa Afya zinalipa zaidi, mfano Mshahara wa mtu mwenye diploma na Fani za afya mfano nesi tu analipwa mshahara karibu mara mbili ya mtu mwenye degree ya fani nyingine nyingi tu.

Tena kama unaweza achana na kwenda kidato cha tano, tafuta kozi ya Clinical Officer au Medical Assistant au hata Nursing soma diploma ukimaliza unaajira, fanya kazi miaka michache nenda kachukue degree yako bila shida ya kusumbuana na Loan Board
 
kijana kwanza hongera maana umekuja kutuambia kuwa wewe combination zote zimebalance! pili tambua hapa umetuletea ishu nyingine ya malumbano kati ya pcb na pcm nijuavyo mimi tukiwa shule watu wa combination hizi ni tabu sana kila mmoja anajiona ni babu kubwa zaidi ya mwenzake! kwa hiyo hapa utapata kizunguzungu!
sasa dogo wewe lazima uelewe pamoja na yoote unauwezo na masomo yapi suala la kuajiriwa kwanza liweke pembeni soma ufaulu basi utaingia kupambana na soko la ajira mbona ukifaulu utajiuza tu woga wa nini. tii kiu yako usiyumbe!
 
KOMBINESHENI YOYOTE NI
NZURI iwapo utaifanya vizuri. Full stop.
Haya mambo ya kusema kombinesheni fulani ina ajira zaidi mara nyingi sio
kweli sana. Halafu kumbuka mambo yanabadilika sana.. mpaka uje umalize
chuo kikuu miaka mi5 ijayo, una uhakika mambo yatakua kama yalivyo sasa?
We chagua kombi unayoiweza, nenda kakomae ufaulu uende chuo.

Si ndio hapo,mi nawaangalia tu wanavyommezesha matango pori dogolasi
 
kijana kwanza hongera
maana umekuja kutuambia kuwa wewe combination zote zimebalance! pili
tambua hapa umetuletea ishu nyingine ya malumbano kati ya pcb na pcm
nijuavyo mimi tukiwa shule watu wa combination hizi ni tabu sana kila
mmoja anajiona ni babu kubwa zaidi ya mwenzake! kwa hiyo hapa utapata
kizunguzungu!
sasa dogo wewe lazima uelewe pamoja na yoote unauwezo na masomo yapi
suala la kuajiriwa kwanza liweke pembeni soma ufaulu basi utaingia
kupambana na soko la ajira mbona ukifaulu utajiuza tu woga wa nini. tii
kiu yako usiyumbe!

ahsante
 
Zote nzuri ila PCB ni the best kwani inakupelekea kuchukua kozi za afya ambazo zinalipa sana, kuna upungufu mkubwa sana wa wataalam wa Afya nchini, kwa mfano wilaya nyingi sana hazina Madaktari (MD) ambao ni Graduates zinaendeshwa na Assistant Medical Officers(AMOs).

Ajira za upande wa Afya zinalipa zaidi, mfano Mshahara wa mtu mwenye diploma na Fani za afya mfano nesi tu analipwa mshahara karibu mara mbili ya mtu mwenye degree ya fani nyingine nyingi tu.

Tena kama unaweza achana na kwenda kidato cha tano, tafuta kozi ya Clinical Officer au Medical Assistant au hata Nursing soma diploma ukimaliza unaajira, fanya kazi miaka michache nenda kachukue degree yako bila shida ya kusumbuana na Loan Board

thanks..!
 
Naomba kutoa angalizo dogo hata baada ya kumaliza kusoma either PCM au PCB cha msingi katika maisha ni furaha na si fedha hivyo basi uchague fani unayoipenda na sio fani inayolipa
 
Kijana kwanza angalia nini plan yako kwanza ikimaanisha unataka kozi gani baadae ili usije kujiroga mwenyewe. Kisha angalia masomo gani unayamudu ili baadae usije kujutia kwanini uliacha somo fulani. Kisha utaamua mwenyewe nini ufanye baada ya kuangalia vigezo hivi.
 
hizo kombi ukitaka kufaulu upate shule kama kibaha,mzumbe,taboraboys,ilboru KWENGINE HUKO UTAAMBULIA MAUMIVU TUU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom