Nianzie wapi mafao NSSF?

Nianzie wapi mafao NSSF?

Nenda NSSF iliyokuwa inahudumia vikahakikiwe , kama viko timamu utasubiri miezi 3 kisha uanze kulipwa asilia 33 kila mwezi kwa miezi sita ...kisha utakaa miezi 18 ndio pesa yako ihamishiwe mfuko wa hiari ambako utaamua kuichukua ama kuiacha
NB. Cheti chako cha utumishi ndio kinaweza kukuokoa ama kukuangamiza kuchukua mafao yako ...kwakuwa kama kimeandikwa kazi yako haikuwa ya ujuzi utapata fungu lako lote hapohapo
Kwa kuongezea hapo ni kwamba navyo jua mimi ni kwamba ukiwa unachangia kwa hiari utaendelea kufanya hivyo ili kuendelea kuweka akiba yako iweze kuja kukusaidia hapo baadae
 
Kwa wewe huna sifa za kuandika hiyo barua, wewe utaenda na barua yako ya kuisha kwa mkataba pamoja na kitambulisho cha NSSF watakupa fomu za kufungua madai, kwa kuwa toka uondoke kazini bado miezi sita haijapita kwa hiyo utaratibu wa NSSF haukuruhusu kuandika barua ya kuomba kibali cha kufungua madai. Wai kufungua madai kabla ya miezi sita kupita.
Asante
 
Nenda NSSF iliyokuwa inahudumia vikahakikiwe , kama viko timamu utasubiri miezi 3 kisha uanze kulipwa asilia 33 kila mwezi kwa miezi sita ...kisha utakaa miezi 18 ndio pesa yako ihamishiwe mfuko wa hiari ambako utaamua kuichukua ama kuiacha
NB. Cheti chako cha utumishi ndio kinaweza kukuokoa ama kukuangamiza kuchukua mafao yako ...kwakuwa kama kimeandikwa kazi yako haikuwa ya ujuzi utapata fungu lako lote hapohapo
Mku cheti za utumishi unamaanisha certificate of service ambacho alinipa mwajiri sio au
 
Habari za mida hii Bandugu, twende kwa hoja moja kwa moja, mimi nilifanya kazi taasisi moja ya kiserikali sasa mkataba wangu wa kazi umeisha tokea mwaka 2019.

Sikuongeza tena mkataba na pia sikufatilia mafao yangu NSSF sababu nilisafiri mbali kumuuguza Mzee wangu now nimerudi wadau nianzie wapi msaada wenu.

Subiri ufikishe miaka 60 ndio udai mafao yako ya uzeeni.
 
Subiri miaka yako igote 55. Vinginevyo wahi NSSF ukadai fao la kukosa ajira upewe hela ya fegi kila mwezi baada ya miezi 6 tangu umefukuzwa
 
Subiri miaka yako igote 55. Vinginevyo wahi NSSF ukadai fao la kukosa ajira upewe hela ya fegi kila mwezi baada ya miezi 6 tangu umefukuzwa
Pesa inatoka ukiwa umefukuzwa pekee au hata kama mkataba umeisha??
 
Acheni kumpotosha jamaa Mimi mwenyewe ni muhanga wa hili suala mkataba wangu wa kazi uliisha 2016 lakini sikufatilia mafao yangu, Siku ya kufatilia ilibidi niandike barua ya kuomba kibali cha kufungua mafao. Barua yangu ilipooitishwa ndio nikafungua mafao na mpaka muda huu tunavyoongea tayari nimeshalipwa pesa yangu, Acheni kumpotosha jamaa.
kwani lile swala la mpaka baada ya miaka 60 ilishafutwa?? kumbe now fao la kujitoa limerejea au sijaelewa
 
Hao ndugu wanaboa sana kimsingi , na wamesahau kama na wao ni astaafu watarajiwa, nchi imeharibika hela za wastaafu zimeporwa na serikali kiufupi mifuko haina hela na ndiomaana wanawaletea mizengwe wazee wa watu, kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita na inayokuja watumishi wa umma na wastaafu watapata tabu sana, hali ni tete ni Mungu tu aingilie kati watu wana vielelezo vyote lakini wanazungushwa sana kuna mmoja mpaka anaulizwa vyeti kama alisoma na amestaafu miaka minne iliyopita sasa haya kama sio makusudi ili adhulumiwe ni nini? Nchi imeharibika kuna kitabaka kidogo sana cha watu ndio wanafaidi lakini waliobaki maumivu tu
 
Cheti cha utumishi sio lazima, hapo kiondoe.
Vinavyohitajiwa kwa ulazima:-
Barua ya mwisho wa mkataba
Kitambulisho cha NSSF.
Picha tatu za rangi.
Bank Statement.
Pamoja Nakala ya kitambulisho cha mpigakura/NIDA.
Hapo Kwenye NIDA, vipi kama una namba tu, id bado?
 
Nashukuru Sana waungwana nimepata picha sasa naanza mchakato nitaleta mrejesho kadri itakavyowezekana
 
kwani lile swala la mpaka baada ya miaka 60 ilishafutwa?? kumbe now fao la kujitoa limerejea au sijaelewa
Sasa hivi kuna FAO LA kutokuwa na ajira kwa wale ambao kazi zao ni za kitaaluma kama mhandisi, daktari, mhasibu n.k, Vilevile FAO LA kujitoa bado linaendelea kwa wale ambao kazi zao sio za kitaaluma, let say vibarua katika viwanda, miradi ya ujenzi na n.k
 
Back
Top Bottom