Kwa ujinga wa wagogo watamchagua tena kwa kishindo njaa yao kubwa ni ubwabwa na choya.
Wadau naomba tuziweke pembeni siasa katika kujadili mada hii, tuweke michango yetu kwa nia ya kulitimiza hili....maneno aliyoongea Mbunge Lusinde yametugusa sana sisi wanaharakati wa haki za watoto, ukizingatia kwamba kulikua na watoto wadogo pale ambao waliyasikia..technically, he did abuse those children..kwa hilo basi, tuna nia ya kulifikisha shauri hili katika vyombo vya sheria ili wanasiasa au watu wenye tabia ya kuongea offensive and abusive words mbele ya watoto wafahamu kwamba watawajibika kwa matamshi yao kisheria!
1. tunaomba weledi wa sheria za kitaifa na za kimataifa; hasa katika Child Rights' watoe mwongozo katika hili...
2. tunaomba wakazi wa Arumeru, waandishi wa habari, au yeyote aliyehudhuria mkutano ule awe tayari kutoa ushahidi, ikibidi mahakamani...
3. tutashirikishana katika kila hatua itakayoendelea katika hili..
3. ikibidi tuwe tayari kwa michango ya hali na mali ili kufanikisha jamobo hili....
Mwisho; tukumbuke kwamba mtoto wa mwenzio ni wako........nakaribisha michango na ushauri...