Niache kula kuku Sea Cliff kisa kupeleka watoto English Medium?

Mimi pia hili ndilo lengo langu kuu la kuwapeleka wanangu english medium Sekonfari watasoma hata za kata. madam wana msingi mzuri wao mbele watajipanga. shida inakuja hali ya kiuchumi upepo umegeuka ghafra na hela hakuna. hivyo unajikuta unafanya maamuzi magumu. ila nashauli asitoke english medium akaenda kayumba. bali atoke shule ya ada kubwa aje ya chini zaidi kulingana na kipato chako. mfano alikuwa Tusiime mrudishe St Nicholau ya 1.5m
Ni kweli wa kwangu watasoma Sekondariza serikali zile nzuri sio za kata lakini,zipo shule nzuri tu mfano hizi za boarding ni kweli uchumi umebana sana kwa sasa ila hakuna namna wa kwangu lazima wasome
 
Mengine fanyia utafiti hata wewe mwenyewe, si umeshapata pa kuanzia!?.
Chukua mtaala wa UK na Tz ilinganishe!.
Ndugu hiyo mitaala sijui ya UK sijui Cambrige ni aibu tupu. niliona scenario moja kitabu kinaelezea what is a familly kwa hiyo mitaala. utakaa chini ulie. kwetu familly ni baba mama watoto kwao ni nuksi bora hata nisielezee ni aibu.
 
Mkuu uko sawa kabisa ila kwa kuongezea, waachishe kabisa shule wabaki nyumbani..
Kama una masterz wafundishe tu mwenyewe kila siku na vidato unawapangia mwenyewe utakapoona inafaa unawapa degree tu kabisa..
 
Hongera kwa masterz mkuu, ila ni muhimu kusomesha mtoto shule nzuri kama uwezo wa kusomesha unao.
Mleta mada mpeni ushauri kuwa mnazaa watoto wanini msioweza kusomesha MTU kama wewe ulitakiwa uhasiwe. Maana una faida duniani na unazidi kuleta majanga apa duniani
 
Ndugu hiyo mitaala sijui ya UK sijui Cambrige ni aibu tupu. niliona scenario moja kitabu kinaelezea what is a familly kwa hiyo mitaala. utakaa chini ulie. kwetu familly ni baba mama watoto kwao ni nuksi bora hata nisielezee ni aibu.
Ielezee what's Family according to wao!.
Utamaduni wa mwafrika kukaa na extended family wanao pia ingawa hawaufanyi sana!. Mambo ya kuja kwangu kujaza watoto wako ni kuniletea umasikini mie na watoto wangu!.
Haiwezekani uzae kama wewe pekee ndio unaweza shughuli matunzo tufanye wengine!..
 
Wewe kula kuku, ushibe, ukajisaidie chooni, mwishowe upate diabetes ujifie bila kuacha legacy, endelea kuinvest hiyo hela chooni, shule za private si tu zinafundisha kiingereza bali zina mtaala ulio na msimamo unaofanana na ambao haujatikiswa wala kubadilishwa ovyo maana ni wa kimataifa sio kama wa shule za serikali unaochezewa kila kukicha na siasa zenye mipango mibovu kila anapobadilishwa waziri, lifespan yako si kubwa kama unavyodhani, hata ukiinvest kwenye hizo tofali ili waje waishi wanao ambao katika elimu yao wamepigwa danadana ya mitaala isiyoeleweka na wamekosa self confidence/communication skills..wataziuza tu zote na legacy yako in this world inafia pale. Enzi zetu shule za serikali zilikuwa na mtaala ulioimara na usiotikisika na umetujenga kwelikweli, hauwezi kuufananisha na hizi mishmash zinazoendelea sasa na kuwachanganya watoto. Moja ya raha duniani ni kuona wanao uliowazaa pia wanafurahi na maisha na wanaishi the best life na wanapata mahitaji yao vizuri kabisa ikiwemo elimu in the best school kulingana na kipato chako, ukikosa uwezo sawa, ukiwa nao usiwe mchoyo wala mbinafsi kwa damu yako mwenyewe, kipato ulichopewa kina kazi yake maalumu kulingana na mahitaji yako. Wazazi wakatili wasio na maadili na washenzi hutengenezwa utotoni na si ukubwani. Wewe muombe Mungu akutimizie mahitaji yako akupe riziki usomeshe watoto wako shule nzuri na si za kubahatisha, wacha ubinafsi, hata huyo mkeo anaweza kukusuprise wakati wowote ukashangaa! ati mtumbue na mkeo halafu upeleke watoto saint kayumba na uwezo wa kuwapeleka HOPAC unao..badilika..acha mawazo mtindi! Mungu akubariki!
 
Ndugu hiyo mitaala sijui ya UK sijui Cambrige ni aibu tupu. niliona scenario moja kitabu kinaelezea what is a familly kwa hiyo mitaala. utakaa chini ulie. kwetu familly ni baba mama watoto kwao ni nuksi bora hata nisielezee ni aibu.
Which book and what does it say?
 
Which book and what does it say?
Na kabla hujaendelea mimi nimesoma shule za serikali, ila nilikuwa agent/supplier wa vitabu vya mtaala wa Cambridge kwa miaka 8 hapa nchini kwa shule nyingi ikiwemo IST. Sasa tueleze hapa kitabu gani, cha somo gani katika mtaala wa Cambridge unachokiongelea na kimeandikwa nini kuhusu tafsiri ya family.
 
Mkuu

Mie nishamwambiaga baba,kama alishindwa kuenjoy pesa z baba yake ni yeye kila Mimi wacha nienjoy za baba yangu,

Mtoto anatakiwa afaid matunda ya Mzee sasa kama baba yako alikuwa masiki mkosi n kwako usipeleke matatizo ya baba yako kW wanao

Wanao wana baba mwenye elimu na pesa ya kuwapeleka shule zenye schools bus kwann wasienjoy

Wewe mbaba acha wivu kwa wanao
 
Sitaki kabisa kuona wanangu wakiishi masha ambayo baba yao nimeishi, yani kisa wakati nasoma nilitembea peku basi nao waende peku shule?

Kisa nilikuwa natembea kilometers 10 kwa siku basi nao watembee hizo hizo?

Haya Maisha yako mkuu utakuwa unalipa kisasi kwa wanao sio bule.
Umenichekesha,analipa kisasi cha wazazi wake kwa wanae
 
Umenichekesha,analipa kisasi cha wazazi wake kwa wanae

Mkuu ni dhahiri shahiri ni kisasi, kama huna pesa sawa lakini pesa unazo unaenda kula bata Serena hoteli wanao wanasoma shule za kata eti Lisa na wewe ulisoma kata.

Watu tunafaiti kutafuta pesa ni kwa ajili ya familia zetu nikiwemo watoto waishi kwenye mazingira bora na wasome mazingira mazuri tofauti na uliyosoma wewe.

Ila Maisha lazima yaendelee kila mtu na choice yeke mkuu kaamua Maisha yake ayaendeshe kwa staili, ila kwa upande wangu hapana.
 
Back
Top Bottom