Tanga: Uhamisho MAALUM Kilindi walimu wamesharipoti vituoni mwao.

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
856
1,006
Habari za muda huu.

Ni habari njema wale walimu wa Parakuyo kule Kilindi tayari wamesharipoti vituoni mwao walipopangiwa kwa barua walizopewa tangu tarehe 03.11.2023.

Ombi langu kwa mamlaka zinazohusika walimu hawa walipwe stahili zao za uhamisho ili mapema ndani ya desemba hii wahamishe familia zao na kadhalika.

Walimu hawa walipomaliza kuripoti vituoni mwao waliandika barua za madai na walishapeleka hizo barua ofisini Halmashauri ya Kilindi tangu wiki ya pili ya November lakini hawajapata majibu hayo mpaka leo.

Walipoulizwa na walimu wenzao wa Handeni walioanza kuripoti Parakuyo walisema hawataondoa vyombo vyao Parakuyo mpaka watakapolipwa stahiki zao.

Aidha hakuna mwalimu hata mmoja alieandika barua ya kutaka kubaki Parakuyo.Zaidi walimu hao wamekiri kuathirika kisaikolojia kutokana na uvumi ya kuwa wametakiwa kubaki wote Parakuyo.

Naibu waziri alitoa tamko bungeni walimu hao mpaka ifikapo tarehe 30 Desemba 2023 wawe wameripoti vituoni mwao baada ya mbunge wa Handeni Ruben Kwagilwa kutaka kujua lini walimu wa Handeni na Kilindi watapewa barua za uhamisho?

Walimu hawa wa Parakuyo walihamishwa wote shule nzima baada ya shule yao kuhamia Handeni Mji kutokana na mabadiliko ya kimipaka yaliyomalizwa na mkuu wa mkoa wa Tanga mnamo Julai 2023.

Nitawaletea updates kuhusu Jambo hili mara kwa mara.
 
Habari za muda huu.

Ni habari njema wale walimu wa Parakuyo kule Kilindi tayari wamesharipoti vituoni mwao walipopangiwa kwa barua walizopewa tangu tarehe 03.11.2023.

Ombi langu kwa mamlaka zinazohusika walimu hawa walipwe stahili zao za uhamisho ili mapema ndani ya desemba hii wahamishe familia zao na kadhalika.

Walimu hawa walipomaliza kuripoti vituoni mwao waliandika barua za madai na walishapeleka hizo barua ofisini Halmashauri ya Kilindi tangu wiki ya pili ya November lakini hawajapata majibu hayo mpaka leo.

Walipoulizwa na walimu wenzao wa Handeni walioanza kuripoti Parakuyo walisema hawataondoa vyombo vyao Parakuyo mpaka watakapolipwa stahiki zao.

Aidha hakuna mwalimu hata mmoja alieandika barua ya kutaka kubaki Parakuyo.Zaidi walimu hao wamekiri kuathirika kisaikolojia kutokana na uvumi ya kuwa wametakiwa kubaki wote Parakuyo.

Naibu waziri alitoa tamko bungeni walimu hao mpaka ifikapo tarehe 30 Desemba 2023 wawe wameripoti vituoni mwao baada ya mbunge wa Handeni Ruben Kwagilwa kutaka kujua lini walimu watapewa barua?

Nitawaletea updates kuhusu Jambo hili mara kwa mara.
sijaelewa ilikuwaje huo uhamisho wa wilaya yote
 
Back
Top Bottom