Mnaosomesha watoto English Medium pokeeni maua yenu

kocha Nabi

JF-Expert Member
Feb 1, 2022
590
1,466
Watu wengi hawafahamu kwanini wanapeleka watoto wao English Medium, wengi wanaamini ni sehem sahihi ya kupata elimu nzuri, ama kwavile mtu unapesa acha uwaoneshe watu anazo kwa kupeleka watoto wake shule hizo.

Sababu kuu ni moja tu ambayo sitakaa niisahau, katika harakati zangu kipindi natoka kumaliza chuo nilipata kijikazi cha kufundisha watoto wa tajiri mmoja hivi biashara zake anafanya South Africa, lakini familia yake inaishi maeneo ya Kurasini.

Ilikuwa kipindi cha likizo kwa watoto wake wawili na mimi nikapewa ratiba ya kwenda kuwanoa, sasa wakati nimemaliza kufundisha kwa siku hiyo, tukawa tunapiga story 2 tatu na huyu faza na katika maongezi yetu alikuwa very exited na historia yangu na kufanya kuita wanae kuwapa maneno ya hekima.

Neno moja kuu ambalo nimelielewa ni kuwasisitizia watoto wake kuwa, amewapeleka shule zenye hela ili wakakutane na watu, waweze kujenga connections. Nilimuelewa sana yule mzee.

Hii dunia imechange pakubwa, zamani watu wa familia maskini waliosoma ndio walibahatika sana kupata post za juu kwenye ajira ama makampuni lakini kwa miaka hii, matajiri huekana wao kwa wao ili kusecure their buzness, kurahisisha shida zao n.k

Ni rahisi kufanikiwa katika hii nchi kama unafahamiana na watu wa maana, na hao watu asilimia kubwa hawapatikani shule zetu za kata, tusije kujifariji kwenye ufaulu.

Hoja kuu ni connection.
 
Ni rahisi kufanikiwa katika hii nchi kama unafahamiana na watu wa maana, na hao watu asilimia kubwa hawapatikani shule zetu za kata, tusije kujifariji kwenye ufaulu.

Hoja kuu ni connection.
Kwa kuongezea tu ni kwamba, connections siku zote hazilazimishwi, hususan watu kama sisi wa kipato cha chini. Connections zinakuja automatically tu. Ishi jinsi Mungu alivyokuumba, kisha wale wanaofanana na wewe watakuja katika maisha yako. Kamwe usiigize tabia ili upate connections.
 
Hata maandiko yanasema bora ufahamu (akili & maarifa). Bora kukubali kugharamika sasa kwa faida ya miaka mingi

Mithali 4 (Biblia Takatifu)
⁷ Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
⁸ Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
⁹ Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.
 
Kwa kuongezea tu ni kwamba, connections siku zote hazilazimishwi, hususan watu kama sisi wa kipato cha chini. Connections zinakuja automatically tu. Ishi jinsi Mungu alivyokuumba, kisha wale wanaofanana na wewe watakuja katika maisha yako. Kamwe usiigize tabia ili upate connections.
Uko nyuma ya muda. Huu ushauri mtu akiufuata lazima afe maskini.
 
Kwa kuongezea tu ni kwamba, connections siku zote hazilazimishwi, hususan watu kama sisi wa kipato cha chini. Connections zinakuja automatically tu. Ishi jinsi Mungu alivyokuumba, kisha wale wanaofanana na wewe watakuja katika maisha yako. Kamwe usiigize tabia ili upate connections.
Kabisa. Yaani unaweza kuwa chawa kwa mtu mwenye hela ili upate connections lakini yeye anakupotezea kwa sababu zake anazojua yeye mwenyewe, mfano anahisi utamzidi au kama unauelewa wa mambo ndio kabisa anakuogopa.

Ukiendekeza uchawa utajikuta unakuwa mtumwa kwakweli.

Dawa ni kupambana halafu connections zinakuja automatically!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante ka mkubwa, pia kuna kitu kinaitwa personality kwa introverted kama mimi hata ningesoma international school na watoto wa mawaziri, ningetoka mimi kama mimi huwa siamini katika connection, the right people to me will be right by my side for the right time, I always stay real.
Be who you are mengine mwachie Mungu
 
Kabisa. Yaani unaweza kuwa chawa kwa mtu mwenye hela ili upate connections lakini yeye anakupotezea kwa sababu zake anazojua yeye mwenyewe, mfano anahisi utamzidi au kama unauelewa wa mambo ndio kabisa anakuogopa.

Ukiendekeza uchawa utajikuta unakuwa mtumwa kwakweli.

Dawa ni kupambana halafu connections zinakuja automatically!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Tena ukiwa na miakili mingi ya kuzaliwa wanakuogopa sana na kukuchukia maana wanajua if you get the chance they have utawaacha mbali. Wakishua wengi wana upepo wa hela ila upstairs their not talented, na ukiona anakusaidia kitu its a trap, anataka akuangushe
 
Hapa unaelezwa umuhimu wa subra man,niamini alichoandika hapa ni sahihi na kiko mbele ya muda
Subra haipo namna hio, Subra ni kutenda jambo then unasubiri sio kulala kisubiri....jamaa kaandika anajenga connection then jamaa anakujasema wewe kaa tu connection zinakuka zenyewe kwahio hio ndio subra.
 
Kulazimisha kujenga connections sehemu ambazo hawakutaki ndio chanzo cha vitendo vya aibu kwa vijana.
Unaandika vitu ambavyo avipo kwa kulazimisha sana wapi mtoa mada kaandika kulazimisha connection, kisomesha mtoto shule ya maana hili ajenge connection kwako ndio kulazimisha connection sehemu ambazo hawakutaki.

Emu soma mada na rejea reply zako zote umeandika ujinga Sana.
 
Back
Top Bottom