Kwa ufupi Mgaya CV kaisha pandisha, na yuko juu, na Mkulu hakujua kwamba kwa kumponda kwakutumia data feki kwa mrindimo wa mipasho ndo kaisha mpaisha jamaa, vijana wa leo wanasema hiyo ilikula kwa JK Yaani sasa hivi Mgaya yuko juu ile mbaya!
Mheshimiwa mmoja bungeni alitoa mifano mingi sana kuwa nchi haiwezi kutawalika ikiwa kuna kundi dogo linafaidika katika nchi huku kundi kubwa linataabika. Nimeshitishwa kusoma taarifa hii kuwa Kikwete ametamka kwenye hotuba yake kuwa kima cha chini hakiwezi kuongezwa kufikia 315,000 hata katika kipindi cha miaka 8 ijayo. Maana yake kwa wafanyakzi ni kutomchagua Kikwete na CCM yake kwa sababu Kikwete amethibitisha kuwa mpaka mwaka 2018 bado wafanyakazi wataendelea kula vumbi. Hapa kweli watanzania tuliuvaa mkenge. Hatuna rais, CCM wanajali matumbo yao tu. Kuanzi wabunge hadi mawaziri na rais hawawajali watanzania.Tamko la TUCTA juu ya hotuba ya Mh. Rais...
Wamejitahidi kucounter pamoja na kwamba kuna kawogawoga flani kwenye huu ufafanuzi,mfano kwa nini hawajanyambulisha hizo trilioni sita zilizokuwa zikisisitizwa na nkulu???????? anywayz ndiyo mambo ya dunia ya tatu!!!!!!!!!! All in all go TUCTA go!!!!!!!!!!!
MgaYa angetulia tu!..Maana zile nyaraka alizotoa Rais wa TUCTA mbona zilitosha kuthibitisha Uzushi na Ubabe na Udhushi wa Mwenye Kaya?... Kujibu tuhuma ni sawa na kuendelea kumdhalilisha Mwenyekaya na wambea wake waliomdanganya......
Kauli mbiu ni maisha bora kwa wabunge, mawaziri, rais, na mafisadi wengine.Aibu kubwa!
Ati huwezi lipa mshahara wa 315 000 hata kama ni miaka 8 ijayo? Ulidhani maisha bora kwa kila mtz yanaletwa kwa 80,000. Hii ni kauli ya kustaajabisha! Wakati wenzako wanasema YES WE CAAAAN!!! Wewe for Christ's sake unasema YES WE CAN'T. Hivi urais nini? Jambo dogo kama hilo linakushinda nini? Kuna wachumi wangapi Tanzania hii ambao ukiwaita wakafanya projection ya kile TUCTA wanataka ukaja na credible figures, Uka side na wafanyakazi wako ukaweka mkakati, ukaziba mianya, ukaongeza ufanisi mambo yaka unfold yenyewe!!!
Badala yake unakuja na kauli mfu kabisa! kabisa! In a simple plain language Mtanzania hana tumaini la kuyaona maisha bora labda mpaka baada ya miaka minane!
Mnafiki ni mtu anayesema halafu hatendi, Kauli mbiu ya mwaka huu yafaa uwaeleze watz unachomaanisha hasaaa! Maisha bora kwa kila Mtanzania 2019 tujue moja!!!