Niache kula kuku Sea Cliff kisa kupeleka watoto English Medium?

heeeh mkuu??

eti mtu ana uwezo wake akampeleka mwanawe shule ya kata na kufuatilia maendeleo yake huku mtoto anaenda shuleni kashiba hana stress,hana mawazo kwamba nikirudi chakula kipo au hakipo,anaenda shuleni na nguo safi na anaenda ama kwa daladala au kabaskeli kake hana tabu.

kwa hivyo hii ni kumnyima mtoto mpaka umpeleke shule za mamilioni eti ndo hujamnyima.

bosi samahani nikuulize hivi kweli ulifikilia unachokiandika kweli??

dah aisee hatari sana

Bro nenda mwenyewe hizo shule za kata uone hali halisi ndo utanielewa..shauri lako. Mimi mlinzi wangu ana mshahara wa kawaida anafanya overtime na kazi za ziada anamsomesha mtoto english medium. Mimi mama yangu alikua single mother na mpishi tu yani tuseme mama ntilie na alinisomesha english medium mpaka scholarship alinitafutia ..sasa wewe una pesa zako unaweka ubahili katika elimu aibu yako mkuuu. aibu sana.. umekaa baa unalewa mtoto unampeleka shule ya kufikirika.. we utakkuwa tu choka mbayaa. hata hio hela hauna sema tu ukweli.huwezi ukawa na uwezo wako unaona ubahili million mbili kwa mwaka na umekaa cape town fish market.nyie ndo wale mnaenda pale mnakunywa maji bro...
 
No way!

Nishasema, kila mmoja atabeba msalaba wake. Mtoto atayeshindwa masomo atapelekwa VETA angalau akajifunze kuosha magari. Atayefaulu atakwenda shule ya kata na kingereza atajifunzia kwenye Isidingo.

Siwezi kuishi kwa shida na kwenda kuteketeza rasilimali pesa kisa mtoto akafundishwe kingereza. Pesa zangu ni za kutumbua mimi na mke wangu. Wengine ni by the way. Nishawaambia watoto wangu. Hapa ni kama wamepanda daladala ambayo konda asipoweza kukimbilia na kudandia, anaachwa kituoni.

Wenye pesa za kuchezea endeleeni kuziteketeza. Mimi nimesoma shule za kata, ila nikikaa na Maxence Melo tukaongea kiingereza, utadhani tumeshuka kutoka Marekani.

Ninaandika hivi nikisikitika, baada ya kumuona ndugu yangu mwenye maisha ya kuunga unga akiteketeza pesa yake English media. Milioni mbili kwa mwaka ni pesa ya matofali ya block elfu mbili, kwa watoto watatu ni matofali elfu sita. Mpaka wamalize darasa la saba ni matofali elfu 42! (Hiyo shule ya msingi bado hujazungumzia sekondari). Hiyo pesa si bora ujenge majumba wakae?

Kupeleka mtoto kufundishwa kiingereza English media kwa pesa ya kuungaunga ni sawa na kumlipia mtu fedha aishi hotelini ihali wewe unalala kwenye nyumba ya nyasi.

Narudia tena wewe ni mzazi wa kusikitisha sana. sijawahi kuamini kuna wazazi kabisa wana fikra hizi. Mimi sikulelewa na baba na ninasikitika kuna mtu kabisa baba wa familia ana mawazo kama haya. Naomba Mungu usipate mtoto maana hamnA mtoto anadeserve kupewa mzazi kama wewe. WEWE NI AIBU KWETU WANAUME KUWEKA UBAHILI KWA PESA ZAKO KWA DAMU YAKO MWENYEWE. Samtimes nashkuru hata sikuwa na baba kama wababa wenyewe ndo kama nyie. AIBU SANA MKUUU. HUFAI chama cha wanaume eti hela ya kutumbia we na mkewe...basi usizae. FUNGA KIIZAZI KAMA HAUKO TAYARI KUGHARAMIA MALEZI YA MWANAO
 
Unaweza ukawa dhahiri Huna mtoto, Huwezi ukawa una mtoto ana soma kwa shida wewe unakula bata. Napata Shida kidogo
 
No way!

Nishasema, kila mmoja atabeba msalaba wake. Mtoto atayeshindwa masomo atapelekwa VETA angalau akajifunze kuosha magari. Atayefaulu atakwenda shule ya kata na kingereza atajifunzia kwenye Isidingo.

Siwezi kuishi kwa shida na kwenda kuteketeza rasilimali pesa kisa mtoto akafundishwe kingereza. Pesa zangu ni za kutumbua mimi na mke wangu. Wengine ni by the way. Nishawaambia watoto wangu. Hapa ni kama wamepanda daladala ambayo konda asipoweza kukimbilia na kudandia, anaachwa kituoni.

