Nianze kwenda kwa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nianze kwenda kwa nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, Aug 30, 2011.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nianze kwenda kwa nani?
  1. Leo nimepata simu, Huko kwangu ofisini, Zote tena taslimu, Zimefika mikononi,
   Na zote hizo muhimu, Nimezisoma yakini,
   Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  2. Simu ya kwanza yasema, Tia mguu njiani,
  Mama yako ana homa, Imemuanza kondeni,
  Fanya uje hima hima, Kupona si tumaini
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.


  3. Simu ya pili yasema, Hamza njoo Omani,
  Mkweo anakoroma, Kakumbwa na datsani,
  Ukweli hana uzima, Ajekupa buriani,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  4. Simu ya tatu yasema, Barubaru harahara,
  Mkeo wa huko Doha, leo kaumwa na nyoka,
  Waganga wanavyosema, Imebakia dakika,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  5.Simu ya nne yasema, usidharau kufika,
  Mwanao Dar isalaama, Mguu umevunjika,
  Homa raha alalama, Jinsi anavyoteseka,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  6. Simu ya tano yasema, kaka yako ana kesi,
  Kaiba mali ya umma, Wamemzoa polisi,
  Majibu ya mahakama, Uje ulipe upesi,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  7Watunzi huo ukweli, msidhani naropoka,
  Zimeniruka akili, Nabaki kuweweseka,
  Mwanakijiji na Ali, Choveki nipe hakika,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.  Dr Hamza Yousuf Al Naamany (Barubaru)
  H/N 2436, Umm hays Block.
  Minal fahal Street.
  Doha.
  Qatar
   
 2. talentboy

  talentboy JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,625
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  nenda unakoona kuzito sana,natumai moyo wako unakuvuta zaid sehemu fulani kt ya hz ulizozitaja.Wassalam!
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  zote zina ni touch sana ndio maana nikaomba ushauri wenu.
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  wachunie wote jifanye na wewe unaumwa...hongera kwa utunzi, nasubiria mwezi hapa kibarazani
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Barubaru .... naona umeshiba chui la ilboru .... mzulu hajambo?
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Barubaru umefuturu weye? naona kama futari inafanya kazi tumboni....anyway sikujua kama wewe ni mtunzi mzuri wa mashahiri
  basi nivizuri ukaja huku Igunga ili uwasaidie ndugu zako wa cuf na ccm kwa kuimba mashahiri haya majukwaani ili kuvutia watu
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  nenda kwa mama.......hakuna anayeweza kuziba pengo la mama......hakuna spare ya mama......
  nakuja kwako eid.....niandalie biriani
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mpwa hii kali lakini barobaro yeye ameuona jana sisi huku tulikuwa tunasubiri wa bakwata!
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kaa mkao wa kula. Nimetunga kitabu cha mashairi kinachoitwa MTU SI KITU ambacho kwa sasa kinachapishwa huko Port of Spain, Trinidad na insh'Allah mwezi Oct kitakuwa tayari kwa kuuzwa huko Tanzania. na fund zote zitapelekwa kusaidia TAKIRUKI (taasisi ya kiswahili na lugha za kigeni- Zanzibar.)

  Kikiwa tayari nitawajuza ili mchangie taasisi hiyo.

  Babu wa mama yangu alikuwa mfanya biashara maarufu sana na aliishi SIKONGE na wengine wapo Urambo. Hivyo mara nyingi nikija Tz napenda kutembelea huko kusalimia.

  Kila la kheir Igunga.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha mbaali sana. We Muulize Mchunganji Natse (Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu) atakwambia vitu vyangu pale Ilboru. wakti nikiwa High school.

  Mzuru najua yupo Arusha Sec kama mkuu wa shule. Vipi Mwl Juma, Mzava Kapombe, Mama Capt Mushi, Mapambano na mpishi wangu mzee Lukumay
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Akh'lan wa sah'lan.
   
 12. b

  binti ashura Senior Member

  #12
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu Fungu la nne ni lakipekee sana, Adam Hakuwa na kaka wala Mama wa aina yeyote ile lakini alikuwa na mke tu kabla ya kuwa na watoto lakini aliishi. mkeo ni sehemu ya mwili wako lazima apewe kipaumbele kuliko wote. Nenda kwa mkeo!.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ahsantum kwa ushauri.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,054
  Likes Received: 6,495
  Trophy Points: 280
   
 15. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  &lt;br /&gt;<br />
  &lt;br /&gt;<br />
  Nenda kwa mama kwani hakuna kama mama.Mkwe ni mama wa kukopa! At anytime mnaweza kuwa watu mnaofahamiana tu baada ya kuachana na mwanae.Mama mzazi ana radhi zako hata mbele za Mungu,pia kumbuka pepe inapatikana kwa wazazi hivyo haraka nenda kwa mama.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu kwa ushauri
   
Loading...