Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 686
- 1,360
Habari za muda huu wanajamii...
Natumaini humu kuna watu mbalimbali wenye uzoefu katika masuala ya biashara na pia kuna waajiriwa wa serikalini na sekta binafsi au vyote kwa pamoja(waajiriwa ila ni wafanya biashara pia).
Iko hivi, nilimaliza elimu ya juu miaka mitatu iliyopita katika kitivo cha elimu lakini nikiwa chuo niliweza kujishughulisha na vibiashara mbalimbali na nikabahatika kushika kibiashara kimoja nikaganda nacho nikitumia pesa za kujikimu(BOOM) kama mtaji.
Nilipomaliza masomo sikuhangaika kutafuta shule za kujishikiza kufundisha ila niliendeleza kibiashara changu ambacho hadi sasa nashukuru Mungu bili zote nalipa bila wasiwasi.
Sasa mkanganyiko unakuja kwamba kuna baadhi ya ndugu na jamaa wananipambania nipate ajira ya kudumu hivyo kunipa connection mbalimbali ila najikuta sizitilii maanani kwa kuwa nishazoea biashara na ninaona mwanga mzuri mbele kwenye biashara yangu.
Kwa wazoefu wa haya mambo naombeni ushauri nifanyeje ili baadae yasije nikuta majuto kwanini sikufata upandee huu huenda ningetoboa au kwanini niliacha hiki asaivi niko ivi, naombeni ushauri wenu.
Natanguliza shukran.