Wenye pesa za kuchezea endeleeni kuziteketeza. Mimi nimesoma shule za kata, ila nikikaa na Maxence Melo tukaongea kiingereza, utadhani tumeshuka kutoka Marekani.

Ninaandika hivi nikisikitika, baada ya kumuona ndugu yangu mwenye maisha ya kuunga unga akiteketeza pesa yake English media. Milioni mbili kwa mwaka ni pesa ya matofali ya block elfu mbili, kwa watoto watatu ni matofali elfu sita. Mpaka wamalize darasa la saba ni matofali elfu 42! (Hiyo shule ya msingi bado hujazungumzia sekondari). Hiyo pesa si bora ujenge majumba wakae?

Kupeleka mtoto kufundishwa kiingereza English media kwa pesa ya kuungaunga ni sawa na kumlipia mtu fedha aishi hotelini ihali wewe unalala kwenye nyumba ya nyasi.
Hivi VETA ni Mahali pa Kujifunza Kuosha Magari? Gari lako huwa anakuoshea nani? Hapa kuna jamaa wanahangika kumsema kwenye mitandao kisa mtoto wake anasoma shule za kata. Uliwahi kusikia shule inaongeza IQ? Kama IQ ya mtoto ni kubwa hata shule za kata anasoma tu...na anafaulu kama watoto wengine.
 
No way!

Nishasema, kila mmoja atabeba msalaba wake. Mtoto atayeshindwa masomo atapelekwa VETA angalau akajifunze kuosha magari. Atayefaulu atakwenda shule ya kata na kingereza atajifunzia kwenye Isidingo.

Siwezi kuishi kwa shida na kwenda kuteketeza rasilimali pesa kisa mtoto akafundishwe kingereza. Pesa zangu ni za kutumbua mimi na mke wangu. Wengine ni by the way. Nishawaambia watoto wangu. Hapa ni kama wamepanda daladala ambayo konda asipoweza kukimbilia na kudandia, anaachwa kituoni.

Wenye pesa za kuchezea endeleeni kuziteketeza. Mimi nimesoma shule za kata, ila nikikaa na Maxence Melo tukaongea kiingereza, utadhani tumeshuka kutoka Marekani.

Ninaandika hivi nikisikitika, baada ya kumuona ndugu yangu mwenye maisha ya kuunga unga akiteketeza pesa yake English media. Milioni mbili kwa mwaka ni pesa ya matofali ya block elfu mbili, kwa watoto watatu ni matofali elfu sita. Mpaka wamalize darasa la saba ni matofali elfu 42! (Hiyo shule ya msingi bado hujazungumzia sekondari). Hiyo pesa si bora ujenge majumba wakae?

Kupeleka mtoto kufundishwa kiingereza English media kwa pesa ya kuungaunga ni sawa na kumlipia mtu fedha aishi hotelini ihali wewe unalala kwenye nyumba ya nyasi.
Ukizingatia viongozi wetu ni wavivu, wakiona hiyo English Medium hawajui kama ni ya KUUNGAUNGA akiwa na viakili na kusonga mbele hapewi mkopo . wale wanaopiga hesabu zako za tofali watoto wao watapata mikopo huku wakimiliki majumba.
 
