Ni yupi MwanaJF bora kwa mwaka 2022

Ni yupi MwanaJF bora kwa mwaka 2022

Kama agera 1 hayupo huu Ni utapeli
Mwaka unakaribia kuisha ni wazi kwamba wapo wana JF wengi walijitokeza na kufanya vizuri au kuchangamsha kutokana na mada au michango yao mbalimbali.

Baadhi ya wa JF wameonekana kufanya vizuri zaidi kwa mwaka huu, unadhani ni nani anastahili Tuzo ya mwana JF bora kwa mwaka 2022, kwa upande wangu ningechagua miongoni mwa wafuatao;

1. Mshana Jr - Hujitokeza katika majukwaa mbalimbali kwa kuchangia au kutoa mada, ni mzuri sana kwenye mada za Dini na za Sayansi ya asili.

2. Paschal Mayalla - Pamoja na kujipambanua itikadi yake kisiasa lakini haiondoi ukweli kuwa mada na michango yake ili elimisha wengi.

3. Gentamycin - Hushambuliwa na baadhi ya wana JF kila anapotoa uzi, lakini haiondoi ukweli kuwa alikuwa bora kwa mwaka huu, anastahili Tuzo.

4. Erythcrote- Mwana CHADEMA kindakindaki, hujitokeza pia kwenye majukwaa mengine hasa michezo, amekuwa mwana JF mzuri kuharisha members wengine kwa mwaka huu, naona pia anastahili Tuzo.

5. MK254 - Kwenye vita ya Urusi na Ukraine amekuwa akitoa breaking news kila inapotokea ingawa ameegemea sana upande wa Ukraine.

6. Okwi Boban Sunzu - Hupatikana sana kwenye michezo akiisapoti timu yake ya Simba na pia Siasa akikisapoti chama chake cha Chadema, alikuwa member mzuri mwaka huu.

7. Sky Eclat - Ni mwanamama mwenye madini mengi kichwani na amekuwa akiyatoa bila shida kwa wana JF.

8. Umughaka - Story zake za kusisimua zimewaburudisha na kuwafundisha wengi kungekuwa na Tuzo angekuwa miongoni mwa wanaowania.

9. Victoire - Yeye pia ni miongoni mwa wana JF alitamba kwenye majukwaa mbalimbali mwaka huu.

10. Mpwayugu village - Mtaalam wa story ingawa zingine zilikuwa hazifiki mwisho.

11. Shaadeya - Mwana Yanga lia lia, yeye na Yanga yake.

12. Bujibuji - Amechangia sana kwenye majukwaa mbalimbali bila kumdhihaki mtu.

13. Rickboy - Sijui kama nimepatia spelling, huyu yeye kwenye Jukwaa la kugegedana amepakamata.

14. Mzee Mohamed- Jukwaa la Historia ni kama lake, amekuwa akishusha nondo za uhakika, ingawa anashutumiwa kwa kupendelea Dini yake.

Kwa upande wako unadhani nani anastahili Tuzo hii kama ingekuwa inatolewa?
 
Kwa hio wewe umeangalia stori na majukwaani unayopenda tembelea ndo ukawapanga hao watu,, Kuna wabobezi maswala ya tech na kule jf garage Sasa wewe unaleta watu wa stori Nyingi hizo habari za mchepuko kafanya hivi kafanya vile ndo kigezo Cha mtu kuingia kwenye hio list , Africans tunatabu Sana


Viva morroco usikubali kushangaliwa na watu weusi Ni laana
 
Kwa hio wewe umeangalia stori na majukwaani unayopenda tembelea ndo ukawapanga hao watu,, Kuna wabobezi maswala ya tech na kule jf garage Sasa wewe unaleta watu wa stori Nyingi hizo habari za mchepuko kafanya hivi kafanya vile ndo kigezo Cha mtu kuingia kwenye hio list , Africans tunatabu Sana


Viva morroco usikubali kushangaliwa na watu weusi Ni laana
Ni maoni ya mtu unaweza kutoa pia maoni yako
 
Back
Top Bottom