Nianze kwenda kwa nani? (Shairi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nianze kwenda kwa nani? (Shairi)

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Barubaru, Sep 7, 2011.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nianze kwenda kwa nani?
  1. Leo nimepata simu, Huko kwangu ofisini, Zote tena taslimu, Zimefika mikononi,
   Na zote hizo muhimu, Nimezisoma yakini,
   Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  2. Simu ya kwanza yasema, Tia mguu njiani,
  Mama yako ana homa, Imemuanza kondeni,
  Fanya uje hima hima, Kupona si tumaini
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.


  3. Simu ya pili yasema, Hamza njoo Omani,
  Mkweo anakoroma, Kakumbwa na datsani,
  Ukweli hana uzima, Ajekupa buriani,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  4. Simu ya tatu yasema, Barubaru harahara,
  Mkeo wa huko Doha, leo kaumwa na nyoka,
  Waganga wanavyosema, Imebakia dakika,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  5.Simu ya nne yasema, usidharau kufika,
  Mwanao Dar isalaama, Mguu umevunjika,
  Homa raha alalama, Jinsi anavyoteseka,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  6. Simu ya tano yasema, kaka yako ana kesi,
  Kaiba mali ya umma, Wamemzoa polisi,
  Majibu ya mahakama, Uje ulipe upesi,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.

  7Watunzi huo ukweli, msidhani naropoka,
  Zimeniruka akili, Nabaki kuweweseka,
  Mwanakijiji na Ali, Choveki nipe hakika,
  Nianze kwenda kwa nani, washairi nambieni.  Dr Hamza Yousuf Al Naamany (Barubaru)
  H/N 2436, Umm hays Block.
  Minal fahal Street.
  Doha.
  Qatar
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu kwako ni makini, wengine watajifia,
  Hima hospitalini, waganga kumtibia,

  Utakwepa kisirani, laana kujipatia,
  Muwahishe mama yako, wengine hao maiti!
   
 3. C

  Choveki JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pokea pole wakwetu, kwa mama huko anzia,
  Tena sisubiri mtu, kwa mama watimkia
  Si namba mbili wala tatu, ya kwanza ashikilia
  Hakuna sawa na mama, sikia baba sikia

  Wala sisubiri simu, nyengine ije ingia
  Umeshapata salamu, mama wasikilizia
  Wajibu kwako muhuimu, safari ukianzia
  Hakuna sawa na mama, sikia kaka sikia

  Wengine watasubiri, kichwani hilo julia
  Tulia uwe mahiri, ni mama wakimbilia
  Kwa mama kweli nakiri, ni nani akaribia?
  Hakuna sawa na mama, sikia ndugu sikia

  Na tena una bahati, mamako anapumua
  Chomoka kama baruti, usije kuja jutia
  Kwa wako wote wa dhati, ni mama anaanzia
  Hakuna sawa na mama, sikia shekhe sikia

  Tano nasema kikomo, ni miye nakomelea
  Nimeshakupa kisomo, kwa mama kuashiria
  Natena hana kipimo, muhimu hiyo kujua
  Hakuna sawa na mama, we Barubaru sikia!
   
 4. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180

  Panapo tumika shoka,usije leta jambia,
  Sifananishe na soka,na maisha ya dunia,
  Mama yako shamchoka,hivi ndo watuambia?
  Wakuanzia ni mama,wengine wafuatia

  Tena fanya hima,usije ukajutia,
  Hakuwekewa kwa bima,maisha yatalipia,
  Ufanya kwake khidima,mola tampa afua,
  Wakuanzia ni mama,wengine wafuatia

  Kakiyo ana dhahama,kwakweli kajitakia,
  Hicho kwake ni kiama,apate pa kujutia,
  Umwache akale sima,kamwe sije kimbilia,
  Wakuanzia ni mama,wengine wafuatia

  Mkweo toka omani,mola pekee ajua,
  Omba dua kwa imani,apate japo afua
  Mke ombea jirani,wapate kumwangalia,
  Wakuanzia ni mama,wengine wafuatia

  Mtoto yupo salama,hofu ndio yasumbua,
  Nenda mwangalie mama,yeye wakupigania,
  Kamwe acha kulalama,nakupa japo usia,
  Wakuanzia ni mama,wengine wafuatia
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Nitarudi...
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana kwa ushauri.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa ushauri wako.
  Nimelipenda sana shairi lako.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakika upo juu, Nimekukubali.