ila hajafikiria in future yeye anaona kula kwenye mighahawa ya kifahari ndiyo dili, wakati dili ni kuwapa wanawe wabuni madini mbeleni watatusua kilife...
Sina nia ya kupingana na wewe mkuu lakini binafsi naamini kwa huu mfumo wa elimu yetu, elimu ya msingi ndo kila kitu. Mimi nilisoma shule zote za serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu, kwa bahati nzuri shule ya msingi niliyoisoma walimu walikuwa wamajitoa kweli darasani, Mwl wa Sayansi alikuwa wa Sayansi kweli na Mwl wa Kingereza alikuwa wa Kingereza kweli, nilikuwa na akili za kawaida darasani kuna wakati nilikuwa naingia kumi bora na wakati mwingine nilikuwa nakosa, nakumbuka mpaka namaliza shule ya msingi nilikuwa najua mikoa yote na wilaya zake najua miji mikuu yote ya nchi zote, najua historia ya nchi yetu na waasisi na viongozi wengine, kifupi tulipewa elimu ambayo sijajua kama huko kwenye shule za English medium huwa inatolewa, nakumbuka hata nilipofika chuo kikuu watu walikuwa wanashangaa inatokeaje najua mambo mengi ya kisiasa ilihali ninasoma uhandisi, kumbe ni misingi tu niliyoipata katika shule ya msingi, ila udhaifu mmoja niliogundua ulikosekana pale ni malezi, kwa kweli walimu walikuwa wanaamini kila kosa adhabu yake ni fimbo, hakuna cha kujitetea wala nini, madhara ya mtizamo huu ni kwamba unamfanya mtu asijiamini na pia unaua vipaji vya uwakili, wakati mwingine unatakiwa umuache mtoto ajitetee hata kama utamuona ana kosa unamuacha na hii itamjengea ujasiri wa kujitete na kujenga hoja. Nilifaulu kwenda shule ya kata, hapo ndo elimu ya msingi ilienda kunisaidia, yaani kila kitu nilikuwa naona ni marudio isipokuwa lugha tu ndo imebadilika, ila lugha haikuwa kikwazo sana kwa sababu ya ubora na juhudi za Mwl wangu wa kingereza wa shule msingi, alijitoa sana kutusaidia wanafunzi wake,yaani sekondari ilikuwa rahisi sana kwangu kutokana msingi nilikua nao, nilibahatika kwenda kidato cha tano katika shule ya serikali pia, huku hakukuwa na walimu kabisa ila ni wewe mwenyewe tu kujisomea na namshukuru Mungu nilibahatika pia kufaulu kwenda chuo kikuu cha serikali tena kile ambacho ni ndoto ya Watanzania wengi kujiunga nacho. Binafsi nikiangalia nyuma kwenye maisha yangu naona elimu yangu niliipata shule ya msingi na chuo kikuu, elimu ya kidato cha kwanza mpaka cha nne haina maana zaidi ya kukuvusha tu kwenda kidato cha tano, na elimu ya kidato cha tano na sita haina faida zaidi tu ya kukupeleka chuo kikuu. Kwa hyo kama tungepata walimu wenye wito na wanaopenda kazi zao wala hatuna haja ya kupeleka watoto English medium, Serikali ingeweza sana kuwatua watu mzigo mkubwa wa gharama wanazoingia kwa kutafuta ubora wa elimu, Naamini kabisa kama katiba yetu itawalazimisha viongozi wetu wa kisiasa kusomesha wanao katika shule za kata na kuwatibu ndugu zao katika hospitali za umma kama sifa ya mtu kugombea nafasi fulani basi elimu yetu ingeboreka na hata huduma za afya pia..Lugha kujifunza ni jambo dogo sana tena kwa gharama ndogo, kwa hyo kama unataka kumpatia mwanao msingi bora basi hakikisha anapata elimu bora ya msingi.
Usisahau pia kumtengenezea mazingira ya kujua lugha ya kiingereza kwani ndo lugha ambayo maarifa nyingi zimejificha ndani yake, tafiti nyingi zimechapishwa kupitia lugha hiyo.
 
No way!

Nishasema, kila mmoja atabeba msalaba wake. Mtoto atayeshindwa masomo atapelekwa VETA angalau akajifunze kuosha magari. Atayefaulu atakwenda shule ya kata na kingereza atajifunzia kwenye Isidingo.

Siwezi kuishi kwa shida na kwenda kuteketeza rasilimali pesa kisa mtoto akafundishwe kingereza. Pesa zangu ni za kutumbua mimi na mke wangu. Wengine ni by the way. Nishawaambia watoto wangu. Hapa ni kama wamepanda daladala ambayo konda asipoweza kukimbilia na kudandia, anaachwa kituoni.

Wenye pesa za kuchezea endeleeni kuziteketeza. Mimi nimesoma shule za kata, ila nikikaa na Maxence Melo tukaongea kiingereza, utadhani tumeshuka kutoka Marekani.

Ninaandika hivi nikisikitika, baada ya kumuona ndugu yangu mwenye maisha ya kuunga unga akiteketeza pesa yake English media. Milioni mbili kwa mwaka ni pesa ya matofali ya block elfu mbili, kwa watoto watatu ni matofali elfu sita. Mpaka wamalize darasa la saba ni matofali elfu 42! (Hiyo shule ya msingi bado hujazungumzia sekondari). Hiyo pesa si bora ujenge majumba wakae?

Kupeleka mtoto kufundishwa kiingereza English media kwa pesa ya kuungaunga ni sawa na kumlipia mtu fedha aishi hotelini ihali wewe unalala kwenye nyumba ya nyasi.
Kaka umenitua mzigo mkubwa sana uliokuwa umenielemea kwa mda mrefu nikikosa hata mtu wa kumsimulia nikiogopa kuchekwa na co workers na marafiki. kwa maelezo haya leo nyumbani kwangu lazima kitanuka. Wife analazimisha watoto wasihamishwe shule ili hali mzigo naubeba mimi. Leo nafanya maamuzi magumu kama mzee Wenger.
 
