Ni zipi taratibu za uhamisho wa kubadilishana?

Taiq

Member
Feb 14, 2023
83
71
Ndugu walimu wenzangu na wanajanvi naomba mnisaidie taratibu za kufuatwa ili mwalimu asainiwe barua za uhamisho wa kubadilishana kituo cha kazi.

Nimeamua kuwauliza swali hili kutokana na halmashauri ya wilaya ya Ngara ninayofanya kazi kugomea kusaini barua zangu wakidai mpaka niambatanishe nakala ya barua za mwalimu mwenzangu ambaye ninabadilishana naye kituo cha kazi na ziwe ni zile zilizosainiwa na mkurugenzi wake.

Je, ikitokea na na mwenzangu akaambiwa ambatanishe na za mwenzio. Sijui ndo itakuwa mwisho wa uhamisho au hili linafanyika kuwakomoa walimu. Lakini kiujumula ulasimu ni mkubwa sana hapa Ngara sasa sijui halmashauri nyingine hali ni kama hii ya Ngara au Ngara inasheria zake na miongozo yake ndani ya Tanzania?

Tafadhali unapochangia jenga hoja na usitumie lugha chafu.
 
Back
Top Bottom