  Ahsante kwa ushauri.
   
 9. A

  Albimany JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Malala miko tumesikia,nashangaa unachelewa.
  Majibu umeshapewa,mama ndio wakuanzia.
  Mataizo utapata,mama radhi akikuachia.
  Wima fanya haraka.dunia iisijekuelemea.

  Waomani anamata,mkwe mpehishima pia.
  Wapigie ndugu,wamaskati kukusaidia.
  wampeleke mkwe,hospitali asijejifia.
  Wima fanya haraka,maisha kuyaokoa.

  Doha usidharau,mke atajapotea.
  Dada atajachukia,pilau hutapikiwa.
  Doctari agizia,nyumbani kusaidia.
  Wima fanya haraka,sumu yawezauwa.

  Angalia Dar,kunawatu wawajua.
  Albimany nikonawe,nitakusaidia
  Angalu Muhimbili,mtoto kukufikishia,
  Wima kwamama,huyu Moi watampasua.

  Hamza,sikia.nduguyo kajitakia
  Hahitaji kusaidiwa,kuiba nivibaya.
  Huyo hakulelewa,dunia kaivamia.
  Wima kimbia,matatizo yakujitakia.

  Majibu umepewa,mama wakuanzia.
  Mkwe akifuatia,baada ya mama nakwambia.
  Mke si wakudharauliwa,hachelewi kukukimbia.
  Mtoto akiumia,muhimu kutibiwa.
  Mwisho kakaako,hujuma katifanyia hapaswi kusaidiwa.

  BY
  Albimany.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Nimefanya hima miye, nije na nikuambie
  Barubaru usikiye, haraka ukafanyie
  Shauri nikupatie, nawe ulizingatie,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia

  Kwanza nakusalimia, na pole nakupatia
  Yote yalokufikia, mazito nakubalia
  Masahibu ya dunia, bila hodi yatujia
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  Swali ulilouliza, moyoni limeniumiza,
  Na tena likaniliza, huzuni likinijaza,
  Nikakaa nikawaza, sasa jibu nakujuza,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  Mama kashikwa na homa, mauti ayatazama,
  Hofu yake kama mama, wanae wako wazima?
  Mmoja jela katama, habari mbaya kwa mama
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia!

  Ukishamtoa kaka, kwa mama fanya haraka,
  Wa kaka mkono shika, mwende mpate baraka,
  Kwa mama mkishafika, uzima hautatoka,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia

  Kisha umtume kaka, awahi kwenda Tandika,
  Kwa mwana wako hakika, mguu alovunjika,
  Huko akishakufika, hali itatulizika,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia!

  Nawe ufanye haraka, kwenda Doha kwa hakika,
  Mauti yasije fika, habiba akakutoka,
  Msiba ukakufika, wa nyonda akiondoka,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia!

  Na piga simu Omani, kwa wakwe walo tabuni,
  Binti yao taabani, mautiuti kitandani,
  Utachelewa njiani, wauguliwa mtani,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  Uwaambia Omani, dua zapaa mbinguni,
  Kwa Subhana Maanani, mwingi wa rehemani,
  Wawatakia imani, ukiomba ahueni,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  Mke akinusurika, Barubaru kwa hakika,
  Nenda Omani haraka, uende bila kuchoka,
  Mkweo asije toka, bila ya wewe kufika,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  Kama wote watatoka, ukenda kumtoa kaka,
  Msiba utawafika, pamoja mtawazika,
  Mke wewe utazika, mama kaka atazika,
  Kamtoe kwanza kaka, ya Mungu yatafuatia.

  M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 11. C

  Choveki JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Nahisi huyo ni gamba, kwa nini akimbiliwe?
  Ni gwanda kama si gamba, walio wengi viwewe

  Mwache apate kingwamba, atupwe selo alewe!

  Awe gamba au gwanda, najuwa wote viwewe!


  Kakako si kimbilio, hata aliwe na mwewe

  Hata atoe kilio, kelele navyo viwewe

  Asisubiri ujio, ajue yupo mwenyewe

  Awe gamba au gwanda, nahisi wote viwewe!


