Nianzie wapi mafao NSSF?

Nianzie wapi mafao NSSF?

Nilichogundua, serikali kuweka mambo haya ya sijui fao la asilimia 33 na 50 then usubiri miaka 55 upewe nusu ya iliyobaki ni wizi. Wizi ambao ni wa waziwazi, mwaka 2008 niliacha kazi nikakaa miezi nikaenda kudai nikapewa hela zote. Sasa hii kuanza mara hivi mara vile ni kuiba haki ya wanyonge
 
Habar Mkuu Mimi nipo mfuko wa PSSSF na nilikua ajira za mikataba nimefanya kazi kweny ilo shirika kwa mwaka mmoja na nusu na kuachana nao

Nikapata ajira ya kudumu serikalini na wamenitaka nijiunge tena PSSSF vipi je ninaweza kupata fao langu au wanaweza kuni link michango yangu ya nyuma kweny Hilo shirika ikaingia kweny ajira hii mpya??
Hata pale mkataba unapoisha na hawana mpango wa kuendelea na wewe.
 
Mimi naomba kuuliza wakuu kwa vibarua wa viwandani ambao hawana mikataba ila huwa wanakatwa NSSF wanawezaje kupata hela zao?

Maana mwajiri hawezi kukuandikia barua ya kukuachisha kazi sababu huna mkata wowote na yeye.

Mwenye kujua naomba anielekeze.
 
Cheti cha utumishi sio lazima, hapo kiondoe.
Vinavyohitajiwa kwa ulazima:-
Barua ya mwisho wa mkataba
Kitambulisho cha NSSF.
Picha tatu za rangi.
Bank Statement.
Pamoja Nakala ya kitambulisho cha mpigakura/NIDA.
Na je kama mtu hajapata kitambulisho cha NSSF inakuwaje?
 
nimeenda leo jibu nililopewa nimekata tamaa kabisa.
Yaani mimi nilifanya kazi kwenye mkoa tofauti na ninapoishi sasa hivi.
Wakasema kwamba siruhusiwi kusubmit fomu zangu mpaka niandike barua kwa meneja halafu niondoke na fomu zangu nyumbani nikasubiri wiki 3 barua ijibiwe halafu baada ya hapo ndipo nitaruhusiwa kusubmit hizo fomu zangu.
Sasa kila nikiufikiria huu mlolongo naona hovyo tu na ukizingatia sitakuwa na muda kuanzia wiki ijayo nitaenda maporini kutafuta,hata sijui itakuwaje maana nikiondoka sasa hivi kurudi ni mwakani
Hiyo haina shida nenda tu kwenye ofisi zao ukawaelezee wapo wengi wamelipwa na hawakuwa na ID isipokuwa walikuwa na namba.
 
nimeenda leo jibu nililopewa nimekata tamaa kabisa.
Yaani mimi nilifanya kazi kwenye mkoa tofauti na ninapoishi sasa hivi.
Wakasema kwamba siruhusiwi kusubmit fomu zangu mpaka niandike barua kwa meneja halafu niondoke na fomu zangu nyumbani nikasubiri wiki 3 barua ijibiwe halafu baada ya hapo ndipo nitaruhusiwa kusubmit hizo fomu zangu.
Sasa kila nikiufikiria huu mlolongo naona hovyo tu na ukizingatia sitakuwa na muda kuanzia wiki ijayo nitaenda maporini kutafuta,hata sijui itakuwaje maana nikiondoka sasa hivi kurudi ni mwakani

Mkuu labda nikufungue kitu hii pesa ya Nssf unatakiwa usiwe na haraka nayo kwani haitoki kirahisi rahisi,wewe fanya walivyokuambia achana nayo ukipata muda unakuja kuchungulia imefika wapi,kwa sababu unaweza pata dharura ya kuja town kutoka porini huko. Huwa haihitaji haraka kabisa
 
Yes kuna brother wangu amenipa mawazo kama yako.
Maana nilikuwa nawaza au nisafiri fasta nirudi kwenye ule mkoa nilikofanyia kazi niwaachie makaratasi then nigeuke ili niwe huru.
Yule brother akaniambia niachane nayo kwa sababu inahitaji ufuatiliaji sana na ni ngumu sana kufanya ufuatiliaji kwenye mkoa tofauti na unaoishi kwa sababu inahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara kuwakumbusha huwa hawaingizi wenyewe bila kusumbuliwa.
Na akaniambia nisiwe na wasiwasi hela haiwezi kupotea hata nikirudi baada ya miaka 2 nitaikuta tu.
 
Back
Top Bottom