Watu wanashindwa kuelewa, shule za kata sio mbaya ila walimu wake wamechoka kila siku wanahangaika na madeni, sijui kupanda vyeo, mikopo imewajaa, mara wahangaike na uhamisho, wengi hawana nyumba nzuri za kuishi, vyumba vya madarasa vina mazingira ovyo kabisa yaani wanamambo mengi ya kuwakatisha tamaa ujuzi wao wa kufundisha unamezwa na mazingira hayo. Tena afadhali siku hizi Magufuli kasaidia kuondoa vyeti feki, maana wengi ambao walishindwa form 4 na maisha kuwagonga walikuwa wanakimbilia kutengeneza vyeti wakasome uwalimu waajiriwe. Hata hao walimu wa shule za kata mambo yao yakinyooka kidogo wanawapeleka watoto wao shule hizo unazoziita za kiingereza.
 
Jamaa una master alafu milioni mbili ni headache, Master yako haijakusaidia broo
Acha kudanganya hata prof muda huu 2m ni ishu inategemea idadi ya watu unaowasomesha mfano wanao 3 wadogozako 2 watoto wa dada zako 3 jumla 8×2m hapo hata prof lazima afanye maamuzi magumu. huwezi kusema nawaabot wasiendelee na masomo nibaki na wakwangu wakati ulishadecrare kiwasomesha sio sawa lazma utafute soft mechanism ya kuhandle situation. Hivyo usidhani 2m anayosema means ile unayoijua wewe na hawezi kufafanua kila kitu mengine siri yake.
 
Mm baada ya kuona mitoto yangu nalipa ada kubwa na haijui chochote ....nikaifukuza na kuipeleka shule za kata.....
Wapambane huko ....
Hongera na pole maana yawezekana hela ipo ila wasomaji ndio hawakuwepo.
 
Kwani Hiden bado anafundisha mchikichini. Mwendo ni ule ule. Shule atasoma za kata ila chobingo zote za tuition namlipia.
 
Diamond hakusoma hadi chuo kikuu ila anatamani wanawe wasome hadi chuo kikuu tena PhD wachukue.

Cristiano Ronaldo akiwa na miaka 14 aliamua kuacha shule kwa kumpiga kiti mwalimu lakini anatamani wanawe wasome na kuitwa Doctorate / professor.

Think big maaaan... !!
Anatamani ila Ki uhalisia kelele unazobiga huku hatuna hela yeye hapigi,tuendelee kujifariji tu.Ila ana Elimu ya michezo amabyo wengi mnai dharau mnaishia tu kukariri kusoma ni hesabu tu za logic ambazo hata wanasoka wanazitumia kwa namna yao.Tunaakariri tu utaratibu wa huo huo...ona PHD zilipo tupelekea.Nenda NBA kule,Mwangalie huyo huyo Ronaldo,Messi kisha jitafakari kuwa mnafanana hata kama una hiyo PHD?Mtu wa miaka 30 kimechezo huwezi fananisha kima slahi na mtu mwenye miaka 30 huku kwetu.Wachache sana,ndio maana Extended Family haziishi kwa kuwa hatujaelewa TAFSIRI ya Elimu.
 
Huu ni mtazamo tu na nauheshimu binafsi watoto wangu ile wanayoita Elimu ya msingi watasoma English Medium harafu za sekondari watasoma tu hizi za kawaida kwa kuwa watakuwa wameshapata msingi hasa lugha hawatosumbuka na kikubwa ni kuwajengea tu uwezo wa kupenda kujisomea na kurudia mara kwa mara wanayofundishwa shuleni. Mimi siwezi acha kuwasomesha watoto elimu bora eti kisa watakosa mikopo Noo!! Itajulikana tu huko huko by the way sio lazima wafike Chuo kikuu wanaweza komea hata Diploma zinawatosha degree zipo tu
Mimi pia hili ndilo lengo langu kuu la kuwapeleka wanangu english medium Sekonfari watasoma hata za kata. madam wana msingi mzuri wao mbele watajipanga. shida inakuja hali ya kiuchumi upepo umegeuka ghafra na hela hakuna. hivyo unajikuta unafanya maamuzi magumu. ila nashauli asitoke english medium akaenda kayumba. bali atoke shule ya ada kubwa aje ya chini zaidi kulingana na kipato chako. mfano alikuwa Tusiime mrudishe St Nicholau ya 1.5m
 
Back
Top Bottom