Mkuu unashindwa kujiongeza??!!, kazi ya nyonyo za kiume ni kunyonyeshea mtoto kama jinsi mama anavyonyonyesha, tofauti ni hii kwamba nyonyo za mama hutoa maziwa lakini za baba hazitoi.
Ni hivi, kazi ya kulea mtoto anapokuwa katika umri wa kunyonya (miaka 0- 2) ni ya wote wawili mama na baba ila zaidi ni ya mama, inapokuwa ni kazi ya baba ni wakati ambapo mama anafanya shughuli fulani ambapo hawezi kuambatana na mtoto hapo ndipo zamu ya baba kuwa na mtoto inapofikia, sasa kwa wakati huo inapotokea mtoto akaanza kulia ndipo baba anatakiwa ampe nyonyo ili kumyamazisha kusubiri hadi mama aje, kwa maneno mengine unaweza sema nyonyo za baba ni nyonyo bandia (dummy nipples) kwa kazi hiyo.
Kutokana na hali za maisha na maendeleo ya mwanadamu na mazingira ndipo badala yake kulikuwa na "dummy nipples" za kutengeneza na hata chupa za maziwa (ya ng'ombe au ya kopo) kama mbadala wa nyonyo za wanaume. Hiyo ndiyo Kazi ya nyonyo za wanaume, lakini ni watu wachache mno wanaojua jambo hilo.
Ni mbilikimo wa kiume wa Misitu ya Congo DRC (Congo pygmies) ndiyo wanaofahamika kutekekeza jambo hili la kunyonyesha watoto katika mazingira niliyoyataja.