  Asake wapambe wake, aende hata msewe

  Kama
  kaoa na mke, asake hata mkwewe
  Walipokula vya kwake, malipo sasa wajuwe

  Awe gamba au gwanda, najuwa wote viwewe!


  Wote hao lao moja, wanagawana wenyewe

  Gwanda na gamba wamoja, nishaelewa mweyewe

  Watuonesha viroja, Dodoma ndiko kwenyewe!

  Awe gamba au gwanda, najuwa wote viwewe!


  Zangu hizi ndiyo mwisho, naomba unielewe

  Nasema yeye wamwisho, foleni aielewe

  Avilapo bila jasho, ajuwe vina mwishowe!

  Awe gamba au gwanda, najuwa wote viwewe!
   
 12. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ikiwa hujui beti kaa mie soma tu usidanganye.
   
 13. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  hahaha choveki hakika umenena!
   
 14. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Barubaru we sikiya,wenzangu lotangulia.
  Mwakijiji kapoteya,Segerea kapitia.
  Kwa mamako harakiya,na gari kumchukua.
  Mama wa kwanza sikia.Nduguyo mi nakwambiya
  .

  Kwenu Manundu wajuwa,tibaye pata poteya
  Mama wa maji kutiwa, mwiliwe umenyongeya
  Akifa mama ukiwa, habari kikufikiya
  Mama wa kwanza sikia.Nduguyo mi nakwambiya
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,478
  Trophy Points: 280
  Kama hayo yatokea, Hapa kwetu duniani,
  Mara moja kwa sawia, Mbona hicho kisirani?
  Haraka bila kawia, Tazama juu mbinguni,
  Kwa kwanza kukimbilia, Kwa Mungu kuwaombea.

  Wanaosema kwa mama, wajuaje utafika?
  Waweza katwa mtama, Ukashindwa na kufika,
  Mungu muweza daima, Ombi lako likifika,
  Kwa kwanza kukimbilia, Kwa Mungu kuwaombea.

  Watu wako taabani, Wewe utafanya nini?
  Yamefikia pomoni, We una jeuri gani?
  Ukawatoe wodini, weshakuwa mautini?
  Kwa kwanza kukimbilia, Kwa Mungu kuwaombea.

  Pole ninakupatia, kwa yote yalokupata,
  Imani kishikilia, Afueni watapata,
  Mungu kimtegemea, Yote hayo yatapita
  Kwa kwanza kukimbilia, Kwa Mola kuwaombea.

  Na Big Braza Asprin -ODM
  Kaunta ya Juu.
  MMU.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  1.Yakhilahi ya wadudi, Nizishusha kwa karima,
  Nizidishie imani, pamoja na usalama,
  Asprini karudi, Dua zote nishasoma.
  Nawashukuru kwa dhati,Mola atawajalia.

  2 .Hakika nimeshukuru, Mawazo kunipatia,
  Nimeridhia hakika, Majibu kunirushia,
  Wengi wamenihakika, Mama kumkimbilia,
  Nawashukuru kwa dhati,Mola atawajalia

  3 .Mwanakijiji hakika, Kweli nimekusikia,
  Damu nzito ya kaka,Jela kaikaribia,
  Nimemtuma haraka,Ndugu deni kulipia.
  Nawashukuru kwa dhati,Mola atawajalia.

  4. Ammi nimekuridhia, Choveki nimesikia,
  Pakajimi katulia, Jidu amesha kimbia,
  Abimani kaishia, majibu kunipatia,
  Nawashukuru kwa dhati,Mola atawajalia.  Barubaru
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  TITI LA MAMA


  Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
  Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
  Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
  Toka kama mlizamu, funika palipozibwa,
  Titile mama litamu ,Jingine halishi hamu.

  Lugha yangu ya utoto,hata sasa nimekua,
  Tangu ulimi mzito,sasa kusema najua,
  Ni sawa na manukato,moyoni mwangu na pua,
  Pori bahari na mto,napita nikitumia,
  Titile mama litamu,jingine halishi hamu.


  By Shaban Rorbert
  from Jahadhmi's anthology of Swahili poetry
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,859
  Trophy Points: 280
  aisee thread nzuri
   
 19. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mi ndo naiona hii. Inapendeza na ni tamu.
   
Loading...